
Kwa heshima na taadhima tunawaalika Watanzania wote popote walipo pamoja na watu wa mataifa yote kuhudhuria sherehe za jadi za Mwaka Kogwa tarehe 20.07.09 zitakazofanyika huko Makunduchi, Wilaya ya Kusini, Mkoa wa Kusini Unguja.
Sherehe zetu zinachukua siku nne; siku ya kwanza, ambayo huwa kivutio kwa watu wengi, huanza na mapigano yanayoanza kuanzia saa 5 Asubuhi katika eneo liitwalo Kae Kuu, katikati ya mji wa Makunduchi.
Mapigano hayo hukutanisha Wamakunduchi wanaoishi upande wa Kusini na wale wanaoishi upande wa Kaskazini. Silaha inayotumika ni makoa ya migomba. Zamani bakora zilitumiwa. Lengo la mapigano ni kujaribu kuondoka tofauti au uhasama wowote ule uliotokea miongoni mwa Wamakunduchi kutoka pande hizo mbili kwa kipindi cha mwaka uliopita ili kuanza mwaka mpya bila ya chembe ya uhasama ya mwaka uliopita.
Mila hii husaidia sana watu wa Makunduchi kuishi kwa mapenzi na mshikamano. Baada ya mapigano ambayo huishia kwenye saa 8 mchana watu hurejea nyumbani ambako chakula kizuri kimeandaliwa. Kimila chakula hicho cha mchana huliwa nje ya nyumba ili kutoa nafasi kwa wageni kujumuika na wenyeji.
Wakati wa usiku sherehe huendelea kwa ngoma, disco na mambo kama hayo katika viwanja vya sehemu iitwayo Koba, karibu na kituo cha Polisi. Kwa maelezo zaidi angalia mtandao wetu wa kijiji cha mzuri, miongoni mwa vijiji vya Makunduchi:
http://www.mzuri-kaja.or.tz
Kwa waandishi wa habari na watafiti wanaweza kuniandikia kwa kupata maelezo ya ndani ya namna nzuri ya kupata habari za kutosha za mwaka kogwa Jina:
Mohamed Ameir Muombwa
mmuombwa@hotmail.com
mobile: 0773539504
Karibuni nyote Makunduchi kusherehekea
mwaka mpya wa watu wa Makunduchi.
hello kaka,
ReplyDeleteZanzibar is full of suprise, Mwaka Kogwa na kila kitu.
Art and music is moving to the next level.
zumari people in the middle of modern life.
mwaka kogwa, maajabu ya tamaduni.
Tazama hii:http://www.youtube.com/watch?v=lwimCclZP74
and more to come
Sekibaha
Ndio ni utamaduni lakini ni ushirikina mkubwa. Ni mabaki ya waarabu kutoka shirazi. Ni ibada inayojulikana kama namruz. Ni ibada kwa wasioamini Mungu wanaoamini nguvu za moto.
ReplyDeleteKama mcha Mungu hiki sio kitu cha kushangiria.
Nashukuru kwa kutuelimisha, lakini ni vizuri pia katika mambo kama haya waandaaji mkawa wawazi na hasa kuhusu gharama.
ReplyDeletekwa mfano mimi nimevutiwa sana na sherehe hizi na najiisi kuwepo mahari hapo,tatizo ni kuwa sijui nitafikaje sehemu hiyo. hivyo kukiwa na taarifa sahihi itasaidia sana mtu kujua na hasa gharama za maradhi na huduma nyingine kwa siku nne.
mila za kiafrika zidumu
ReplyDeletemila za kitanzania zidumu...
ila hope ukimwi hausambazwi maana..
safi sana
asante
Kutunza mila ni kitu kizuri ILA kaka Muombwa jaribuni sana kudhibiti mambo ya kihuni wakati wa mwaka kogwa (kuvuta bangi, unga, ulevi wa kupindukia na ukahaba unakithitiri sana). Tathmini yangu ni kwamba watu wengi wanaokuja ktk sherehe hizi wanavutiwa na kuja kufanya ngomo ama matendo machafu. Beach ya makunduchi ni bomba sana na watu wanatumia vichaka na beach kumaliza haja zao. Hata pale ktk vichaka vyenye mzimu utaona kondom zimezagaa!!. Pia ni kwa kiasi gani wananchi wa makunduchi wanafaidika (kiuchumi) bada ya sherehe hii, think strategically ili ila baada ya sherehe kuwe na mradi wa maendeleo umetekelezwa kutokana na matunda ya sherehe zenyewe.
ReplyDeleteMdau
Zanzibar
Naam, tamaduni za kirani zadumishwa Afrika Mashariki!
ReplyDeleteMuoge vyema!