leo ilikuwa hepi besdei ya kuzaliwa kwa anitha ambapo ilisherehekewa na kamnuso fulani hivi ka kishkaji katika mgahawa mmoja wa kichina katikati ya dar
anitha akikata keki akishuduwa na mai hazbendi wake dennis na wakweze
anko nanihii naye alikuwepo anko nanihii huwa hajivungagi kwenye mnuso kama huu
baba wa ubatizo wa dennis akimzawadia anitha kadi huku dennis akishuhudia
anitha akipokea zawadi toka kwa wifi huku wakweze mzee stephen rweikiza na mai waifu wake na dennis wakiangalia
anitha akipozi na wakweze, wifi na dennis
anitha akipozi na wakweze na wifie
Angalizo: Anitha na Dennis ni wadau wakubwa wa glob ya jamii wakitokea Wichita, Marekani. Wao wako hapa bongo kwa vekesheni ya kumeremeta na mnuso wao ulifanyika hivi karibuni. kwa kumbukumbu hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 10, 2009

    michuzi wewe ni muislam amruhusiwi kula ulevi naona kijani ipo karubu na plate yako. sio sawa mtu mzima

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 10, 2009

    fanyeni mrudi tuliendeleze libeneke la box

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 10, 2009

    Anko Michuzi, io picha ya nne mbona vidole vimepauka sana?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 10, 2009

    mweee michuzi we tangu lini umeanza kula kwa kutumia hivyo vijiti vya kichina...maana hapo naona vinakutoa ushamba kidogo maana wewe ushazoea kula kwa madole matano kama unavyo kula kule kwa mtogole

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 10, 2009

    Michuzi,
    Duuh wee kweli Mzee wa Libeneke. Naona unawahi kuku mapema. Unanikumbusha wakati wa minuso linaletwa sinia la pilau wataalam walikuwa wanavamia nyama kwanza ten wanamalizia na wali :)

    ReplyDelete
  6. Heh!! wee! Muhidini ! umeanza lini kukamata kilaji? staghafilulaaah!!!! halafu naona vijiti vinakutoa ushamba si ula na mikono tuu

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 10, 2009

    oneni mifano mizuri, ndoa hiyo, kitu imetulia hiyo.
    Ila mdumishe na uaminifu kwenye Ndoa pia.
    Tuwaache walafi wakipukutika kwa kutokuwa waaminifu kwenye ndoa zao.
    Tuonyeshe mifano bora na watu waseme nataka ndoa kama ya yule aliye kwenye Blog ya Michuzi.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 10, 2009

    Mmependeza Anita!! Huyo wifi yako nimempenda. Naomba details zake, natafuta Jiko!

    Jerry

    Makao Mapya

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 10, 2009

    sasa apo ni ndoa au bethidei??

    jamani

    ivi adi mjichoreshe umu bloguni??

    khaaaaa

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 10, 2009

    siku izi unajiita anko???????????

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 10, 2009

    nakukubali mkuu wa wilaya. Ila tutambulishe basi huyu Anita na mai hazibandi wake umewapa shavu sana ni kina nani hawa tupe intro basi.
    wako mdau mtiifu.
    ETM

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 10, 2009

    ..annon #1

    ivi dini ni nini?ni asili yako wewe?ndo nyie kuiba ofisini kwa makaratasi na kutukana ni kawaida ila ngono ni kosa....nyambafu

    yan mtu kwa raha zake na maamuzi yake mwenyewe

    akhaaa

    ReplyDelete
  13. Mmependeza sana rafiki, pendaneni daima.Anitha umekubalika kichizi na familia yako mpya.kaza buti kwenye upendo, uko juu
    E.K.L One of four manyaras' - DOM

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 10, 2009

    lo familia nzuri anitha your luck my husband wako yuko cool,wakwe wanaonekana wana upendo ni bahati maanake nashindwa kuelewa familia nyingine ukiolewa na mtoto wao basi wanakua wanakuonea wivu kana kwamba unafaidi,hongera wanaonekana 100% they loves u.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 10, 2009

    michuzi me na my husb wangu we like u a lot infact your our idol,ure humble,intelligent,simple guy.one in a million in bongo,tukija holiday na sisi tutapenda kukutana na wewe.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 10, 2009

    sasa akila na mikono siku nyingine hatatumia nini?

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 10, 2009

    Jamani mwacheni Michu ajichane, ni heri yeye anapata hadharani kuliko nyie mnao jitia swaafi alafu kumbe mnapata kwa kujificha! Mwana endeleza libeneke achana na wazushi.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 10, 2009

    Hizo chopstick mithupu hazishikwi namna hiyo. Kweli uliweza kuinua kipande hata kimoja cha nyama hapo kwa ushikaji kama huo?

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 10, 2009

    anony Fri Jul 10, 12:52:00 PM unaona mbali sana! kula tano

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 11, 2009

    Hiyo michango yetu haijaisha tu?kumbe tulichanga pesa ya maana,khaaaa!

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 12, 2009

    hii noma sana, yaani hata B'day tuliichangia? sisi tulifikiri tunachangia harusi kumbe tulichangia mambo mengi eeeh! rudini bills zinawasubiri huku.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...