Ashimba akiwajibika katika moja ya onesho lake ughaibuni
Wahudhuriaji kibao kwenye maonesho ya Ashimba ughaibuni.
Hili lilikuwa Denmark wakati wa uzinduzi wa albamu yake

ASHIMBA, MSANII ANAYEKUJA JUU KWA KASI KATIKA KUPIGA MUZIKI WENYE MAHADHI HALISI YA KITANZANIA HUKU AKICHANGANYA NA VIONJO (EFFECTS) VYA KIELEKTRONIKI ILI KULETA LADHA MBADALA AMEONDOKA TENA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 16 KUELEKEA NCHINI FINLAND AMBAKO ANATARAJIWA KUFANYA MAONYESHO MATATU.
BAADAYE ATAELEKEA NCHINI HISPANIA KWA AJILI YA ONYESHO LINGINE MOJA KABLA YA KURUDI TANZANIA HAPO MWANZONI MWA MWEZI WA SEPTEMBA.
ASHIMBA TAYARI AMEFANYA UZINDUZI WA ALBAMU YAKE YA KWANZA IJULIKANAYO KAMA “NURU NYIKANI” HAPO MWEZI WA JANUARI NCHINI TANZANIA NA MWEZI WA MEI NCHINI DENMARK.
ALBAMU HII INAPATIKANA KATIKA MADUKA YA NOVEL IDEA DAR ES SALAAM, ONE WAY DAR ES SALAAM NA ZANZIBAR PAMOJA NA DCMA ZANZIBAR. VILE VILE ALBAMU HII INAPATIKANA KATIKA ITUNE ONLINE STORES.

NCHINI FINLAND MAONYESHO YA ASHIMBA YATAKUWA KAMA IFUATAVYO:


19 AGOSTI LIBERTE - HELSINKI
20 AGOSTI CLUBI – TURKU
21 AGOSTI TAMPERE – TELAKKA

SAFARI HII IMERATIBIWA KWA PAMOJA BAINA YA MAISHA MUSIC TANZANIA NA UDUMOOD YA FINLAND

Kwame Mchauru
Maisha Music
PO Box 105094
Dar es Salaam
Tanzania
+255.777.461911

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. hao mapromoter akina nani huku finland?, mbona hatujasikia habari zozote kuhusu huyu msanii kutumbuiza huku finlannd?.

    ReplyDelete
  2. Ashimba msanii mzuri nilikuwepo kwenye show yake copenhagen DK ila alichotuangusha wabongo wenzie wengi tuliokwenda kumuunga mkono siku ile ni kuimba nyimbo zake kinyamwezi badala ya kiswahili sasa tukawa tumebakia kubungĂ a macho tu sisi wabongo tusiojua kinyamwezi ni sawa sawa kabisa na kwenda kumuona msanii alietoka Togo akiimba kitogolese.WASANII MNAOTOKA NYUMBANI IMBENI KILUGHA LKN PIA MSIKISAHAU KABISA KISWAHILI KINA ASHIMBA NA WENZIO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...