Kwanza nakupa pongezi mkuu wa nanihii kwa kuendeleza libeneke. Udumu. Kuna ujumbe ningependa kuutuma kwa jamii kupitia globuni.
Hivi karibuni nilitumia huduma za posta kutuma kipeto chenye mipira miwili ya kandanda kutoka kwa Obama kwenda Mwanza. Mpira mmoja ulikuwa mpya kabisa na manailoni, mwingine ulikuwa umetumika kidogo.
Kuna mwizi bila aibu akafungua kile kipeto, akatwaa mpira mpya na kuurudishia uliotumika kidogo kisha akafunga lile kasha. Aliyetumiwa zawadi alilipa kodi za TRA kwa ajili ya kupokea mipira miwili kama ilivyoonyeshwa kwenye fomu za customs kwenye mzigo ule bila kufahamu kwamba mzigo umeibwa nusu. Alishangazwa alipofika nyumbani.Tukio hili limenisikitisha sana.
Inawezekana mwizi huyu amejaaliwa uwezo wa kifedha kuliko wadau waliokuwa wanausubiri mpira kwa hamu lakini bado ameona awaibie.
Mie bwana bila ya kwenda Mlingotini wala Sumbawanga nimelivalia njuga suala hili na sina shaka kwamba nitakapofikia mwisho wa ufuatiliaji wangu mpira huo utamtokea puani mwizi huyo.
Naomba kuwatahadharisha wadau mnaohitaji kutuma vipeto kutoka ughaibuni kwenda nyumbani. Kuna wezi wa vipeto wamejichanganya na wafanyakazi wa posta. Mabosi wa Posta mmesikia hili? Fanyeni usafi idara ya vipeto, kuna wezi wamejichanganya kwenye ofisi zenu.
Kama posta za ughaibuni zinaweza kufikisha vipeto vya watu na kuviacha mlangoni vikafika, kwa nini sisi tushindwe?
Mdau mwenye Usongo na mbaya wake
Pole sana na hilo kwa sababu hata mimi mkasa huo ulinikuta.nilimtumia mama yangu parcel,zilikua ni picha tu na zawadi ndogo ndogo,basi posta wakazifungua na hakupata mzigo huo wakati address ilikua sahihi. jana nimemtumia nephew wangu zawadi,na nimeweka risiti vizuri kabisa,kama isipomfikia,basi kusema kweli tutafikishana mbali,lazima mtu awajibike na hili suala.
ReplyDeleteKwa hili nakuunga mkono mara 100%. Ujue mimi nilipiga simu kwa manager wote wa posta pale Tanzania kudai mzigo wangu. Kwani mtu aliyeiba alianza kuwauzia anwani yangu pale St. Augustine University- Mwanza. Baadhi ya wanafunzi walianza kuniandikia barua wanaomba msaada. Wakidai kuwa Mr. Kamala ni mfanyakazi wa posta alikuwa anawauzia anwani yangu. Akiwaambia huyu kaka ana roho nzuri sana atawasaidia. Sasa siku mmoja nikatuma tena mzigo na kuweka mtego mkali kwa posta ya Dar. Mbona mzigo ulifika. Make niliwaambia mzigo huu umetuma kwa barua za kawaida na nataka ufike. Kwa hiyo unachosema hapa nakuelewa. Yafundishe adabu. Na juzi nimetuma mzigo mwingine nasubiri usifike watakiona cha moto. Make huku unaonyesha umetoka na umefika salama pale posta Dar. Sasa usipomfikia mwenyewe kiama chao. Moto utawaka mwenye minomo yao. Nimewawekea mtego.
ReplyDeleteHivi umeshaffanya uchunguzi na kugundua kuwa huo wizi umetendeka wakati mzigo umeshafika Tanzania.
ReplyDeleteWhat if ulipekechuliwa kutoka huko, ulikotumia
Sio kwamba natetea posta TZ, asilimia kubwa inawezekana umechangamkiwa at destination. lakini ni bora kuhakiki from source as well...
Wezi wako sehemu yeyote
Pole mdau kwa hilo, mie ninachokuomba waandikie posta barua rasmi ya kuibiwa na natunmai wakati unatuma uliorodhesha vitu vilivyomo ndani kwa aidha wakala au posta ya huko kwako na kusema wazi(ku-declare) thamani yake.kisha wasikilizie watasemaje.
ReplyDeleteKama hawakujibu tuma malalamiko mamlaka ya mawasiliano tanzania hawa ndio wasimamizi wa mambo ya mawasiliano nchi ikiwemo usafirishaji wa vipeto zaidi tembelea www.tcra.go.tz.suala hili litashughulikiwa.hatutaki kuona mambo haya ya wizi siku hizi wanaharibu sifa za shirika letu.
Tatizo la watu wengi ndio maana wanafeli katika mitihani yao sababu wakiulizwa hawalengi kwenye swali lile wanatoka nje ya mada.
ReplyDeleteJIBU : Kwa hakika wanaume kuvaa chupi si utamaduni wa muafrika. Utamaduni hasa wa muafrika ni kuvaa shuka, kanini, ngozi nk. Mfano hapo zamani watu walikuwa wanavaa hivyo. Mavazi mengi tunayovaa sasa si ya kitamaduni zetu ila ni tumeiga tu kutoka kwa Wazungu, na Wahindi.
Walioleta mavazi haya ni Wakoloni (Europeans) walipokuja kututawala basi tukaanza kuiga kila kitu kwao kwa kuwatukuza wao na vitu vyao.
Angalia mifano wa makabila mengi ya kiafrika ambayo bado yapo katika tamaduni za kiafrika bado hayavai mavazi haya eg:- Baadhi ya wamasai, Wamangati, Baadhi ya Wambulu, Wabarbaig etc.
Ukitaka kujua zaidi utamaduni wa Muafrika na Wabara la Afrika yani ikiwepo nchi ya Tanzania iko katika bara la Afrika pendelea sana kusoma vitabu vya Historian a tamaduni za Muafrika hapo kabla ya Ukoloni yaani PRE COLONIALISM utajua yooote.
Hili ndilo lilelile siku moja nilitoa maoni kuhusu Ufisadi nikasema ufisadi sio tuu serikalini kila mmoja anaiba katika sekta zake. Upo maofisini, Majumbani kila mahali.
Nahii inatokana na hali ngumu ya uchumi naye anataka awe nacho, wengine tamaa za macho tu, wengine ushamba ndio unaemponza kuchukua kitu pengine wala asiende kukitumia.
Lakini hii naimani ktk kila sekta wakiendeleza libeneke la kuwachunguza na kuwaumbua watu hawa wanaoharibu sifa basi Wataumbuliwa na watakoma.
Watu wanatakiwa kuwa na sanduku la maoni ya siri kila sekta ili kuwafichua watu hawa coz nahisi atakuwa anajulikana na hata mmoja wapo wa sekta hiyo ila anashindwa kumuumbua.
POLE SANA MDAU...KAZA BUTI FUATILIA SUALA HILO.
Mimi niliwahi kutumiwa feni toka Marekani, nikafika pale nikalipia post chgs, nikasogezwa upande wa TRA, nilipigiwa gharama ya kulipa ambayo ni mara mbili ya thamani ya ile feni. Nikawaambia ni bora wairudishe kwa aliyetuma. nikawsiliana na aliyetuma akasema ni sawa ni bora irudishwe.
ReplyDeleteCha ajabu haikurudishwa mpaka leo, na katika kumbukumbu zao ukiuliza wanadai nimeshaichukua. Yule aiyenitumia akafuatilia bila mafanikio. Hapo posta hasa hiyo idara kuna mafisadi wanaokula mali za watu tena wanyonge, wamulikwe ili posta iaminike, vinginevyo,...
anon june 12, 8:49,
ReplyDeletehivi wee unawatetea nini hawa posta? kwani wameanza leo wizi huo?
au nawe ni mmoja wao?
Huyo anayedai huenda wizi huo ulitokea kwa Obama hajui mfumo wa posta wa Amerika. Mdau mwenye usongo amesema kweli, kuna mizigo huwa inaletwa na posta majumbani mwa watu na kuachwa mlangoni kama wenyewe hawapo. Ukirudi kutoka kazini unaukuta mzigo wako. Kama tatizo lingetokea ughaibuni mzigo usingefika kabisa bongo, sio kuibiwa nusu. Hata mimi nimeshakumbwa na dhahama ya huduma za posta bongo. Nilimtumia bibi yangu karedio ka betri mbili aweze kuburudika na bongo flava na kujikumbusha enzi zake. Kuna jizi Posta liliona bora laana kuliko fedheha ya kumfikishia bibi yangu redio. Wapo wafanyakazi hawana dini kwenye hiyo idara.
ReplyDeletePole sana ndugu yangu kwa matatizo yaliyokupata.kwanza naomba kama inawezekana posta wawe na kitengo kinachoshughulikia parcel za nje na watu wa sehemu hiyo wawe wanajulikana kwa chochote kile kitakachokosekana au kupotea kwenye hii kitengo na pia wawe wanalipishwa/kukatwa mishahara yao iwapo mzigo utapotea.Pia nauliza kwa nini mzigo unakaa muda mrefu sana kwenye kitengo cha TRA?Kwani ukituma kwa express ya UPS,USPS na FEDEX mizigo huwa inachukuwa siku tatu tu, lakini cha ajabu ni TRA wanakaa nayo wiki nzima wakifanya nayo nini kama sio kukaribisha wizi?Mzigo ukifia mapatie mwenyewe na kama ni kodi sema ili mtu achukuwe kabla vicheche hawajapitia.cha muhimu watoeni puru halafu watashika adbu yao wao wanafikiri hizi pesa zinaokotwa.Mkurugenzi wa posta na TRA rahisisheni mizigo ya watu haraka wacheni urasimu usikuwa na mpango wowote.
ReplyDeletekwakweli ni aibu kwa watendaji wetu. huko ni kukosa maadili ya kazi... siyo posta tu, hata pale bandarini, watu hulalamika gari za watu kuchomolewa vitu... hii ni aibu na ni tabia mbaya kuliko... kabaya zaidi unaolalamika watendaji wakuu wamekuwa wajeuri mno, wanasahau kuwa kampuni ipo kwakuwa kuna wateja, kama wateja wakiondoka hakuna kampuni. posta wanakula ruzuku ya serikali, lakini ufanisi ni bure. wito kw watazania wote,, tuisuse posta, tutume mizigo kwa kutumia kampuni binafsi posta ikifungwa watakwenda kula nanihii zao
ReplyDeleteASIKUDANGANYE MTU,USITUME KITU CHA MAANA KWA POSTA KWENDA TANZANIA WATAKUIBIA ESPECIALLY WAKIJUA KINATOKA MTONI,LABDA UTUMIE OTHER COURIER KAMA DHL,FEDEX ETC.BADO KUNA UJINGA NA UMASKINI SANA TANZANIA INANIUMA SANA.WE KAMA UPO HUKU MTONI SUBIRIA MTU ANAENDA BONGO MPE BAG NA VITU VYOTE APANDE NAVYO PIPA,KAMA BAG KUBWA WE LIPIA TU EXCESS YA DOLA 150 THEN NENDA KAPIGE MZIGO URUDISHIE UKIWA NA UHAKIKA NDUGU ZAKO WANAPATA ZAWADI FRESH,HATA PALE AIRPORT HUWA WANAIBA PIA MUWE MACHO,UMASKINI MBAYA SANA!
ReplyDeleteMungu ibariki Tanzania, Mungu bariki posta TZ, poleni kwa mikasa kwani posta TZ kuibiwa ni kama kawa, hao wezi wa vi-parcel kama vile wana madudu vichwani, wakiona address kutoka ughaibuni huwa wanaenda wazimu. kuna siku nilituma picha moja tu kwenye frem ya plastic hivi, na mtu akafungua nafikiri alikwenda kuiweka nyumbani kwake hadi akafurahi alafu akairudisha posta ni baada ya miezi mitano ndo nyumbani waliipata na bahasha mbovu iliyokwisha funguliwa. kuna siku tu mtu atafungua akutane na joka humo ndo watakoma
ReplyDeletethank michuzi
Huyo jamaa anayewatete hao jamaa wa posta, nafikiri kama si mmoja wao basi ana ndugu yake anafanya kazi hizo
ReplyDelete12, 8:49 unachekesha
ReplyDeleteWa huku wachukue package inayoenda nje ya nchi???? Teh teh teh
Mizigo ikitoka bongo inatufikia vizuri.
Kwa wapenzi wa eBay huku wala mizigo haipotei na sio lazima uende ukapokee posta. Unawekewa nje ya malango wapo kama haupo ukirudi nyumbani jioni unakuta package yako inakusubiri.
Tanzania wanaiba hata picha, document za shule ukimtumia mtu zitafunguliwa......Jamani ukiiba hizo form za shule utaweza kuzijaza ili uje usome hiyo shule kweli au ni kupotezeana tu muda tu
KWELI WAFANYAKAZI WA POSTA MNACHOSHA SANA
Ninachoweza kuwashauri ni ku-insure mzigo. It wont cost you more than a few dollars. Lakini usitume vitu invaluable kama picha etc...
ReplyDeleteWewe unayewatetea posta nafikiri huko kwenye hiyo Idara. Sasa mimi niliibiwa mzigo wangu. Nilitumia hii anwani hapa hadi mzigo wangu ukapatikana.
ReplyDeleteZONAL POSTAL MANAGER
P.O BOX 707
DAR ES SALAAM
TANZANIA, EAST AFRICA.
Make nilifatilia kwa Obama nikaona umetoka na kutua Bongo. Nilichofanya niliambatanisha Risiti ya malipo, na nikawaambia kuwa niwapeleka mahakamani kama mzigo wangu haujapatika. Mbona walirudisha. Na nilituma kwa kawaida. Ilikuwa ni printer. Ukumbuke hiyo tarehe, mwezi walipeleka pale nyumbani utapata tu.
Kwa hiyo usilegeze kama wabane watarudisha.
Mimi ninakupa pole sana. Hiyo tabia wafanyakazi wa shirika la posta wanayo sana na nashindwa kuelewa ni nini kinasababisha hiyo tabia, sasa sijui ni tamaa ama la. kwani mimi mwenyewe kuna barua nilitumiwa kutoka nje sasa ilikuwa na vitabu sijui walifikiri kuna kitu cha maana humo maana walizifungua tena bila hata haya wakanipa zikiwa zimefunguliwa. inaudhi na inaboa kweli. na sijui kwanini viongozi wa juu hawaishughulikii hii kero maana na hakika wanajua kabisa.
ReplyDelete