baada ya kutoa watu machozi kwa video ya awali ya hawa vijana wa shule ya msingi kule same, mdau baraka wa chibiriti aliyeko Cesena, Italy, anasema kafurahishwa sana na jinis wadau mlivyofurahishwa na video hiyo. na leo kaamua kutupa ingine
Home
Unlabelled
zawadi ingine toka kwa baraka chibiriti
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
mdau Chibiriti inaonyesha wewe una fan ya ualimu, na unanitia machungungu ya kutamani niende nika-visit shule moja nikasikilize nyimbo hizo.
ReplyDeletelaiti huo wimbo ndo ungekuwa wimbo wa taifa kaka ulivyo tarajiwa, labda watu wangepnguza ufisadi. wadau mnsemaje, sasa ndo tukachukua wimbo wa afrika kusini. kina mzee sykes wakadharauliwa.ASANTE KAKA IMETULIA.
ReplyDeleteDuh safi sana. Yani hiyo school band inanikumbusha mbali sana wakati na mimi napiga drums kwenye school band ya kisutu primary school in 1986 and 1987
ReplyDeleteEnzi Hizo Unakaa nyuma kabisa Sema Wengi humu wamesoma Enzi za Unaimba Chama Chetu Chamapinduzi cha jenga nchi Nyerere eeeeeeeeeeeeh na Mwinyi wajinga nchi hahaha kudadeki tulikuwa tunalazimishwa yasiokuwa na msingi. Bora nyimbo ya Taifa. walionyuma hawajui kuimba kimya. James
ReplyDeletekudadadeki Chibiriti, narudi songea
ReplyDeletethey are more patriotic than our leaders.
ReplyDeleteCHIBIRIT NI SHULE GANI HIO KAMA VIPI UNAONAJE TUWAFANYIE HARAMBEE HUMU?
Nilikuwa nacheck nione kama kuna mtoto asiye na viatu kama sisi enzi zetu za sabini lakini naona afadhari. Ila naona kuna baridi lakini wenye sweta ni watatu tu. mdau wa Italia basi fanya mchango wa kutuma angalao mitumba. Thanks for the pics.
ReplyDeleteUongo mbaya watoto wanakumbuka wimbo vyema kuliko nilivyofikiria. Siwezi kuimba kama walivyoimba wao!
ReplyDeleteGood job!
Barack Chibiriti, naona unafuata nyayo za rais mmoja hivi mwenye jina kama lako."kuipenda nchi yako"
ReplyDeleteNyerere was so successfull kwa kuwa brain wash watu kuhusu patriotism.
ReplyDeleteI surggest kila siku kabla ya bunge kuanza wabunge wajipange waimbe kama hawa watoto.
ahavache avae!ndi ndi mdevedhi))
ReplyDeleteswafi sanaa kiberiti aka chibiriti.
watu tumetoka mbali sana sijui nami nilikuwa dogo kama waonekanavyo hao lakini fujo tupu za LY! wato wa O-BAY Primary mpo?1987
namwunga mkono mdau aliyesema "laiti huo wimbo ndo ungekuwa wimbo wa taifa kaka ulivyo tarajiwa, labda watu wangepunguza ufisadi". Ni kweli au yule mdau aliyesema hii mibunge iwe inaimbishwa na Mh. Spika wimbo huu kabla ya kuanza kikao.
ReplyDeleteWamenipeleka mbali sana enzi za 1970s wakati huo mwalimu wetu katoka JKT tunaimbishwa nyimbo za uzalendo. Hapo inanifanya nimkumbuke mzee wetu Nyerere. Mjitu siku hizi imekengeuka na kupoteza uzalendo utafikiri haikuzaliwa wakati huo. Hongera ndugu yetui Chibiriti kwa kutukumbusha. jamani inauma kuona mifisadi hii. natamani mnipe urais niitie "chibiriti" niwashe moto
Ndugu zangu kuna mtu ana lyrics kamili za huo wimbo? Naupenda sana ila huwa sijui maandishi yake kamili.
ReplyDeleteTafadhali tusaidiane
HII inanikumbusha mbali sana,wakati huo mimi sina hili wala lile,wakati unaimbwa huo mwimbo nilikuwa nimejibanza sehemu fulani nikila chabo mwalimu akae vibaya na mimi nijiunge kwenye mstari hapo nimeshachelewa shule na ukijipeleka ovyo mwalimu akikuotea unakula bakora kuliko anazokupiga baba yako na hata akiambiwa na yeye kama mzazi anakuongezea,ila kusema ukweli tulikuwa na adabu sana ingawa tulikuwa na tabu kuandika tunakaa chini wenye viatu ni wachache na wote viatu vinacheka chini,du pindi ile.ukiangalia hao watoto utadhani na wewe hukupitia huko ila miaka ndio inakata uwanja tena.big up chibiriti
ReplyDeletehapo mtu mzima ukiwa mpiga ngoma basi hupigwi ukichelewa na shule nzima inakutambua ila kasheshe ipo kwa hao wengine usiponyoosha mstari unakula za uso na kunyoosha mstari inabidi umshike mwenzako begani.nakumbuka pinde hiyo hananasif primary school kinondoni nakumbuka niliwahi kurekodi kipindi mama na mwana sijui aliyekuwa host wakipindi hicho alikuwa ni mama deborah mwenda sina unakika vizuri hapo.
ReplyDeleteNi kweli kabisa inafaa kabla ya Bunge kuanza wanatakiwa waimbe hawahawa watoto labda hao viongozi watakumbuka wametoka wapi.
ReplyDeleteTanzania Tanzania, Nakupenda kwa moyo wote,
ReplyDeleteNchi yangu Tanzania, jina lako ni tamu sana,
Nilalapo nakuota wewe, niamkapo ni heri mama wee!
Tanzania Tanzania, Nakupenda kwa moyo wotee!.
Tanzania Tanzania, Ninapokwenda safarini,
Kutazama maajabu, biashara nayo makazi,
Sitaweza kusahau mimi, mambo mema ya kwetu kabisaa!
Tanzania Tanzania, Nakupenda kwa moyo wotee!.
Tanzania Tanzania, Karibu wasio kwao,
Wenye shida na taabu, kukimbizwa na walowezi,
Tanzania yawakaribisha, mpigane kiume chema wee!
Tanzania Tanzania, heri yako kwa mataifa!.
Tanzania Tanzania, Watu wako niwema sana,
Nchi nyingi zakuota, nuru yako hakuna tena,
Na wageni wakukimbilia, ngome yako imara kweli wee!.
Tanzania Tanzania, Mola awe nawe daima!.
Kaka chibiriti umenikumbusha mbali sana wakati niko TABATA SHULE YA MSINGI 1979 wakati huo shule ilikuwa ya udongo na makuti. Sasa niko nabeba box kwa wazungu kuna siku nakumbuka nyumbani basi kitu cha kwanza kuniingia kichwani ni huo wimbo nawexza kuuimba hata siku nzima mpaka nitoke job.
ReplyDeleteKuna mdau ameeleza jinsi ya kuwasaidia watoto kama kuna mtu ataanzisha njia yoyote mimi niko tayari na kuchangia nilicho nacho.
mdau TVZ kicartoon...
ReplyDeleteoyaaa kuna ubeti mmoja,km sio wa mwisho uo unaanza na "Nchi nzuri Tanzania" au "Nchi yangu Tanzania,"
ila umepatia uko juu dah!!
michu unabana nini??
ReplyDeleteunajua kama mtu unataka kusaidia sasa ivi watu/kundi la wasiojiweza BORA tena BORA uende phisically toa msaada sehemu husika ishia zako,usilogwe upitishe eti sijui sirikali au whatsoever,hauwafikii walengwa,longolongo kibao...
itabidi tujitoe sana wadau,umepewa bure toeni bure
me naanzia MAKETE-IRINGA,
nashuka na misaada wa milele mayb nife ndo iwe mwisho mf kujenga ku-adopt families pale nk nk
TVZ Kicartoon, ahsante sana wengine tulikuwa hatujui maneno kamili ya wimbo.
ReplyDeleteBe good,
thanx!
ReplyDeleteni huo wa mwisho nafikiri, ni zamani sana,
Nchi nzuri Tanzania, Watu wako ni wema sana,
Nchi nyingi zakuota, nuru yako hakuna tena,
Na wageni wakukimbilia, ngome yako imara kweli eeh,
Tanzania Tanzania, Mola awe nawe daima!.
WAMEKOSEA CAMON THIS IS WESTERN CRAP HUU WIMBO HAUIMBWI NAMNA ILE. KUNA MAKOSA YA KIMSINGI SANA CHIPUKIZI HUWEZI SIMAMA UKIWA MKONO UKO LEGE NAMNA ILE. INABIDI UWE MGUU PANDE NA MKAKAMAVU MWILI MZIMA. KAMA HUJAKIMBIA MCHAKAMCHAKA BASI JASHO LINAKUTOKA WIMBO UKIISHA!! NAOMBA MWALIMU WA pE AKAPEWA ADHABU KWA KUSIMAMISHA WATOTO LEGE LEGE WAKATI WIMBO WA BENDERA UNAIMBWA.
ReplyDeleteMVUTA UGORO KILEMA
Ahsante, kuna watu wanapenda kujenga mazingira ya kuudhi wengine, basi leo tangu asubuhi kuna watu wanajitahidi kuniudhi. lakini nilivyosikiliza haka ka wimbo kakanfariji, ubarikiwe sana kwani wewe si mchoyo.
ReplyDelete