Serikali imepiga marufuku maonyesho yote ya filamu kwenye hadhara ya watu, majumba yasiyo rasmi,vibanda ,kumbi ndogondogo, hoteli na maeneo ya baa bila kufuata masharti ya jumba la sinema na kwa mujibu wa sheria na 4 ya mwaka 1974 inayotumika nchini.
Agizo hilo limetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo George Mkuchika wakati wa Uzinduzi wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu nchini ambayo itakuwa na jukumu la kukagua na kusimamia maonyesho na shughuli za filamu nchini.
Amesema sehemu nyingi zinazotumiwa kuonyesha filamu hazina leseni halali za kuonyeshea filamu na kuongeza kuwa sio salama kwa mali na afya za watu.
“Nachukua fursa hii kutoa onyo kwa mtu yeyote atakayeonyesha filamu kwenye hadhara ya watu katika majumba yasiyo rasmi ,vibanda,kumbi ndogondogo,hotelini, baa na katika vyombo vya usafiri waache mara moja” amesisitiza.
“Nachukua fursa hii kutoa onyo kwa mtu yeyote atakayeonyesha filamu kwenye hadhara ya watu katika majumba yasiyo rasmi ,vibanda,kumbi ndogondogo,hotelini, baa na katika vyombo vya usafiri waache mara moja” amesisitiza.
Amefafanua kuwa sehemu nyingi zinazotumika kuonyeshea filamu sasa hazikidhi matakwa ya ujenzi wa kumbi za kuonyeshea filamu na ni kinyume cha sheria kwani nyingi zimekuwa chanzo cha maficho ya wahalifu, majambazi, biashara ya dawa za kulevya na kuchochea vitendo vya ngono kwa vijana.
Amesema athari nyingi tayari zimeshajitokeza katika jamii yetu na kuongeza kuwa filamu nyingi zimechangia kubomoa na kudunisha Utamaduni wa taifa letu na hata kuchangia kwa kiasi kikubwa kubomoa misingi ya amani , Upendo , Uadilifu,heshima, uaminifu na utu ambao ni utambulisho wa mtanzania jinsi ulivyokuwa umejijenga na kuenea katika jamii yetu.
Waziri Mkuchika amewataka wanaojishughulisha na shughuli za kuonyesha filamu kwa kuzingatia sheria na kufuata kanuni za nchi licha ya kuwa ya fani ya filamu kukuza ni biashara na inakuza uchumi na pia kuleta maendeleo na kuwataka kuepuka kuonyesha filamu zinachochea vitendo viovu na mmomonyoko wa maadili ndani ya jamii kutokana na filamu nyingi kutokaguliwa na kupangwa katika madaraja kulingana na matakwa ya watanzania.
Aidha amesema serikali iko makini kuhimiza na kusisitiza matumizi ya sanaa katika masuala mbalimbali ya maendeleo na kuvitambua , kuvikuza na kuviendeleza vipaji vya wasanii katika kukuza taaluma na fani ya filamu nchini.
Awali akizungumza kuhusu majukumu ya Bodi hiyo amesema kuwa Bodi itakuwa na jukumu la kuweka misingi ya kuimarisha utaratibu wa usimamizi wa utengenezaji wa filamu na pia kutoa vibali vya kutengeneza filamu hapa nchini.
Mbali na jukumu hilo Bodi ya Ukaguzi wa Filamu itakuwa na jukumu la kuratibu, kusimamia na kushauri namna ya kukuza Tasnia ya Filamu kwa kuzingatia sera ,sheria na kanuni zikiwemo taratibu na miongozo mbalimbali ya nchi hasa sera ya Utamaduni na Sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza.
Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo Bi. Rose Sayore ameihakikishia serikali kuwa Bodi yake itafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha kuwa kanuni, sheria , maadili na taratibu za uonyeshaji na utengenezaji wa filamu zinazingatiwa kwa maslahi ya watanzania na vizazi vijavyo.
Vipaji vimeingiliwa na sasa mtaona bomoa bomoa hiyooooooooooooooooo.
ReplyDeleteSerikali, acheni kuwa wazazi wetu. Hizi ni fikra za kizamani na hazina nafasi katika miaka ya sasa. Je, mtafunga pia mitandao? Kwani, kila kitu unaweza kupata sasa katika mitandao kuanzia picha za hazina mpaka namna ya kutengeneza mabomu ya nyumbani.
ReplyDeleteKama mimi ni mtu mzima zaidi ya miaka 21, huwezi kuniambia nitazame picha hii na nisitazame ile kwa kuwa serikali haitaki nione picha za watu wazima. Huu ni utoto. Kama mnaheshima uhuru wa binadamu, hamuwezi kunikataza nisiangalie filamu za ngono kama nataka kuangalia. Kama tuna mitandao. Hii itakuwa sawa sawa na kuishi Korea ya Kazkazini au Burma au Cuba, kila kitu lazima uombe ruhusa ya serikali. Kwa nini msiendelee na kukataza uuzaji wa pombe au sigara? Kwani madhara yake ni madogo kuliko kuangalia filamu za ngono au mapenzi? Msitufanye sisi ni watoto wadogo kila tukiamka mnatupa lecture kama vile tuko katika siasa ya ujamaa na kujitegemea za enzi za kale.
Hapo kazi ipo kwani watanzania wengi wamefanya kuonyesha video ni sehemu ya kipato sasa kuwakatisha ghafla ni kuwaweka katika hali ngumu. Sijui serikali ilikuwa wapi miaka yote hiyo mpaka sasa hivi ndo waikumbuke hiyo sheria ya mwaka 74 na kuanza kuitumia ghafla! Well inabidi serikali itoe muda maalum sio kuachisha ghafla. Je kutazama filamu nyumbani na familia hilo litakuwa ni kosa kwa jamii. Itabidi swala hili liangaliwe kwa undani pamoja na athari zake kwani unaweza ukawakataza watu kuangalia filamu kwenye kumbi lakini wataangalia kwenye sehemu za maficho na utamaduni utazidi kuporomoka. Serikali itambue kwamba sayansi na technologia imekua kwa kazi na lazima nchi iendane na kukua kwa technolojia, hizi sio zama za kale ni kizazi kipya.
ReplyDeleteTunahitaji kuzungumzia swala hili kwa undani ninaona kama kuna mizengwe mingi ndani yake na sijui kama serikali itaweza kudhibiti swala hili nchi nzima!
Mdau USA
HII SERIKALI YETU IMETAWALIWA NA WATU WASIO NA UPEO WA KUFIKIRI!!KUNA VITU VYA MAANA VYA KUFANYA,INAWEZEKANA WAMESHAANZISHA MAKUMBI YAO MAKUBWA YA SINEMA NA MIKAMPUNI YAO YA KIFISADI
ReplyDeleteYaleyale UPUHUZI mtupu, kweli watu na Elim zao wamekaa na kujadiri upuhuzi huu kwa mwaka2009 kweli?
ReplyDeleteKwa kweli mbona serikali inatia kichefuchefu.Hivi tabia mbaya na kuvunjika kwa maadili kumetokana na filamu,Yalabi ebu nipeni nafasi nipumzike!Halafu wanakaa maprofesa wa wizara na maafisa wakuu na kutoa tamko la ajabu kama hili.
ReplyDeleteTunataka sheria zilizotokana na utafiti wa kina,sheria za kubuni,sheria zisizo na manufaa na zisizotekelezeka hazina nafasi kwenye karne hii.
Juzi wasanii walikaa na kuiomba serikali itengeneze sheria za kulinda kazi zao za sanaa.Jambo hilo ni muhimu mara mia moja kuliko hili la kujifanya eti uonyeshaji wa video kwenye mabasi na mitaani mwisho.Kwa manufaa ya nani? huku tatizo kuu la wizi wa kazi za sanaa za walalahoi wanaoganga njaa kwa kujishugulisha wakilifumbia macho.
Hakika ni wepesi kutoa matamko kwa mambo ya kitoto na yasiyo na maana sana lakini ni wagumu kama visiki kutoa matamko kwenye mambo yenye mshiko na maslahi kwa jamii ya wahangaikaji.
Sawa, wamezuia maonyesho ya video mitaani,je wamezuia watu kuangalia video hizo majumbani kwao? je wamezuia watu kuuza video hizo mitaani na madukani?je wamezuia mitandao kutoonyesha video tena zilizombaya kuliko hizi?je tofauti ya video kwenye majumba ya filamu yanayotambulika(formal) na ya mitaani ni nini?hawaoni ni viingilio tu lakini messages na ujumbe wa filamu hizo ni uleule.
Na kama sehemu tajwa juu hazikuzuiwa au kufutwa, hawaoni tabia mbaya na maadili kushuka itabakia palepale, tena yaweza kuwa mbaya zaidi kwani watu watajificha na kuanza kuangalia vichochoroni na kuongeza nafasi kubwa ya kutazama hata video mbaya za pono NK, au watakimbilia mitandaoni ambako ni kubaya zaidi.
Huo uhuru wa kupata habari uko wapi? kama serikali inataka kutupangia ni video ipi tuangalie na ipi tusiangalie.kwanza video mbaya ni ipi na nzuri ni ipi? Ni nani anaamua na kwa vigezo vipi? vya kidini, kama ndio, dini ipi? islamu,cathoric,sabato,orthodox,pagan,au vya kisomi,kisomi kipi,cha kifedhuri au cha kisayansi.Kwa taarifa yao video hipi ni nzuri kimaadili na hipi si nzuri is very subjective ukiondoa za pono tu,zilizobaki tutadanganyana,je video za kimapinduzi ni mbaya,je video za kujenga morali wa kugundua ,kufanya kazi,kupigania haki,mapenzi tuziweke upande upi.ze za mafunzo ya kujilinda.
Nawashauri serikali wafanye utafiti kwanza kabla ya kukurupuka.Kiutafiti tunaweza kusema kwamba,samahani ninakopi kwa kiingereza.
" There are a lot of confounding factors which may totally jeopardiza the effect of bad video to reducing Tanzanian's respected values and culture .They were supposed first to tell-us categorically how street video and not other confounders are the main source of deteriorating our national values. They were supposed to tell-us why beauty contest,European music,local(half naked)dances,mushrooms of 24 hrs night clubs etc are not the main factors and not affordable street videos.
Hivi huyu Mkuchika mbona ni kama anakurupukakurupuka hivi? Kwanza uwezo wa kupiga marufuku wa video au sinema za huko uswazi hana. Pili ambao wanaweza kuzuia ni wenyeviti wa mitaa ambao huwa hawalipwi kwa style hii tayari wamepata mlo. Huo ndiyo ukweli wenyewe. Mimi nazungumzia uzoezi. Jamani huko uswahilini maisha ni tofauti sana na kule Masaki na Mikocheni na Oysterbay jamani. Nenda Mazese, Vinguguti, Kipawa, Kiwalani hii biashara ya video hasa ya mashindano ya mpira ni kubwa sana na ndiyo vijana wanapata riziki. Bado mchezo wa pool amabo huko uswahilini huchezwa kama kamari. Hivi Mkuchika amefanya utafiti au anajitolea amri tu. Hebu waacheni vijana wajitengenezee ajira. Huko mpira na movies za ngono kama wenyewe wanavyoita la liga haina hata mipaka unakuta mpaka vitoto ambavyo hata kubalehe bado wanaenda kuangalia. Huo ndiyo utandawazi na soko huria. Too bad
ReplyDeleteSiku moja nilipata kuongea na Waziri mmoja wa Tanzania. Nikamwambia "..Mheshimiwa bado tupo nyuma katika masuala ya IT. Nafikiri kama mtapendekeza mawaziri na wabunge wapewe warsha za mara kwa mara juu ya maendeleo na matumizi ya IT litakuwa jambo zuri sana kwa sababu kuna wakati mwingine kauli za wakuu zinaonyesha dhahiri hawajui IT ni nini?.." Mheshimiwa Waziri akanijibu "..Wakuu wapo very up to date na mambo ya IT..Pia huwa wanapata mafunzo every now and then.." Akaninyamazisha na baadhi ya wajumbe aliofuatana nao wakapiga makofi.
ReplyDeleteBaada ya kikao kuisha Mheshimiwa Waziri akanifuata akaniambia "..Sijakuambia lolote wala usininukuu.. Hivi wewe unafikiri wale jamaa wanaweza kujifunza lolote jipya? Hawana muda wala interest. Ukitaka kuwapata waambie vikao na posho..Very disappointing fellows..Juzi hapa mwenzetu mmoja kamwambia Mhariri wa gazeti moja kwamba kalifungia gazeti lake. Yule Mhariri akasema ataenda kulifungua gazeti lake mtandaoni. Yule Waziri akamwambia hata huko mtandaoni tutalifunga satelite si yetu?..Haya niambie utasema nini?..Hawa jamaa wanajua kutuma email kusoma magazeti hapa na pale mengineyo kwenye IT hawayajui.."
Hapa naona taswira ya yale aliyoniambia Mheshimiwa Waziri. Film Censorship Board tuseme imezinduliwa tena kwa sababu ilikuwepo zamani. Wakati ule Filamu zilikuwa zinaletwa na wakala mbali mbali kupitia Tanzania Film company na zilikuwa zinaonyeshwa kwenye majumba maalumu ya sinema. Pia kulikuwa na suala la itikadi za kisiasa wakati ule wa vita baridi. Sinema nyingi za kimagharibi tulizokuwa tunaziona kwenye majumba zilikuwa ni action movies zilizokuwa zinaonyesha uhonvyo wa utamaduni wa kimagharibi.Filamu zilizokuwa zimetulia zilikuwa za Kihindi.
Kufikia miaka ya 80 zikaanza video (VHS)ambapo watu walikuwa wanaanza kutazama filamu majumbani mwao. Baada ya video kutawala biashara ya maktaba za kukodisha kanda za video ikatanda ikaua kabiasa biashara ya majumba ya sinema. Matakaokumbuka mtakumbuka jinsi jumba la sinema la Empire ilivyokubali ushindi wa video kwa kugeuka kuwa maktaba ya kuazimisha, video JO Traders Library.
Mheshimiwa Waziri pamoja na wanabodi kwa hali ilivyo sasa naomba mtueleze mtatumia njia gani kuchuja sinema? Halafu mtueleze ni sinema gani zinazoruhusiwa na zipi zisizoruhusiwa? Filamu Zinazoruhusiwa zinaruhusiwa na zisizoruhusiwa kwa kufuata vigezo gani? Wakaguzi wa sinema hizo watakuwa kina nani na watateuliwa au kusailiwa kwa vigezo gani?
Samahani, lakini kwa mawazo ya upesi upesi ninaona jinsi uamuzi wenu unavyotengeneza mwanya kwa polisi na mgambo wa city kuanza kuwasumbua waonyesha filamu kama wanavyowasumbua wamachinga.
Nadhani yule Waziri wa Habari wa Saadam Hussein alikuwa anaongea sense kuliko huyu wa kwetu.
ReplyDeleteTUSICHAGUE MAFISADI JAMANI,WAKISHAFIKA JUU WANATUSAHAU KABISA.
ReplyDelete