
Ninapenda kuwajulisha, kwa watakaohitaji, kuhusu Southern Highlands School iliyopo mji wa Mafinga mkoani Iringa, Tanzania.
Hii ni shule ya msingi ya bweni inayotumia kiingereza, yaani english medium boarding primary school, na ambayo tangu kuanzishwa kwake haijawahi kufelisha mtoto.
Hivi sasa Southern Highlands School inapokea wanafunzi kwa madarasa karibia yote. Kwa walio USA, ukipenda kupata habari zaidi kuhusu hii shule na labda ungependa kumpeleka mtoto wako au kumfadhili ndugu yako yeyote hapo SHS, basi unaweza kuwasiliana na mkurugenzi wa shule hiyo, ambaye yupo hapa USA kwa muda mfupi,
kupitia namba 214-604-1726.
Ahsante.
Mdau Kitova
Ahsante.
Mdau Kitova
Inaonekana shule imetulia,ila waendeshaji ningewashauri muifungulie website ili watu wakitaka kupata more information wazipate kwa urahisi,haya mambo ya kutafutana kwenye simu kwa ajili ya details wazazi wengi hatuna imani nazo.
ReplyDeleteHivi mbona mnakua malimbukeni jamani wenye shule. Mmeweka namba ya sim kwa wale waishio Marekani sasa sisi tuliopo hapa Bongo tupige Marekani? Anzeni na namba ya nyumbani then mseme walioko huko majuu wapige ... Plz tundikeni namba yenu ya sim hapa bongo tuwaendee hewani faster kabla nafasi hazijajaa.
ReplyDeleteWeka basifull information, kama fees ni kiasi gani, mahali ilipo, matokeo ya taifa shule inakuwa ya ngapi! vitu kama hivyo!
ReplyDeleteHuyo mtu anayetaka watu wampigie simu yake bado hajagundua watu hupata more information about school from the website, naungana na anon no 1, we mwenye shule acha hiyo mambo, fungua hata kablogu.
ReplyDeleteKwa walioko nyumbani namba ya simu ipo kwenye tangazo lao. 026-277266. Mpaka namba ya nukushi na anuani pepe wametoa.
ReplyDeleteNafikiri kutumia au kutotumia Kingereza si muhimu (labda uwe na itikadi kama ya shangazi yangu). Ningependa kuona wasifu wa walimu waliopo hapo shuleni. Mwalimu mwenye sifa mwenye Kingereza alichojifunzia Chang'ombe ni bora kuliko mwalimu mwenye lafudhi ya Kimarekani (alozaliwa na kukulia US) na anaingia ualimu baada ya kazi ya miaka kadhaa ama ya kufanya kazi Posta au shirika la bima (AIG). Na kama alivyoomba mdau mmoja hapo juu, tunaomba na sisi namba za simu za hapa nyumbani ili tujaribu maana za Uganda na Kenya tushazichoka. Mwisho, mkurugenzi mkuu anafanya nini US?
ReplyDeletebongo bwana sasa kiingereza ndo elimu hio si lugha tu km lugha nyengine,, mungeweka sifa za maana sio eng,,,kuna nchi duniani zimeendelea bila hata ya kutumia hicho kiingereza ktk elimu
ReplyDeleteMara nyingi malimbukeni huwaita wengine malimbukeni. Angalia kwenye hiyo picha ya kwanza info zote zipo hapo.
ReplyDeleteMkuu KITOVA hii shule inaonekana si mchezo, naona vijana wakila internet kwa mbali. Sasa mimi ninaenda nyumbali karibuni nitaenda kuiangalia shule na kama ni mvuri sio kwa sura ni kwa ufundishaji basi nina vijana wako nyumbani wanatakiwa kuanza shule january itabidi niwapeleke huko ila kama nitarizika na ufundishaji na matokeo ya nyuma ya wanafunzi. Na nikikosa nafasi nitakusumbua uongee na huyo mkurugenzi anisaidie, shukrani kwa information.
ReplyDeleteNyie ndugu zangu mnaoulizia namba za simu, mbona imewekwa hapo juu kabisa kwenye picha, kwaa jili ya watu wote walioko TZ na wasiokuwako TZ. Simu ya walioko US ni moja tu, nayo ni kwasababu mkurugenzi yuko US sasa. Lakini akisharudi, simu ya kuwasiliana ni moja tu kwa walio nje na walio ndani. Watu wakishasikia tu Marekani wanajisikia hasira kama wametengwa vile!
ReplyDeleteMy God, Mafinga is growing fast so tremendously! Kwa uchumi hata wana Iringa town watakwama si mud mrefu. Na ukiacha vyuo vikuu vya Iringa, eneo la Mafinga/Mufindi, wana shule nzuri sana sasa.
ReplyDeleteMafinga Seminary..
Donbosco Seminary...
Consolata Seminary...
Bethel Sabs Girls...
Mafinga Sec School/J.J.Mungai
Changarawe sec school...
Ukiacha shule ya J.J.Mungai sec school, zote zilizobaki zinatamba kitaifa. Sijataja shule zingine za eneo hilo nyingi, ambazo ni za Kata, bado zinasuasua.
Mnaoomba Namba ya simu za TZ ipo kwenye Tangazo.
ReplyDeletebela mwagito...kamwene na makasi
ReplyDeletesasa shule km iko bomba ivi email website sii ndo muhimu???yan tunataka full information ya shule yako yan huduma zipatikanazo apo,ada na michango mingineyo na wasifu wa walimu jamen...
websites zooote zenye akili dunian wanaweka wasifu za kuanzia head of school/college na waalimu wote na administrator nk
ili watu tuwe na imani na tufanye kasi si kupapasa siku izi kuna usanii mwiiingi sana izi english medium...uganda/kenya ukipeleka watoto wanarudi vyangu/mashoga.
wee utapiga simu uongee masaa mangapi???na unaweza sahau maswali mengi tu,SO WEKA WEBSITES APO
ila nakufagilia sana bela kufungua skuli IRINGA-MAFINGA kwetu kubooma
ni hayo tu
hao wote wanaolalamika kupata namba ya simu ya nyumbani lazma watakuwa alifeli kwa uzembe kwenye mitihani yao ya shule..hawako makini,contacts zote zipo kwenye picha ya tangazo lao hapo..yani wabongo zie kulalamika tu bila sababu..so disgusting!!
ReplyDeleteMafinga, mh????
ReplyDeleteToo cold for my Dar-born kids!
Asante. Au unasemaje my neighbour Rwegasira?
Anony wa June 18, 2009 1:16 PM
ReplyDeleteETI, '..... TOO COLD FOR MY DAR-BORN KIDS!" HIVI WEWE MZAZI WA JINSI GANI? UMESOMA NA KUELIMIKA? WATOTO WAKO KUZALIWA DSM UNATOA TANGAZO AU UKO SERIOUS KUWA HAWATASOMA NJE YA DSM? WANGAPI WANASOMA ULAYA, USA NK. KWENYE BARIDI, TENA BARAFU NA WAMEZALIWA DSM?
UNAONEKANA KAMA MZAZI UNA FIKRA ZENYE UPUNGUFU KIASI.... POLE.