zawadi ya video ya wanafunzi katuletea mdau baraka wa chibiriti wa cesena, italy, ambayo aliirekodi alipokuja vekesheni bongo. chibiriti anasema yeye hachoki kuiangalia kwani humkumbusha mbaaaaaaaaaaaaaaali....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 09, 2009

    MAN! THAT WHAT'S UP. REMINDS ME LONG TIME,I CAN'T IMAGINE I WAS THAT SMALL IN PRIMAY SCHOOL! I FEEL LIKE I WAS BIGGER THAN THESE KIDS. I CAN'T TURN BACK THE TAPE (CAN'T GO BACK TO THAT AGE) THAT'S WHY I HATE LIFE. ONCE IT GOES NEVER RETURN, ONLY ONE SHOT.

    IT IS WHAT IT IS.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 09, 2009

    Aksante sana wadogo, I needed something like this to give more energy for boxes,
    Wamwsahau kuombea mishahara ya walimu wao,
    Otherwise inatukumbusha majukumu tulioyonayo kama Viongozi wa leo na kesho
    Mdau US

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 09, 2009

    Chibiliti yaani leo umenifanya nitake kulia, umenikumbusha zamaaani tena za kale. Nakumbuka nilipo kuwa shule ya msingi nami nilikuwa napiga band ya shule nilikuwa napiga ngoma ndogo ila siku ya usafi nilikuwa napewa ngoma kubwa kwa kuwa ilikuwa ni rahisi kuipiga kwa usafi ila kwa kwenda darasani ilikuwa inahitaji uzoefu. Nilikuwa na rafiki zangu ambao nilikuwa nao kwenye band ya shule hata sijui wako wapi Stanslaus Mapima, Joakim Njarangi, Musa Athman, Steven Suka na wengineo kama watasoma hii mail naomba tuwasiliane kwa Email watchnare@yahoo.com

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 09, 2009

    Chibiliti ahsante sana, umenikumbusha mbali, sasa sisi baada ya hapo tulikuwa tunapigwa table, unaijua table? yaani wewe ukipatia ndio unaingia darasani fimbo sio lazima. Siku hizi nashangaa hata madaftari hayana table kwenye majalada kama zamani.
    OMBI: Naomba wanunulie boksi mbili za raba wavae sare wapendeze kama sadaka tu au malipo ya kututumbuiza, wako wachache tu hawa halafu kuna baridi lakini sio wote wenye sweta wadau wengine haya boxi mbili za sweta, hii shule iko wapi nitaenda kuwaona, niwalipe siwezi kutumbuizwa bure, itakuwa ni wizi wa fadhila.

    Mungu ATUPE NA TUTOE, Mungu ibariki TANVZANIA. amin.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 09, 2009

    Aww!,soo qute!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 09, 2009

    jamani!!

    nimedondosha chozi sijui kwanini?

    nimesikia apa ni kilimanjaro wilaya gani sijasikia vizuri

    ila nyinyi,kuna watu wana shida uko vijijini??

    siwezi ongea zaidi

    aisee

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 09, 2009

    heeeee!!

    awa ndio maboss wa baadae

    Mungu tusaidie

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 09, 2009

    ...wilayani Same

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 09, 2009

    ...cheki mwalimu kuleeee nyuma anavozunguka...ole wako uimbe ukosee BAKORA

    mtoto ana kifua kikali,no sweta

    asante kwa video

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 09, 2009

    Yani mdau umenikumbusha 1984-1986 shule ya msingi kipampa huku ujiji,nikiwa kwenye bendi ya shule napiga ngoma ndogo ya mstari wa kwanza,nawakumbuka Rajab saidi bend master,Hanzuruni gonga(chaka)katika filimbi,songoro husein,misolo kihuna,sudi, na wengine wengi nimewasahau bila kumsahau mwalimu wa musiki charles nkombe jamani tuwasiliane mlipo.nakukumbuka ili ushaguliwe kwenye ngoma lazima uwe msafi!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 09, 2009

    Hi kama iringa vile au wapi ? wamependeza kweli lol back on those day will never comes back wametuburudisha safi sana viji vetu bana mhhh

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 09, 2009

    This video impose challenges that are infront of every Tanzanian. Look at those kids eyes, majority of them doesn't understand what is ahead of the life.

    Ask your self how much money do we need to build schools, roads and mazingira mazuri ya kusomea.

    I still believe Tanzania is the street of Ghost... am sorry but i lather wipe white bats lather than came back and witness that humiliation and unjust society.

    Mwanaharakati wa Marekani

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 09, 2009

    Chibiliti..., wewe ni noma. asante kwa hii, imenikumbusha 1985 mwalimu mwanjisi anatufundisha a,e,i,o,u mada ya wiki (machozi kidogo, then ha ha haaaaa) class tupo na lazaro mwakitosi, neema mhagama, ester liwenga, zena kilindo, abdul lila, kimata, edward kumwembe, alex mwanjisi, eunice kawanga, mage mwambe (class monitor) rashid jeba (kaka mkuu), musa juma, maimuna wakati, daniel singano, irene shuli......mwalimu chimpepo na ngonyani wanakula mingo watutandike..dah. jamani tuwasilianeeeeee. CHIBILITI THANX A LOT ONCE AGAIN

    gordon, dar

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 09, 2009

    Dah, halafu WANANATA NA BEAT. bravo BRAVOOOOOO

    chiggs, deslam

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 09, 2009

    Awesome. A very nice melody! watoto kama hawa hata hawajui kama ufisadi ni nini...so honest!

    mdau-Germany

    ReplyDelete
  16. Al MusomaJune 09, 2009

    Itabidi niache kuwashangaa rafiki zangu wa Kimombasa ambao hata wakiandika wao neno "kibiriti" wakilisoma watatamka "kiribiti". Hapa naona jina limeandikwa "Chiribiti" lakini wadau wanaomshukuru wanamwita "Chilibiti". Is this a genetic problem?

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 09, 2009

    thanks jamani long time.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 09, 2009

    Bravo Chubiliti..... what a post!!!

    ReplyDelete
  19. dah
    asante sana yaani umenifanya nilie machozi kabisa. kweli hii ina kufanya ujifikirie na ku appriciate more tulivyo navyo sasa, haswa sie tuliopo nje ya nchi.hata hivyo kama mdau hapo juu alivyo sema inge kuwa vizuri kama kaka Michuzi ungetueleza jinsi gani tuna weza kuwa saidia hawa watoto sare zao za shule na labda madawati sijui dah Its very nice nad painful at the same time.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 09, 2009

    ...Nimetokwa machozi kwa clip hiyo.Ona hayo mazingira tizama hao watoto ona hizo ngoma.ndiko tulikotoka,ndio ukweli halisia mtanzania mtoto mkulima.

    Je mafisadi huona hayo? mazingira ya nyumbani,nyumbani.

    Ishi mtanzania,inuka tanzania huo ndio mwanga wako siku zote...

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 09, 2009

    unanikumbusha mbaaaali, mkiimba wimbo huo hamruhusiwi kutembea ni kama wimbo wa taifa, angalia kwa makini picha hiyo.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 09, 2009

    HIVI WADAU TUNASHINDWA KUANZISHA MFUKO WA KUCHANGIA SHULE ZA VIJIJINI KUPITIA MICHUZI? NAJUA TUNAJIITA GLOBU YA JAMII KWA MDA MREFU JE MNAONAJE TUKISAIDIA JAMII? MICHANGO IKATUMWA KWA MICHUZI ALAFU TUNASAIDIA SHULE FLANI KAMA VITABU,MADAWATI.FUND RAISING INAWEZA KUFANYIKA KILA BAADA YA MIEZI MITATU NA KWA KIWANGO CHOCHOTE MTU ALICHOKUWA NACHO.NI WAZO TU NIMEJARIBU KUTOA NA KAMA MWINGINE ANA WAZO ZURI ZAIDI ANAWEZA KUSEMA.TUKISUBIRI SERIKALI HIWASAIDIE NDUGU ZETU KWENYE MASHULE TUTATENDELEA KUPISHANA KUKAA CHINI MPAKA VITUKUU VYETU.
    mdau mzawa

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 09, 2009

    WEZI WENGI HIZO PESA ZITAFIKA HATA NUSU NJIA WEWE KANUNUE DESKI WEKA PALA DALASANI KANUNUE PENCELI WAPE WANAFUNZI UKIPITIA KWA WASWAHILI UMEULA ZINAISHIA MBEZI GADENI ZOTE

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 09, 2009

    Kweli ni Muda wa kujengwa shule Ya Wadau Kisarawe au Mkoani ndani ndani na mie naunga mkono. Hahaaha Eti wananata na Beat.

    Mmoja kakohowa nikasema doh Mwalimu mwenye sifa atamchapa bila sababu.

    Mungu inshallah atawasaidia wafike mbali kwenye maisha yao, hasa watoto wa kike manake wengi tunajuwa sehemu kama hizo watoto wa kike hawafiki mbali.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 09, 2009

    daaah.... nakumbuka na mimi nilivaa hzo kaptula rangi ya kaki na wasichana walivaa hvyohivyo blue mtejeta mpwapwa. suruali za mzee zilizomruka mama alikuwa anazikata nakuwa kaptula ya shule.

    tuliosoma shule za serikali tulienjoy sana...hayasahauliki mambo ya kasunzu...

    mdau,kuala lumpur

    ReplyDelete
  26. AnonymousJune 09, 2009

    Mdau wa 3.41 pm umetoa mawazo yangu kichwani,sisi wadau tunaoitwa wabeba mabox please please tufungue account yetu tuweze kusaidia shule kama hizi, bweni za wanafunzi,wodi za wakina mama na watoto.Tukichanga hata dola 3 au 5 kila mwezi tuna MAKE CHANGE..... PLEASE, au tufungue group kwa facebook much better.. Ninamakoti ya watoto na viatu chungu mzima vya watoto, nahitaji tu gia namba tano nitakuwa mchangiaji mzuri sana, mdau wa Danmark

    ReplyDelete
  27. AnonymousJune 09, 2009

    Kweli hii clip imenikumbusha nilikotoka kabisa, ni kweli haichoshi kuitazama inatukumbusha mengi mno. Shukrani kwa alieiweka.

    Watoto huko mliko mpokee baraka nyingi kutoka kwa Mungu.

    ReplyDelete
  28. AnonymousJune 10, 2009

    Chibiriti asante sana. Post yako inaamsha mixed emotions, furaha na huzuni. Furaha kwa sababu nimepita katika maisha hayo ya kukulia na kusoma vijijini katika mazingira magumu sana miaka ya 80, na kwa neema ya Mungu kufika hapa nilipo. Huzuni kwa sababu leo hii watoto wengi wanapitia mazingira magumu zaidi ya umasikini, ukiwa, gharama za juu sana za maisha, uhaba wa walimu, walimu wamekosa motisha,udhalilishaji n.k. God bless them. By the way, mi nilikuwa mpiga filimbi!

    ReplyDelete
  29. AnonymousJune 10, 2009

    Duh tumetoka mbali sana
    asante kwa kutukumbusha..... enzi zile

    ReplyDelete
  30. AnonymousJune 10, 2009

    yan mie nilikua kiranja

    natoa tu amri "sasa ni wakati wa wimbo wa shule,ngoma anza,darasa la 5C anzisha..." talala lalala aa

    asante sana

    ReplyDelete
  31. AnonymousJune 11, 2009

    Wakati nasoma hizi post zetu kabla sijafikia kwa mtoa maada wa june 9 saa 3:41. Nilikuwa najiuliza kwa nini tusiungane na kuunda chombo ambacho kitaendeshwa na sisi wenyewe kupitia kaka Michuzi. Tuanzishe mfuko wa kuwasaidia watoto wa shule hususan za vijijini naomba kama tutaafikiana na hilo basi tuanze na watoto hawa maana wao ndio wametutia hari na mshawasha wa kukumbuka tuliko toka . Ili kufanikisha hili naomba tuaminiane kwenye suala la pesa, kwani najua pesa inaweza hata kutoa roho ya mtu. Kaka michuzi tunakuomba uandike maanda kuhusu suala hili na wewe tunaomba utumie muda wako kwa suala hili. Mimi binafsi napendekeza wewe uwe na vyeo vyote ingawa kwenye mambo ya pesa hutakiwi kuwa na vyeo vyote kwani CEO na CFO lazima wawe watu wawili tofauti. Nakupendekeza wewe kwa kuwa itakuwa rahisi kukufunga kama utakuwa fisadi. Naomba uwe unaonyesha kila cent inayo tumwa kupitia kwenye mfuko ambao tutauanzisha hata kwa wale watakao tumia money gram or western union. Tunaomba uorodheshe majina na amount iliyotolewa ili kuepuka manung'uniko. Halafu sisi watoa maoni tutakuwa tuna kusaidia kwa mahesabu tukiwa huku huku tuliko ila itabidi mtu kama Chibiriti tumshirikishe vilivyo kwa kuwa ni mmoja wa watu ambao wanashiriki vilivyo kwenye glob hii ya jamii. Mimi ni mbeba box sina pesa nyingi ila kama itaanzishwa hii kitu nitaanza kutoa dollar mia tano. Naomba mtu mwingine asianzishe ni kaka Michuzi pekee aanzishe kwani kwa kufanya hivyo kuna leta imani na michango yetu. Kama nitakuwa nimekosea naomba mnisamehe, ila mimi ninaona kama ni njia bora ya kuwasaidia wasomi wetu na viongozi wa baadae. tuwasiliane kwenye email watchnare@yahoo.com.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJune 12, 2009

    I feel emotional listening to these cute kids.Ins nikumbusha nidhamu ya lhali ya juu uwapo mistalini dah.I love these kids God bless them.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...