Dege la Continental likitokea Brussels kwenda New York ilibidi leo litue kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Newark baada ya rubani kufariki dunia wakati wakiwa angani.

Dege hilo aina ya Boeing 777 flight, likiwa na abiria 247 passengers lilitua salama mnamo saa kumi katika uwanja wa New Jersey , ambao ni mmoja kati ya viwanja vitatu vya jiji la New York

Shirika la ndege la Continental katika taarifa yake limesema rubani huyo alikuwa na umri wa miaka 61 akiishi mjini Newark na alishafanya kazi kwa muda wa miaka 21. Hadi sasa sababu ya kifo cha rubani huyo hakijajulikana.

Shirika la ndege la Continental ni la tano kwa ukubwa duniani na hutoa huduma kati ya Brussels na New York-Newark kila siku, na kuhudumia njia zipatazo 230 za Marekani, Latin na Amerika Kusini pamoja na Caribbean.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2009

    pamoja na kutuhabarisha, ni vema ukawa unatupa taarifa iliyokamilika. mfano, mambo yalivyokuwa baada ya kugundulika kwa kifo cha rubani huyo, nani aligundua kuwa rubani huyo kisha aga dunia, nani aliisaidia ndege kutua salama nk. taarifa kama hizi zitatusaidia kupata uhakika wa jambo na kuelewa zaidi, pia itatusaidia kujifunza.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 19, 2009

    poleni ni kama zali la precision pale KIA,rubani mkuu alipozimia!!palikua hapatoshi umo ndani

    ...abiria 247 passengers...hahahaaa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 19, 2009

    WE mr Anon wa kwana ktk ndege kunakuepo zaidi ya rubani mmoja kwahio usifikirie rubani akifa abiria atachukuwa sukani alafu pia kuna cabin engineer kwahio sio kama bus ya yarabi salama dereva akipata tatizo abiria anajisukuma mbele kula usukani na hapa unapewa vichwa va habari tu kama unataka maelezo zaidi zama ktk gazeti si unajua ni kama jinsi ya sms language au ulitaka blog nzima ijazwe kwa story ya huyu Rubani?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 19, 2009

    mambo mengine na wewe anon tumia ubongo wako we unahisi michu anapata wapi taarifa zote>au wazani michuzi alikuwa one of the crew member?well there was a doc onbod d flt kama ulisikia nyuzi au huna hata redio?wataka kutafuniwana kumezewa ee yakheee?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 19, 2009

    mdau wa mwanzo umewahi kusikia msemo "ustaarabu wa paka ni kunya mavi akajipaka"? huo ndio ulioufanya hapa, ulitaka kujifanya uonekane ni mwerevu na mjuzi matokeo yake kila mtu anakucheka. hivi ulidhani kila ndege kunakuwa na rubani mmoja na ni peke yake kwenye cockpit? au ulidhani huwa pia waliopo kwenye cockpit hawana mawasiliano na wahudumu wa ndege? JINGA KUBWA WEWE

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 19, 2009

    NDEGE HUWA NA DEREVA ZAIDI YA MMOJA, PIA KUNA AUTO PILOT, NDEGE INAWEZA KUJIENDESHA YENYE BILA YA DEREVA, SO NDENGE INAPORUKA HUWA NA RUBANI ZAIDI YA MMOJA NA PIA WANA SWITCH ON AUTO-PILOT IN CASE OF ANY THING.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 19, 2009

    mtu kama hajaelewa mnatakiwa mumueleweshe tu sio kumfanya kama hana akili binadam tunatofaotuana katika uelewa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 19, 2009

    Na wewe anon wa 1:57 pm ndege haina dereva ina rubani na auto pilot haitumiki in case of anything. ongea kinachoeleweka

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 19, 2009

    mweeee
    maanons mnavojifanya mnajua km waendesha ndege vile??hahahahaaaa
    aya tumewasikia ma-engineer wetu wa bongo/wabeba box

    mngemweleza kistaarabu tu uyo annon #1

    ila jaman izi ndege mboni zimeanza kututisha ivi??

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 19, 2009

    Newark iko New Jersey siyo New York na ndege ilitua saa sita kasoro siyo saa kumi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 19, 2009

    Waheshimiwa,Hili dege lilipangiwa kusafiri kutoka Brussels Kwenda Newark(Newjersy)ambapo coincidently ndipo nyumbani kwa marehemu.Halikutua kwa dharura Newark ambapo ni magharibi zaidi ikilinganishwa na JFK na LaGuardia(Airport za Newyork).Kama dharura lingetua Western Canada Kama ilivyo kawaida ya trans atlantic flights nyingi huingilia na kutokea pale juu ili kufupisha upana wa bahari kuelekea na kutokea Ulaya ndipo zinakwenda kwenye miji iliyopangiwa.Ruti zote ndefu huwa na marubani watatu ambao wote ni fully qualified na pia huwa na auto pilot.Hivyo haikuwa hatari wala dharura.Marehemu alikuwa na uzoefu wa miaka 32.Flight crew hupewa defibrillator ambayo hutumiwa kumsaidia mtu yeyote anayekuwa incapacitated.Newjersy na Newyork city zimetenganiswa na mto kwa umbali kama ule wa feli na kigamboni.Hivyo Newark pia inahudumia wakazi wa Nework kama vile JFK na LaGuardia.Thanx

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...