
Matangazo ni moja ya mambo muhimu katika uendeshaji wa biashara. Kutangaza biashara kukifanywa kwa umakini ndivyo huvuta wateja kwa wingi zaidi. Matangazo ni sehemu mojawapo ya mikakati ya utaafutaji masoko ikiwemo kukuza mahusiano ya kibiashara , promosheni za bidhaa, kutoa motisha kwa wateja, barua za kibiashara, na ujume wa mdomo au maneno.
Endapo unafikiria matangazo ni jambo la kisasa , basi fikiri kwa upana zaidi. Hapo mwanzo matangazo kwa sehemu kubwa yalikuwa yanafanyikwa kwa njia ya midomo ama maneno. Kwa mara ya kwanza matangazo yalipatikana maeneo ya Misri, Ugiriki na Italia ambapo matangazo ya biashara yaliwekwa ukutani na yaliyochorwa kwenye mawe, katika miaka ya 4000BC, na baadaye kuendelea kukua maeneo ya India, Africa na duniani kote .
Samabamba na kukua kwa matumizi ya matangazo,tekinologia ya matangazo imekuwa ikikuwa muda baada ya muda, kuanzia kwenye matangazo ya magazeti, kwenye redio, televisheni na sasa kwenye internet.
Matumizi ya internet yameleta mabadiliko makubwa katika jinsi ya kutangaza biashara na kuleta maendeleo ya kibiashara, ambapo taarifa za biashara husafiri kwa haraka zaidi toka upande moja mpaka mwingine na kuwafikia watu wengi kwa muda mfupi zaidi.
Faida za Matangazo
Kuwafikishia taarifa kwa urahisi wateja walengwa; Biashara yoyote inapoanziashwa huwa na wateja walengwa na kundi hili ndilo linalotakiwa kufikishiwa ujumbe kwa njia ya matangazo. Biashara inaweza kutofautisha wateja walengwa kwa umri, mahali, utamaduni n.k. Basi jambo la muhimu ni kujua kundi la wateja walengwa wa biashara ba kuangalia ni jinsi au ni aina gani ya matangazo itakayorahisisha ujumbe kufika kwa urahisi.
Kutambulisha bidhaa mpya; Mara nyingi bidhaa mpya huitaji nguvu ya ziada ili kukubalika katika jamii. Matangazo husaidia jitihada hizi na kuleta mafanikio kibiashara.
Kuelimisha wateja kuhusu biashara au bidhaa na huduma yako; Mpaka mteja afikie uamuzi wa kununua bidhaa au kutumia huduma yako anahitaji kuridhika kwanza. Mteja inabidi apewe taarifa za kutosha kuhusu bidhaa hiyo na kufuta maswali mengi kichwani mwake. Kwa kufanya hizi kutamrahisishia mteja kufikia maamuzi yake kwa urahisi.
Kutofautisha biashara moja na nyingine; Katika upinzani wa kibiashara, wateja hupenda kulinganisha kati ya biashara moja na nyingine. Basi tumia fulsa ya matangazo kwa kuelezea ubora wa bidhaa na faida nyinginezo ili kuvutia wateja katika biashara.
Kuwakumbusha wateja kuhusu bidhaa ama huduma; Ukosefu wa matangazo ya biashara hupelekea wateja kuisahau biashara na mauzo kushuka, basi wenye biashara hawana budi kuwa na ratiba ya kuwakumbusha wateja wao kuhusu bidhaa ama huduma mara kwa mara kupitia matangazo. Kuwakumbusha wateja kuhusu biashara yako huongeza ukaribu kati ya wateja na biashara.
Kuongeza mauzo na mapato ya biashara; Bila shaka umekwishasikia misemo hii, “Wateja ni uhai wa biashara” na “ Biashara ni matangazo”. Matangazo hupelekea wateja kuongwezeka na wanapoongezeka mauzo huongezeka na kipato cha biashara kuongezeka. Ongeza uhai wa biashara yako kupitia matangazo.
Mambo muhimu ya kuzingatia,
1. Gharama za matangazo; Gharama za matangazo zinatofautiana kutoka njia moja mpaka nyingine na ufanisi wa njia moja hutofautiana na ufanisi wa njia nyingine. Jambo la muhimu ni kuchagua aina ya matangazo kulingana na uchumi wa biashara yako.
2. Ujumbe katika Tangazo: Jambo jingine muhimu la kuangalia ni aina ya Ujumbe Unaotumika, hapa nina maana ujumbe wa matangazo uwe wa uwazi na usiomchanganya mteja.
Kuna mambo mengi ya kutazama kabla hujafanya Ad. Hapa huyu jamaa amezungumzia kwa vibiashara vidogo.
ReplyDeleteLakini kwa big business lazima kuna baadhi ya ratio uzitazame kama zinamake sense... Mfano lazima utazame ad:revenue... uone kama kweli ina ad zina boost sales, na jee ad:profit imekaa vipi?
so... again lazima ujue cost/benefit ratio zimelala vipi.....
Mchumi wa Texas
Independent consultant.
afri(k)a...
ReplyDeletezingatia hili unapoandika
Mchumi wa Texas, hayo maelezo ya jamaa yana cover kila aina ya biashara mzee. kitu ambacho wewe umekizungumzia ni kupima effectiveness ya matangazo. kila biashara inatakiwa ipime kama matangazo yameongeza kitu kwenye iyo biashara.kupima effectiveness ya matangazo sio tu kwa ratio maana kuna vitu vingine ni qualitative ambavyo huwezi kuviweka katika ratios.iwe biashara ndogo au kubwa concept itabaki palepale. Mzee wa Kibada
ReplyDelete