Vijana kutoka Tanzania wakifurahi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Beijing, China wakitokea Dar es salaam .Vijana hao wako katika ziara maalum nchini China kufuatia mwaliko alioutoa Rais Hu Ji Ntao wa China katika ziara yake aliyoifanya mwanzoni mwa mwaka huu kwa kutaka vijana kutembelea nchi hiyo.

Hapa vijana wanaonekana wakiwa ndani ya basi la kusafirisha abiria mjini Beijing tayari kuelekea hotelini.

mojawapo ya shoo waliyoandaliwa vijana Beijing
Vijana wa Tanzania (hawapo pichani) wakiwa na raia wenyeji wakiangalia Burudani zinazopendwa na kuwavutia watu wengi nchini China ikiwa ni sehemu ya makaribisho.Hapa ni Acrobatic show kiendelea katika eneo la Hujialou, Beijing.
picha kutoka angani ikionyesha sehemu na mandhari safi ya mji wa Beijing na jinsi ujenzi wa nyumba, ofisi,viwanda ,sehemu za huduma za jamii na mashamba ulivyokaa katika mpangilio na kulifanya jiji hilo kuvutia zaidi.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2009

    Nataka kuuliza kama kuna kijana wowote kati ya hawa ambae ametoka Zanzibar. Au ni ujumbe wa Tanzania jina tu?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2009

    Hivi mchakato wa kuwapata hawa vijana ulikuwaje au ndio undugunization na mafisadi

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 21, 2009

    hamna alietoka zanzibar wala alietoka kigoma kwakua zanzibar ni sehemu mojawapo ya tanzania kama ilivyo mafia au newala vile kwahio si lazima sana kila mahali patoe kijana aliekupo kwenye hio zira ya china...mkitaka hivyo na mie nitahoji kwanini hakuna mgosi yeyote alietokea lushoto,vuga,mtae au mombo?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 21, 2009

    Safi sanaaa Said!!!!!

    ReplyDelete
  5. Anony wa 12:01:00 AM nimependa sana jibu lako na shukrani kwa kuwashushua wabaguzi kama anony wa 1. Mikoa mi5 ya Zanzibar ni mikoa kama ilivyo mikoa mingine 26 ya Tanzania. Ukianza kuulizia Zanzibar ili iweje. Haya mi natokea Kusini, nikianza kuulizia kwetu je? Na kama yupo wa Kusini lakini anatokea Lindi nitalalamika Mtwara haijawakilishwa. Kama yupo wa Mtwara lakini anatokea Tandahimba nitalalamika Masasi haijawakilishwa. Na kama yupo wa Masasi lakini kama anatokea Mchaura nitalalamika kuwa wa Namalenga hayupo.

    Jamani tushirikiane na tujikubali wote kuwa ni watanzania na tuwamoja. Huu uzanzibari na ubara; mara sijui kanda fulani vs kanda fulani; mara udini; mara itikadi za siasa kwanini zitugawanye?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 21, 2009

    Mdau wa 12:01:00 AM na Mdau wa 12:47:00 AM mmetoa majibu sahihi kabisa. Napenda kuwashukuru sana. Kwa sababu hii, tujaribu kurudi nyuma na kusikiliza hotuba za Marehemu Baba wa Taifa Letu la Tanzania (TanZania), Mwalimu Nyerere: alisema hivi (paraphrasing....): Dhambi ya kuulizia kwa nini vijana wa Zanzibar hawakuwepo au tendo la kuulizia iwapo vijana wa Zanzibar walikuwepo au la, ni tendo linaloashiria kwamba utakapopata jibu la NDIO ni DHAMBI.... utaendelea kuuliza was pale Mnazi Mmoja walikuwepo, wa Pemba je? Na wa kule (unajua mwenyewe mwuliza swali). Hiyo dhambi itaendelea kukutafuna, baadae utakuja hakuna zanzibar, kuna pemba na maeneo yoote yanayotengeneza zanzibar. Hizi sio zama za kuulizia vitu vya namna hii ndugu. Angalia EU, angalia USA, angalia dunia imekuwa kama kijiji kimoja.......halafu wewe unaongela eneo moja..

    Naomba kutoa hoja

    ReplyDelete
  7. New YorkerJuly 21, 2009

    Hala hala vijana msije "mkajilipua" u-China mkidhani mtapata kazi za "Box"

    kwani wao wenyewe wanapiga "Box" ndani ya nchi yao na haliwalipi.

    China siyo New York muelewe hilo mapema, hivyo mjiandae kurudi nyumbani kulijenga Taifa.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 21, 2009

    Vizuri sana,

    Huyu Rais wa China kawa muungwana, ila sijui kama sisi (waTZ) tume'msoma'. Huko kwao (China) ni wazuri sana kwa Reverse Engineering (tofauti na copy & paste). Na inasemekana ndio mbinu waliyotumia "kuruka" katika technolojia. Yaani, wachina wana peleka ujumbe wa watoto pale ambapo wanahisi kuna techolojia mpya. Wakati wa ziara, kila mtoto anapewa zoezi la kukariri kipande cha mtambo, wakirudi hotelini wana fanya recontruction, wakirudi nyumbani wataalam wanapewa picha then wanai study (wana isoma) na mwisho huunda ya kwao, ila wakipita mle mle. Nasikia kiutaalam haya magari ya mizigo, " Jai feng" ni kama Scania (sweden) na hata kuzidi. Je vijana wetu watanakili chohote? au ni picha tu na simu? Tena wao wachina wakiruhusiwa kubeba kamera ndio kabisa mme kwisha.

    Mdau Kiwoso

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 21, 2009

    Aaaah ni balaa,mchakato ni kuwa wafuatiliaji wa mambo tu jamani.It was fair.MBIJE,A

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 21, 2009

    Mkuu wa wilaya hivi kweli katika kundi hilo kuna vijana wa kimatumbwi na wakule mbamba bay! Nikimaanisha uwakilishi au tu ni watoto wa kina fulani hapo Dar! Maana haya mambo yapo sana katika nchi yetu! Sidhani kama kuna uwakilishi wa mikoa hata 15 kati ya 26 ya Tanzania!

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 21, 2009

    jamani ndg zangu hawa WAMECHAGULIWAJE???? utasikia ni mtoto wa flani au flani! Yaani bongo!! yaani hatuna maana wala hatujasikia tangazo la kukaribisha maombi! Mnaopiga box kaeni huko huko huku hakuna maana

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 21, 2009

    Mimi ni kijana ninayejihusisha sana na masuala haya, nikisikia kuna shindano BBC nime, DW nimo, kama kuna kazi za kijitolea nimo, mashindani ya serikali za mitaa nimo, mbona hii sikuisikia na nilifuatilia sana ziara ya huyu bwana? Kama kuna mtu anajua hawa vijana walichaguliwa vp aniambie, simaanishi lazima ningeenda, but at least nisikie then ni-apply, but nothing

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 22, 2009

    Si mnaona kuwa kuna ubaguzi. SAsa mmefurahia kuwa hakuna kijana kutoka Zanzibar hili hamkuona kuwa tatizo. SAsa mnaanza kuuliza kama kuna vijana wa kimatumbi. Dhambi ya ubaguzi aliyosema Mwalimu Nyerere hiyo. Mmebagua wazanzibari kutokana na wanakotoka sasa mnabagua watanganyika wenzenu kutokana na tabaka gani wanatoka hao vijana. Nafasi wala hazikutangazwa wamechaguana kwa vigezo wanavyovijua wao. Huu ni ubaguzi na upendeleo.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 22, 2009

    mh sitaki kujua wamepatikana vipi ila sidhani kama kuna haki imefanyika katika kuwapata hao vijana.

    maana sijawahi hata kusikia kama kuna mchakato wa kuwatafuta vijana hao lol!

    hii ndio bongo bwana.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 22, 2009

    kuna watu/viongozi tuliowapa madaraka kwa kuwapigia kura...wanapenda kufanya watanzania wooote ni mazuzu sijui mbumbumbu!!!???

    ivi kweli unatupatia hii habari eti vijana wa kitanzania walioalikwa china...bila kutoa source ya walipatikaneje??...

    au rai jintao anawajua kwa majina akaipeleka barua direct kwa JK?

    sio kwa sababu eti watu wanaouliza ivo wanataka kwenda...ila ni swala la msingi

    vioja hivi

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 22, 2009

    ni kweli kijana apo juu 6:46pm

    ivi kwanini mtu akipata nafasi sehemu yoyote tu...asile kwa urefu wa kamba yake???? kwa mwendo huo apo juu unavoonyeshwa

    itakua unaweza kula kulaaaa..huwezi kula ujiju

    ni hayo tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...