zawadi ya video ya wanafunzi katuletea mdau baraka wa chibiriti wa cesena, italy, ambayo aliirekodi alipokuja vekesheni bongo. chibiriti anasema yeye hachoki kuiangalia kwani humkumbusha mbaaaaaaaaaaaaaaali....
Home
Unlabelled
salamu toka kwa chibiriti
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MAN! THAT WHAT'S UP. REMINDS ME LONG TIME,I CAN'T IMAGINE I WAS THAT SMALL IN PRIMAY SCHOOL! I FEEL LIKE I WAS BIGGER THAN THESE KIDS. I CAN'T TURN BACK THE TAPE (CAN'T GO BACK TO THAT AGE) THAT'S WHY I HATE LIFE. ONCE IT GOES NEVER RETURN, ONLY ONE SHOT.
ReplyDeleteIT IS WHAT IT IS.
Aksante sana wadogo, I needed something like this to give more energy for boxes,
ReplyDeleteWamwsahau kuombea mishahara ya walimu wao,
Otherwise inatukumbusha majukumu tulioyonayo kama Viongozi wa leo na kesho
Mdau US
Chibiliti yaani leo umenifanya nitake kulia, umenikumbusha zamaaani tena za kale. Nakumbuka nilipo kuwa shule ya msingi nami nilikuwa napiga band ya shule nilikuwa napiga ngoma ndogo ila siku ya usafi nilikuwa napewa ngoma kubwa kwa kuwa ilikuwa ni rahisi kuipiga kwa usafi ila kwa kwenda darasani ilikuwa inahitaji uzoefu. Nilikuwa na rafiki zangu ambao nilikuwa nao kwenye band ya shule hata sijui wako wapi Stanslaus Mapima, Joakim Njarangi, Musa Athman, Steven Suka na wengineo kama watasoma hii mail naomba tuwasiliane kwa Email watchnare@yahoo.com
ReplyDeleteChibiliti ahsante sana, umenikumbusha mbali, sasa sisi baada ya hapo tulikuwa tunapigwa table, unaijua table? yaani wewe ukipatia ndio unaingia darasani fimbo sio lazima. Siku hizi nashangaa hata madaftari hayana table kwenye majalada kama zamani.
ReplyDeleteOMBI: Naomba wanunulie boksi mbili za raba wavae sare wapendeze kama sadaka tu au malipo ya kututumbuiza, wako wachache tu hawa halafu kuna baridi lakini sio wote wenye sweta wadau wengine haya boxi mbili za sweta, hii shule iko wapi nitaenda kuwaona, niwalipe siwezi kutumbuizwa bure, itakuwa ni wizi wa fadhila.
Mungu ATUPE NA TUTOE, Mungu ibariki TANVZANIA. amin.
Aww!,soo qute!
ReplyDeletejamani!!
ReplyDeletenimedondosha chozi sijui kwanini?
nimesikia apa ni kilimanjaro wilaya gani sijasikia vizuri
ila nyinyi,kuna watu wana shida uko vijijini??
siwezi ongea zaidi
aisee
heeeee!!
ReplyDeleteawa ndio maboss wa baadae
Mungu tusaidie
...wilayani Same
ReplyDelete...cheki mwalimu kuleeee nyuma anavozunguka...ole wako uimbe ukosee BAKORA
ReplyDeletemtoto ana kifua kikali,no sweta
asante kwa video
Yani mdau umenikumbusha 1984-1986 shule ya msingi kipampa huku ujiji,nikiwa kwenye bendi ya shule napiga ngoma ndogo ya mstari wa kwanza,nawakumbuka Rajab saidi bend master,Hanzuruni gonga(chaka)katika filimbi,songoro husein,misolo kihuna,sudi, na wengine wengi nimewasahau bila kumsahau mwalimu wa musiki charles nkombe jamani tuwasiliane mlipo.nakukumbuka ili ushaguliwe kwenye ngoma lazima uwe msafi!
ReplyDeleteHi kama iringa vile au wapi ? wamependeza kweli lol back on those day will never comes back wametuburudisha safi sana viji vetu bana mhhh
ReplyDeleteThis video impose challenges that are infront of every Tanzanian. Look at those kids eyes, majority of them doesn't understand what is ahead of the life.
ReplyDeleteAsk your self how much money do we need to build schools, roads and mazingira mazuri ya kusomea.
I still believe Tanzania is the street of Ghost... am sorry but i lather wipe white bats lather than came back and witness that humiliation and unjust society.
Mwanaharakati wa Marekani
Chibiliti..., wewe ni noma. asante kwa hii, imenikumbusha 1985 mwalimu mwanjisi anatufundisha a,e,i,o,u mada ya wiki (machozi kidogo, then ha ha haaaaa) class tupo na lazaro mwakitosi, neema mhagama, ester liwenga, zena kilindo, abdul lila, kimata, edward kumwembe, alex mwanjisi, eunice kawanga, mage mwambe (class monitor) rashid jeba (kaka mkuu), musa juma, maimuna wakati, daniel singano, irene shuli......mwalimu chimpepo na ngonyani wanakula mingo watutandike..dah. jamani tuwasilianeeeeee. CHIBILITI THANX A LOT ONCE AGAIN
ReplyDeletegordon, dar
Dah, halafu WANANATA NA BEAT. bravo BRAVOOOOOO
ReplyDeletechiggs, deslam
Awesome. A very nice melody! watoto kama hawa hata hawajui kama ufisadi ni nini...so honest!
ReplyDeletemdau-Germany
Itabidi niache kuwashangaa rafiki zangu wa Kimombasa ambao hata wakiandika wao neno "kibiriti" wakilisoma watatamka "kiribiti". Hapa naona jina limeandikwa "Chiribiti" lakini wadau wanaomshukuru wanamwita "Chilibiti". Is this a genetic problem?
ReplyDeletethanks jamani long time.
ReplyDeleteBravo Chubiliti..... what a post!!!
ReplyDeletedah
ReplyDeleteasante sana yaani umenifanya nilie machozi kabisa. kweli hii ina kufanya ujifikirie na ku appriciate more tulivyo navyo sasa, haswa sie tuliopo nje ya nchi.hata hivyo kama mdau hapo juu alivyo sema inge kuwa vizuri kama kaka Michuzi ungetueleza jinsi gani tuna weza kuwa saidia hawa watoto sare zao za shule na labda madawati sijui dah Its very nice nad painful at the same time.
...Nimetokwa machozi kwa clip hiyo.Ona hayo mazingira tizama hao watoto ona hizo ngoma.ndiko tulikotoka,ndio ukweli halisia mtanzania mtoto mkulima.
ReplyDeleteJe mafisadi huona hayo? mazingira ya nyumbani,nyumbani.
Ishi mtanzania,inuka tanzania huo ndio mwanga wako siku zote...
unanikumbusha mbaaaali, mkiimba wimbo huo hamruhusiwi kutembea ni kama wimbo wa taifa, angalia kwa makini picha hiyo.
ReplyDeleteHIVI WADAU TUNASHINDWA KUANZISHA MFUKO WA KUCHANGIA SHULE ZA VIJIJINI KUPITIA MICHUZI? NAJUA TUNAJIITA GLOBU YA JAMII KWA MDA MREFU JE MNAONAJE TUKISAIDIA JAMII? MICHANGO IKATUMWA KWA MICHUZI ALAFU TUNASAIDIA SHULE FLANI KAMA VITABU,MADAWATI.FUND RAISING INAWEZA KUFANYIKA KILA BAADA YA MIEZI MITATU NA KWA KIWANGO CHOCHOTE MTU ALICHOKUWA NACHO.NI WAZO TU NIMEJARIBU KUTOA NA KAMA MWINGINE ANA WAZO ZURI ZAIDI ANAWEZA KUSEMA.TUKISUBIRI SERIKALI HIWASAIDIE NDUGU ZETU KWENYE MASHULE TUTATENDELEA KUPISHANA KUKAA CHINI MPAKA VITUKUU VYETU.
ReplyDeletemdau mzawa
WEZI WENGI HIZO PESA ZITAFIKA HATA NUSU NJIA WEWE KANUNUE DESKI WEKA PALA DALASANI KANUNUE PENCELI WAPE WANAFUNZI UKIPITIA KWA WASWAHILI UMEULA ZINAISHIA MBEZI GADENI ZOTE
ReplyDeleteKweli ni Muda wa kujengwa shule Ya Wadau Kisarawe au Mkoani ndani ndani na mie naunga mkono. Hahaaha Eti wananata na Beat.
ReplyDeleteMmoja kakohowa nikasema doh Mwalimu mwenye sifa atamchapa bila sababu.
Mungu inshallah atawasaidia wafike mbali kwenye maisha yao, hasa watoto wa kike manake wengi tunajuwa sehemu kama hizo watoto wa kike hawafiki mbali.
daaah.... nakumbuka na mimi nilivaa hzo kaptula rangi ya kaki na wasichana walivaa hvyohivyo blue mtejeta mpwapwa. suruali za mzee zilizomruka mama alikuwa anazikata nakuwa kaptula ya shule.
ReplyDeletetuliosoma shule za serikali tulienjoy sana...hayasahauliki mambo ya kasunzu...
mdau,kuala lumpur
Mdau wa 3.41 pm umetoa mawazo yangu kichwani,sisi wadau tunaoitwa wabeba mabox please please tufungue account yetu tuweze kusaidia shule kama hizi, bweni za wanafunzi,wodi za wakina mama na watoto.Tukichanga hata dola 3 au 5 kila mwezi tuna MAKE CHANGE..... PLEASE, au tufungue group kwa facebook much better.. Ninamakoti ya watoto na viatu chungu mzima vya watoto, nahitaji tu gia namba tano nitakuwa mchangiaji mzuri sana, mdau wa Danmark
ReplyDeleteKweli hii clip imenikumbusha nilikotoka kabisa, ni kweli haichoshi kuitazama inatukumbusha mengi mno. Shukrani kwa alieiweka.
ReplyDeleteWatoto huko mliko mpokee baraka nyingi kutoka kwa Mungu.
Chibiriti asante sana. Post yako inaamsha mixed emotions, furaha na huzuni. Furaha kwa sababu nimepita katika maisha hayo ya kukulia na kusoma vijijini katika mazingira magumu sana miaka ya 80, na kwa neema ya Mungu kufika hapa nilipo. Huzuni kwa sababu leo hii watoto wengi wanapitia mazingira magumu zaidi ya umasikini, ukiwa, gharama za juu sana za maisha, uhaba wa walimu, walimu wamekosa motisha,udhalilishaji n.k. God bless them. By the way, mi nilikuwa mpiga filimbi!
ReplyDeleteDuh tumetoka mbali sana
ReplyDeleteasante kwa kutukumbusha..... enzi zile
yan mie nilikua kiranja
ReplyDeletenatoa tu amri "sasa ni wakati wa wimbo wa shule,ngoma anza,darasa la 5C anzisha..." talala lalala aa
asante sana
Wakati nasoma hizi post zetu kabla sijafikia kwa mtoa maada wa june 9 saa 3:41. Nilikuwa najiuliza kwa nini tusiungane na kuunda chombo ambacho kitaendeshwa na sisi wenyewe kupitia kaka Michuzi. Tuanzishe mfuko wa kuwasaidia watoto wa shule hususan za vijijini naomba kama tutaafikiana na hilo basi tuanze na watoto hawa maana wao ndio wametutia hari na mshawasha wa kukumbuka tuliko toka . Ili kufanikisha hili naomba tuaminiane kwenye suala la pesa, kwani najua pesa inaweza hata kutoa roho ya mtu. Kaka michuzi tunakuomba uandike maanda kuhusu suala hili na wewe tunaomba utumie muda wako kwa suala hili. Mimi binafsi napendekeza wewe uwe na vyeo vyote ingawa kwenye mambo ya pesa hutakiwi kuwa na vyeo vyote kwani CEO na CFO lazima wawe watu wawili tofauti. Nakupendekeza wewe kwa kuwa itakuwa rahisi kukufunga kama utakuwa fisadi. Naomba uwe unaonyesha kila cent inayo tumwa kupitia kwenye mfuko ambao tutauanzisha hata kwa wale watakao tumia money gram or western union. Tunaomba uorodheshe majina na amount iliyotolewa ili kuepuka manung'uniko. Halafu sisi watoa maoni tutakuwa tuna kusaidia kwa mahesabu tukiwa huku huku tuliko ila itabidi mtu kama Chibiriti tumshirikishe vilivyo kwa kuwa ni mmoja wa watu ambao wanashiriki vilivyo kwenye glob hii ya jamii. Mimi ni mbeba box sina pesa nyingi ila kama itaanzishwa hii kitu nitaanza kutoa dollar mia tano. Naomba mtu mwingine asianzishe ni kaka Michuzi pekee aanzishe kwani kwa kufanya hivyo kuna leta imani na michango yetu. Kama nitakuwa nimekosea naomba mnisamehe, ila mimi ninaona kama ni njia bora ya kuwasaidia wasomi wetu na viongozi wa baadae. tuwasiliane kwenye email watchnare@yahoo.com.
ReplyDeleteI feel emotional listening to these cute kids.Ins nikumbusha nidhamu ya lhali ya juu uwapo mistalini dah.I love these kids God bless them.
ReplyDelete