askari wa KAR katika tizi la gwaride enzi hizo
Serikali imewataka askari wa King's African Rifles (KAR) waliopigana vita kuu ya pili ya Dunia kuripoti katika ofisi za Mkuu wa mkoa au wilaya zao wakiwa na vitambulisho au vielelezo husika kwa ajili ya uthibitisho wa kutambuliwa .

Katika taarifa iliyotolewa hivi karibuni na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa yamehorodhesha majina ya askari wote waliopigana vita hivyo vya mwaka 1939 hadi 1945.

Taarifa hiyo inasema kuwa orodha ya majina ya askari hao inapatikana katika ofisi zote za mikoa na wilaya za Tanzania bara na Visiwani.

Mikoa hiyo ni Tanga, Arusha,Mjini Magharibi , Unguja na ofisi za wilaya ya Tunduru, Songea, Nchingwea, Bunda, Serengeti, Bahi, Geita, Temeke, Kisarawe, Ilala, Maswa, Babati, Morogoro, Mvomelo, Iringa, Kyela, Singida na Dodoma mjini.

Wilaya nyingine ni Kishapu, Masasi, Shinyanga, Kilosa, Karangwe, Kondoa, Tabora, Nzega, Mpanda, Kongwa, Biharamulo, Igunga, Misenyi, Muleba, Handeni, Namtumbo, mkoa wa mjini Magharibi na unguja, Wilaya ya Magharibi na Kusini Unguja.

Pia katika orodha hiyo ya majina kuna majina ya askari wa KAR ambao hawajulikani maeneo waliyotoka.

Zoezi la uhakiki wa askari hao limeanza kufanyika tangu tarehe 15/8/2009 na litamalizika tarehe 30/10/2009.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Saidia taarifa: hivi gwaride la hawa mashujaa huwa lini na wapi, nina maanisha hawa ambao kikweli kweli walishiriki vita hivyo? halafu nipe umri wa askari wa jeshi hilo ambaye ana umri mkubwa zaidi na mwenye umri mdogo sasa kwa sasa

    ReplyDelete
  2. wengi ni wazee na wamepotea na kusahauliwa vijijini.

    wazee wetu hawa walipigana toka north africa, maeneo ya abyssinia ambayo sasa ni ethiopia au eritrea, na kwenda mpaka burma.

    Muingereza ametambua mchango wa askari toka maeneo mengine lakini mchango wa wazee wetu toka AFRIKA haujatambulika.

    muda wa uhakiki ni mfupi sana na sijui wanafanya juhudi kiasi gani kutoa taarifa hizi.

    ReplyDelete
  3. Ha ha ha haaa!!!!!
    Na wale askari wa vita ya Maji Maji wakamwone Waziri Mkuu wiki ijayo.
    Mfalme Sina ,Meli, Mkwawa wende Ikulu kabisaaa kuondoa usumbufu!!!

    ReplyDelete
  4. Nahofia kuwa serikali imechelewa kwani wengi wao watakuwa wameondoka, na waliobakia ni wazee sana. Namkumbuka mzee mmoja alipita mpaka Malta na wa UK walimfundisha akawa fundi wa magari hodari sana. Alikuwa anaitwa mzee Kandela. Mara ya mwisho aliwaweka hoi mafundi wa kamata kwa kufufua Leyland iliyokuwa juu ya mawe.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  5. ...yan mnawakumbuka saa izi???

    ivi kweli nyie wazima?miaka yoote iyo mlikua wapi?mnawaacha wazee wetu adi sijui nini

    sasa mnawapa nini mnavowaita kiivi?tena hujui kama uyo mzee atafikaje-fikaje apo wilayani maana ni pesa ati!!!nauli

    ovyo sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...