Habari mdau Nanihii,
Pole na majukumu ya kila siku. Napendelea sana blog yako.
Mimi nina kero yangu kuhusu hizi ATM za mabenki zetu Kama tunavyojua kuwa ATM zimewekwa ili watu waweze kupata fedha kwa urahisi na kwa muda wowote. Sasa ijumaa ya wiki iliyopita mimi pamoja na mume wangu tulipata emergency flani hivi, ikabidi tutoke home mkuku kwenye mida ya saa tano usiku kwenda kwenye ATM pale myfair.
Tulikuwa na sh elfu 5000 mfukoni na ndio tuliyochukulia taxi kutoka sinza mpaka pale. Sasa tulivyofika pale tukakuta myfair wamefunga mageti na maasakari hawataki kufungua. Wanadai kuwa uongozi wa myfair hauruhusu mtu kuingia ndani zaidi ya saa 4 usiku. Imagine jinsi ambavyo tulikuwa hatuna hela na emergency ambayo tulikuwa nayo yaani nilipata hasira mpaka nikahisi kuchanganyikiwa.
Nikashindwa nini cha kufanya. Zaidi ilibidi nichukue taxi tena mpaka kinondoni kwenye HQ zao. Nikajaribu kuongea na hao walinzi wakasema haiwezekani wao kuniruhusu kuingia ndani kwani hairuhusiwi, nikawaambia kuwa nini maaana ya ATM? Maana ninavyojua mimi kuwa ATM inatakiwa kuwa wazi 24hrs na ndio maana ikawekwa pale.
Sasa mdau nisaidie swala hili maana limeniudhi kupita kiasi maana emergency ndo kama hivyo imetokea mfukoni huna hata shilingi then unakwenda kwenye ATM unakuta mambo kama haya. Je ungekuwa ni wewe ungefanyaje??
Na hiyo benki kwani walikuwa hawajua kuwa pale myfair wanafunga mida hiyo? Na kama alikuwa anajua kwanini asingeweka hiyo ATM yao kwa nje ili iwe rahisi kwa watu kama sisi tunaopata emergence za gafla? Maana ukienda benki hiyo wanakwmbia kuwa ATM zao ziko 24hrs popote pale walipoweka ATM zao.
Sasa maana yake nini kutufungia tushindwe kutumia hizo ATM? Mdau kweli hili jambo limeniudhi sana.
Mdau jina na email yangu viweke kapuni tafazali, na pia unaweza kuiweka hii msg isomeke vizuri maana nimeiandika haraka haraka tena kwa hasira. Aaaarghhh!
Mdau Mkereketwa
Pole sana mdau. Ninashukuru hii mada umeileta hewani. Kwa kawaida huwa nakwenda gym hapo Mayfair kila asubuhi, maaskari hao hao waliowazuieni hukataza mteja yeyote wa taxi kuchukuliwa ndani kabla ya saa tatu. Sijui huu utaratibu wao umetoka wapi. Ukiingia na gari lako ni sawa ukiwa unafuatwa na taxi si sawa. Naamini wahusika watalishughulkia. Once again pole.
ReplyDeleteMdau
Mimi sijaelewa vizuri ujumbe wako. Hizo ATM ni za benki gani? Ni za benki inayoitwa mayfair plaza au? Nauliza hivyo kwa sababu kuna ATM nyingi zipo nje (namaanisha hazijafungiwa na mlango) na zipo accessible kwa muda wote ingawa kuna walinzi
ReplyDeletePole sana mkereketwa,
ReplyDeleteKijijini kwangu ATM ziko maeneo ya wazi yenye usalama na yanatofikika muda wote.
Wakulaumiwa ni uongozi wa Mayfair na sio walinzi, kwani wao wanafuata maagizo.
Aidha, benki zinatakiwa kufuatilia malalamiko ya msingi kama haya ili kuhahakikisha lengo halisi la kupata huduma muda wowote toka kwenye ATM linazingatiwa.
Mdau
Faustine
http://drfaustine.blogspot.com/
Simpo
ReplyDeleteTafuta mwanasheria, chukua picha za ushahidi na majina ya hao askari waliokuwa doria then sue hiyo bank kwa kuweka matangazo ya uwongo...
Bongo saa yingine.aaaa ama hakika Bongo tambarare
ReplyDeleteKwanza umesema wewe ni mdau mkuu wa hii blog, naweza kukubali, ila napenda pia kukuhabarisha kuwa nanihii yeye sio mdau, wewe , mimi, yule na wao ndio wadau na sio yeye.
ReplyDeletenanihii yeye ni mzee wa libeneke.
kuhusu kauli uliyotoa ni wazi kwamba walinzi lazima watakuwa wamefuata sheria kama mdau hapo juu alivyonena, nakushauri wasiliana na uongozi wa benki ( nina uhakika lazima ujumbe utakuwa umewafikia ingawa hujataja kuwa ni ATM ya benki gani )na kisha wasilisha malalamiko yako kwao.
nina uhakika hiyo ATM ama itahamishwa, au la itakuwa wazi masaa 24 kama ujumbe wa benki unavyojieleza.
natanguliza shukrani zangu.
Mdau Nguli!
Mdau madai yako ni sawa lakini hayabebi obligation yeyote kwa upande wa benki husika. Hoja yako itakuwa na nguvu tu pale utakaposema kuwa ATM zote za benki hiyo haziwezi kuingilika kwa masaa 24.
ReplyDeleteKwa kawaida ATM iliyopo ndani ya eneo maalum is subject to some limitation na hili si bongo pekee hata katika nchi kubwa duniani mambo ni kama hivyo.
Endapo ATM ipo ndani ya store au eneo linalodhibitiwa kwa muda maalum huwezi kuwaambiwa wakufungulie kwa ajili ya kutumia ATM. Sijawahi kuona mlango wa Mall inafunguliwa usiku ili mtu aende kwenye ATM
Ushauri wa bure uwe unaangalia kwanza ATM unayotaka kwenda iko ndani ya eneo linalodhibitiwa au la?
Bongo tambarare??Nani kasema?Yaani mambo kama haya ya kijinga jinga,ndio maana nakata tamaa kuja kuishi home.Kiwanja saa tisa usiku naibuka kwenywe atm bila kokoro na mshiko wangu mkononi.Don't get me wrong najua waosha vinywa mnakuja..
ReplyDeleteWe have a long way to go Bongo.Michuzi usibanie maana na wewe!
Mama nimekupata. nakushuku kwa kuchukua hatua ya kuto kero yako. tatizo la ATM hapo Tanzania limekua sugu sasa. Kwa mara ya kwa kwanzana kupata tatizo ilikua pale Chuo kikuu cha dar katika Bank ya NBC. nakumbuka siku hiyo ilikua jumammosi jioni, baada ya kufika hapo Bank i was supprised the ATMs were not working. Nikajaribu tena jumma pili laki hali ilikua vivyohivyo. nikajaribu kwenda pale ubungo nikakuta nazo hazifanyi kazi. Baada ya kutrace hii trend ya ATM kuwa out of service, I came to realise most of the times juma mmosi jioni na juma pili ni siku ambazo ni risk kwa mteja anayetegemea kufanya transaction based on ATMs.
ReplyDeleteTatizo la pili katika ATMs systems za mabenki mengi hapo Tanzania zimejegwa sehemu ambazo access yake is limited to the particular period of time in a day which contract with the primary objective of enstalling ATMs' system which is giving customers flexibility of doing transactions in convenience of their own time in 24 hours. That is there should not be any obstacle whatsoever for customers to do transaction in 24 hour.
I therefore call upon all banks to revisit their ATMs positioning strategy for their survival in the evergrowing bank industry with stiff competition.
Mdau KAN
Norway
Utoke Sinza kwenda Mayfair Plaza, ATM, za Millenium Towers, Mikocheni pale mbele ya nyumba za TPDC, chuo kikuu, zote hizi kwako zilikuwa mbali hadi ufunge safari, tena kwa TAXI hadi Mayfari!
ReplyDeleteBwana mdogo ATM hata huku majuu kama iko mall na mall imefungwa huruhusiwi kuingia ndani ..ni sheria..ATM haina maana huwa wazi 24 hrs..I dont get your point!
ReplyDeleteATM siyo lazima ziwe wazi masaa 24.....alikuambia nani hiyo???
ReplyDeletekwa kawaida ATM za bank zote bongo ni service 24 hrs..kwa walinzi kutoa sababu kuwa sheria ya jengo la Mayfair haziruhu kufungua mageti baada ya saa 4 usiku ni upuuzi mtupu..lakini sishangai hata mie na dada yangu lilitukuta hili tatizo..nilienda bank ya NMB tawi la Tabora saa 4 usiku na walinzi wa pale ambao ni polisi wakagoma kuturuhusu kutumia ATM(walisema wanaogopa sisi twaweza kuwa majambazi na tumeficha bastola wakati wao walikuwa na smg)ikabidi tuende kituo polisi na kumchukua mkubwa wao aliyekuwa zamu ili atupeleke hadi bank(kituo cha polisi kipo karibu na bank)....hapo ndipo walipoturuhusu...lakini cha ajabu ni kuwa bango la ATM la hapo bank wanasema huduma ni 24hrs
ReplyDeleteU (June 24, 2009 11:36 PM)....U SO STUPID LOL YANI U SHOWIN OFF ON THIS BLOG HAHAH U STUPID YANI U TOO STUPID..nway pole u guys thats the way tz is u cant sue no 1....u just move on....
ReplyDelete(June 24, 2009 11:15 PM)..u must b from uk ama US,dude u cant sue no one huku u just move on t dont help ma guy...
(June 25, 2009 1:07 AM)...wee bwana thats no xcuse hurudi home yani wewe i can bet my all life ni wale ulipelekwa na wazazzi kusoma but messed up n now unabeba box for the rest of ur life.many ppl come back home m sure u dont even have visa...ahaahaa snitch
Hata huku majuu saa nyingine ATM zinaishiwa hela especially weekends, hivyo ni common sema tu sisi tuna choice kubwa maana kila baada ya hatua chache unaweza pata nyingine, na ni kweli nyingine ziko kwenye malls ambazo zina restricted hours but again unaweza kutembea mwendo kidogo tu akakuta nyingine. pole sana mdau hayo matatizo yako kila sehemu ila tafuta zilizo nje ya majengo kama millenium tower.
ReplyDeletenaomba nimsaidie mdau.hiyo ni ATM ya stanbic bank,na ukiangalia,millenium tower,mikocheni hamna ATM ya stanbic karibu yake ni mayfair na head office ya stanbic,pale kinondoni.
ReplyDeleteATM ni kwaajili ya matumizi ya haraka,emergency na kupunguza foleni ndani ya ma bank.Nadhani stanbic wanatakiwa kuangalia upya swala la ATM zao kwa upande wa maeneo hayo.
Hivi huko bongo ukiwa na ATM card ya NBC huwezi ukadraw pesa NMB/CRDB/Stanbic/etc?
ReplyDeleteKama haiwezekani basi makampuni ya bank yaanze mchakato huo. Majuu karibu bank zote zimeshaingia kwenye huo mchakato. Ukiona ATM machine popote pale wapata huduma sio lazima iwe ya bank ulikofungulia account(though at a reasonable price). Otherwise pole sana mdau kwa mateknolojia ya bongo na taratibu za ovyoovyo.
hii mithupu umeandika mwenyewe staili ya uandishi nimeistukia.yaani utoke sinza uaende mikocheni myfair? atm ngapi umeziacha jirani na we ulikuwa na shida ya kufa mtu?sema labda una bifu na uongozi wa myfair yaani pawe wazi masaa 24.au nanii yako iliyopo hapo myfair umeifulia nini?
ReplyDeleteSasa kwani ilikuwa lazima uchukulie pesa kwenye atm ya hapo hapo mayfair tu?
ReplyDeleteNa ulipokataliwa ukaamua kwenda ofisi za kampuni ya ulinzi kinondoni, hiyo nauli ya taxi kwenda huo si unh\geweza kwenda kwenye atm ambayo ipo accessible muda huo? Stupid!
Mdau ujumbe umefika na that stupid bank imesikia kimeo chao, dont mind these MOFOs wanaoosha vinywa. I mean, is it rocket science to know which bank is headquartered in Kinondoni? Benki kibao siku hizi zinasogeza huduma kwa wadau, nyie mnakalia kufungia nyuma ya grilled doors... Take the bloody ATMs to the pips, man!
ReplyDeletemimi mdau uliewasilisha hii mada sijakuelewa,kwanza hujasema una kadi ya benki gani maana sehemu ulioitaja ina ATM za benki zaidi ya nne, na kuna atm zipo nje ya geti mfano UMOJA SWITCH. vilevile kwa sasa benki zaidi ya tano zinatoa kadi ya visa ambayo inakuwezesha kupata huduma kwenye atm nyingine nyingi tu.hiyo umoja switch pia unapata huduma zaidi ya benki saba.sasa sijapata sababu yako kutoka sinza hadi mikocheni !nawe mdau 1:07am hutaki kurudi kwa matatizo yako tu na si kupata huduma za atm saa tisa usiku ndio kigezo.hata huku pia huduma 24hrs zipo usichukulie tatazo la mtoa mada kiujumla.inaonyesha uliondoka kwalongolongo tu wewe.
ReplyDeletedada utatokaje sinza ulikoziacha ATM`s kibao uende hadi myfair labda ndio maana hata hao walinzi waliingiwa na mashaka haiingii akilini kabisa kuna ATM kibao tu ukitoka sinza kabla hujafika myfair au ndio walewale chips za steers tamu kuliko za sinza?
ReplyDeletePole sana mdau. lakini kwa nini mnakaa bila pesa ndani? walau 50,000 mnatakiwa muwe nayo ndani hasa pale unapokuwa na watoto na mtoto mkubwa(ua husband ). ushauri uwe na kiasi kidogo ndani>
ReplyDeleteatm sio lazima ziwe masaa 24.
ReplyDeleteuk kuna atm ndani ya maduka na duka likifungwa atm imefungwa, au ikiwa ndani ya shopping centre inayofungwa basi na atm nayo itakuwa imefungwa
wananchi wanahitaji kuelimishwa kuhusu ATMs. hii itaweza kuondoa mawazo yao ya kuwa ATM zote zipo wazi 24/7..huyu dada pamoja na mumewe wangefahamu hilo wasingepatwa na matatizo yote aliyoyaelezea hapo juu.
ReplyDeletemheshimiwa mkuu wa wilaya ya nanihii naomba uyafikishie mabenki hii message.
Tatizo si ATM bali ni mtumiaji wa ATM. Nina wasiwasi anaamini hawezi chukua fedha benki nyingine isipokuwa benki iliyompa kadi tu!
ReplyDeleteMmeniacha kwenye mataa, Mayfair plaza ndio wapi??? Inamaana ATM zipo chache sana basi Bongo... Dah!
ReplyDelete