matayarisho ya mwisho kabla duka la Chocolate Princes Boutique halijafunguliwa rasmi leo jijini Dar. Lipo Mikocheni karibu na Kwa Mwalimu kwenye maduka mapya katika jengo la kiota maarufu cha 'Talk of Town' katika barabara iendayo Rose Garden.
mmiliki wa Chocolate Princess Boutique, Mboni Masimba, anasema kwa kuwa kinababa wamekuwa wakilalamika sana kwamba viatu vyao vya uhakika havipatikani kwa wingi jijini sasa yeye ameamua kumaliza kiu yao sehemu ya kago la viatu vya kila aina na rangi toka italy. mboni anasema ukitaka maelezo ya kina mpigie tu kupitia namba +255 773 787 272


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2009

    upo juu babyboo kaza sana msuli then mbio sana don't look back,manikizz,athens,GREECE

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2009

    big up mamie, kumbe Barcelona ni kati ya maandalizi ya kitu cha nguvu namna hii? Safi sana

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2009

    mtoto wewe, unaakili, kama mama yako, kaza msuli, bora umerudi bongo na kuanzisha biashara na sisi tutafuta baada ya kupata mtaji wa kubeba box.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2009

    Jamani Tanzania tutaendelea kuwa soko la bidhaa kutoka nje hadi lini? Hizo ngozi tulipeleka kama mali ghafi kwa bei ndogo, sasa nenda kaulize bei ya hicho kiatu. Mungu tusaidie

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 24, 2009

    Tunataka na pia vinavyotengenezwa hapa nchini.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 24, 2009

    baab kubwa !!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 24, 2009

    Ili mkikwamua kutoka ku bu maskini, Watanzania, achaneni na uwakala wa vya kutoka nje. Inueni vyenu

    Ciao

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 24, 2009

    gud luck sis

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 25, 2009

    kubeba box mchezo?kina mabastola wamehonga msingi huo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 25, 2009

    ungezidisha muda kidogo ungekuja kujenga ghorofa kule italy madem dili.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 25, 2009

    ungezidisha nuda kidogo ungekuja kujenga gholofa italy mademu dili kule.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 25, 2009

    Vumbi la Dar na viatu vya Italy haiji. Best wishes lakini.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 27, 2009

    Hongera sana dada. Wanadamu hatuna jema. Si tumsifie tu kashfa hazijengi na ndio maana hatuendelei. Anayetaka na viatu vya bongo wachonga viatu wapo kuna mhindi anachonga viatu yupo opposite na Burhani hospital. Kama hutaki kununua kwa mhindi nenda Morogoro road kuna wa Tz wenzetu wanaochonga viatu pia. Pia wapo wanaovihitaji hivyo vya ITALY wengi tu.

    ReplyDelete
  14. jamani huwezi kumchagulia mtu kitu roho inapenda,kuna wanaopenda bling bling, pia wanaopenda za wachina, waingereza,south africa,bara hindi,basi muacheni huyu dada anajaribu kuwakonga roho wale wanao penda style ya kitaliani na mwenye huwezo basi hatuletee za kutoka ufaransa hata za spain tutanunua.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...