
MUSTAFA HASSANALI KUONYESHA MAVAZI KWENYE “WIKI YA MITINDO AFRIKA” NCHNI AFRIKA KUSINI.
*KUONYESHA “READY TO WEAR COLLECTION” LIITWALO “MDUARA”.
*KUONDOKA NA WANAHABARI KUTOKA TANZANIA
Na Mwandishi Maalumu
Kampuni ya Africa Fashion International imemualika mbunifu mahari wa mavazi kutoka Tanzania kuonyesha mitindo yake kwenye maonyesho ya mavazi iliyopewa jina la ARISE Afrika Fashion Week.
Maonyesho hayo yatafanyika tarehe 12-19 Juni huko Sandton Convention Centre, Johannesburg , Afrika kusini. Maonyesho hayo yatashirikisha wabunifu 52 kutoka nchi 21 barani Afrika yatakayodumu kwa muda wa siku 8.
Miongoni mwao ni Mustafa Hassanali akiwa mbunifu pekee kutoka nchini Tanzania hii ikiwa ni mara yake ya saba kushiriki.
Miongoni mwa maonyesho aliyowahi kushiriki nchini Afrika Kusini ni pamoja na “M'NET Face of Africa Finals Novemba 2008 Sun City”, Tanzanite One Jewellery Showing, Cape Town kwenye mkutano wa Mining Indaba 2007, Durban Fashion week 2006, Cape Town Fashion week 2005 & 2006 na Vukani Fashion Fair and awards, Pretoria 2004.
Mustafa Hassanali anasema “Hii ni fursa maridhawa si kwa kuweza kufahamiana na wabunifu na wadau wengine bali pia ni wakati muafaka kuweza kutafuta masoko kwa ajili ya mavazi yangu”. Mustafa Hassanali atazindua nguo zake za majira ya kiangazi/kipupwe ya 2009/10 iitwayo MDUARA ambayo yana vionjo na mguso wa utamaduni wa jamii ya kiswahili ya kitanzania.
Mustafa aongeza “Imani ya muziki asilia wa mduara umechangia kwa kiasi kikubwa katika mitindo yangu ya kipindi hiki ambayo ni mchanganyiko wa vionjo asilia vya pwani vilivyoboreshwa”.
Mutafa Hassanali amedhamiria kuitangaza fani ya ubunifu wa mavazi Tanzania na pia kuhamasisha watu kupenda vitu ambavyo vimebuniwa na kutengenezwa hapa.
Akiwa anaipeperusha bendera ya Tanzania nchini Afrika Kusini, Mustafa Hassanali atafuatana na wanahabari ambao watahudhuria maonyesho yake yatakayofanyika tarehe 14 Juni na pia kufuatilia yaliyojiri nyuma ya kamera kwa kipindi chote cha Arise Africa Fashion Week.
Safari ya wanahabari hao kwenda nchini Afrika kusini imedhaminiwa na Vodacom Tanzania (www.vodacom.co.tz), Tanzania Broadcasting Corporation(www.tbccorp.org) na 1Time Airlines(www.1time.co.za)
Mustafa Hassanali ni mbunifu maarufu aliyebobea. Kazi zake ni za ubunifu wa hali ya juu, nakshi ya aina ya kipekee ambayo haina upinzani katika dunia ya mavazi na mitindo hapa Tanzania.
Mustafa amefanikiwa kufanya maonyesho Nchi tofauti za Afrika pamoja na Europa hivyo kuweza kubuni mitindo yenye ubora na hadhi ya kimataifa na kuweza kuinua soko la mitindo na mavazi nchini.
MUHUSIKA: MUSTAFA HASSANALI
NAMBA YA SIMU: +255-76-7303880
Jamani huyu mtu si alikuwa pande la baba!! kaka michuzi please naomba ufuatilie huyu mtu ametumia njia gani mpaka kapungua, mana mimi ninagombana na mai husbund wangu kila siku kwa ajili ya mwili mkubwa nilionao, naomba msada wajameni!!
ReplyDeleteKa Mustafa naona unanza kupendeza ume loose weight , ume kuwa bomba , yani halafu u look young ,anza kupiga chuma utakua a hunky dude , maana uko tall utapendeza sana , nilikuona siku moja town nikashangaa kuona lile tumbo hauna tena ,dah afadhali maana ulikua haupendezai kabisa.
ReplyDeleteBora amepungua alikwua too much lolna nguo zake aache kutumia cheap material organza na satini tu matenge babu aka
ReplyDeleteyesuuu!! huyu ni mustafa kweli?? mmmh, imekuwaje?? hongera kaka naona umefanya kazi ya ziada, umependeza
ReplyDeleteyakobo alipoenda kumrubuni baba yake esau ampatie uzaliwa wa kwanza na mibaraka ababa yake hali akiwa aoni alimpapasa yakobo akamwambia SAUTI NI SAUTI YA YAKOBO ILA NGOZI NI NGOZI YA ESAU kwa wakristo nawasoma bible mtanielewa
ReplyDeleteNAMAANISHA USO NI USO WA MUSTAFA HASSANALI LAKINI MWILI NI MICHUZI
beautiful!
ReplyDelete