AH, YANI HII MBONA NI YA KAWAIDA KABISA HAPA BONGO?
YAANI HATA MKITULETEA MABASI
YA GHOROFA SIE TUTAKWEA TU KAMA MINAZI VILE...

toka kwa mmoja wa wadau wa libeneke letu,
Eddymak

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. kabla sijachangia zaidi humu nina swali: Hivi hii ni tabia mbaya tu ya mtu binafsi ama ndiyo utaratibu wenyewe huu? au haya ni mazoezi ya ujambazi?

    ReplyDelete
  2. kweli bongo tambarare...wabongo mumefulia....

    ReplyDelete
  3. jamani.. jamani.. nchi yetu inakwenda wapi?? kama vile nchi haina viongozi inauma ssaanna yani miaka karibia hamsini ya uhuru mambo ndo kama hivi nini hii halafu mnanyanyasa wawekezaji si wengine wapewe vigezo tunataka na transport ya uhakika si wanaka almasi?? wataleta tuu mabasiya kumwaga kuliko hii mambo wananufaika wachache huku watu wanageuka tumbili juu ya magari kundandia hata visivyofaa hii ni hatari
    mdau, canada

    ReplyDelete
  4. YAANI BILA UBISHI HAPO MDAU ALIDAKA ZILE MOMENTS WAKAAZI WA MABIBO HOSTEL WAKIWAHI LECTURES MAIN CAMPUS MLIMAAAANI, HIZO NI ZA KAWAIDA KABISA ILE MIDA YA SAA MOJA KUELEKEA SAA MBILI ASUBUHI

    ReplyDelete
  5. Watu waishazoea. Nimeshuhudia mara nyingi hata kama hakuna watu wengi jamaa wanadandia kupitia dirishani. Mazoea yana taabu kuyaacha karaha. Jamaa alioa mwanamke aliekuwa malaya wake ambaye kila wakimaliza mamobo asubuhi wakiagana jamaa anampa shs 50 elfu. Jamaa siku za baadaye akamuoa. Usiku wa harusi asubuhi kachukua pochi akampa bibie. Bibi kamuuliza za nini? Akamwambia si ujira wako? Bibie akamwambia " Wewe vipi hujui mie mkeo?"!!!!

    ReplyDelete
  6. kazi ipo .. . .. ..

    ReplyDelete
  7. vibaka hao,wanawai mlimani ya wapi?!!!!

    ReplyDelete
  8. hiii itakuwa mbagala tu maana mbagala hata bibi wazee wanajua kuingia madirishani tena kwa kasi kubwa. akina mama wengi wa mbagala wanaotegemea daladala wanavaaga mapensi makubwa ili wapiga chabo wasione kitu!!!! wadau mpo hapo?


    mANGI WA K'KOO

    ReplyDelete
  9. aah aah aah tunashukuru mdau umefanya la maana sana kwani wabongo kila siku wanajifanya kujilinganisha na london au canada nafikiri hii ni LIVE mwenye macho haambiwi tazama wenzenu huku basi la abiria 40 hadi 50 mnaweza panda hata watu wawili na linaendelea na safari tena na kiyoyozi ndani jamani kipanya mnaingilia madirishani halafu mnapanda zaidi ya 30 hata mjapani akija bongo atashangaa sana kwani kipanya kinatakiwa kubeba watu wasizidi 6 au 8 tunaomba picha zaidi za mbagala tujikumbushe zama za giza
    mdau honover-germany

    ReplyDelete
  10. jamani bongo inawezekana kila mtu ni mwanajeshi maana hizo daladala bila kuwa na mabavu huwezi kupanda sasa sijui inakuaje kwa ndugu zetu walemavu na wazee(seniors)

    ReplyDelete
  11. duu duu siamini kama hao ni binadamu wa kawaida waingia kwenye usafiri kurudi home jamani tunaomba ufafanuzi au kuna vita jamaa wanawahi kukimbia nini hivi na lile joto la damu humo ndani ya gari hali ikoje?si kumejaa kikwapa tu humo?nafikiri serikali itafute njia mbadala kwani humo ndani ya basi lazima watu waambukizane magonjwa kama tb

    ReplyDelete
  12. jamani hivi serikali iko wapi/MARA WANAFUNZI WABAKIWE KWENYE MALORI UTAFIKIRI VIFUSI VYA MCHANGA,KUHUSU WATU WAZIMA MNAPIGANIA DALADALA UTAFIKIRI TIKETI YA KWENDA MBINGUNI HII NCHI NI BORA IBINAFISHWE ILI KILA MMOJA ACHUKUE CHAKE ATAKAYEZAMIA MTONI OK

    ReplyDelete
  13. jamani watanzania jaribuni kutembea duniani muone jamani suala la usafriri wa umma ni kitu kidogo sana wala hatuhitaji kusukumana na kungilia madirishani tembeeni jamani ili tujue la kufanya wenzetu magharibi wanatumia treni tena zinapita chini ya ardhi kama ni basi hayana hata kondakta jamani tembeeni tujifunze ili walau kuibadilisha nchi yetu

    ReplyDelete
  14. haiingii akilini eti huo ni usafiri wa kawaida nafikiri mabomu ya mbagala yamelipuka tena hivyo mimi nasubiri picha zaidi hakuna usafiri kama huo katika karne hii ya sayansi na teknolojia wakati binadamu wanasafiri kwenda hata kwenye moon

    ReplyDelete
  15. jamani hii picha siyo kweli kabisa mbona mimi naishi hapa dar maeneo ya kijitinyama hakuna watu kupanda dala dala kupitia madirishani huu ni uongo tu dar iko safi usafiri umetulia

    ReplyDelete
  16. haya ni maigizo au sinema siyo kweli bongo ni tambalale tu

    ReplyDelete
  17. umasikini ni kitu kibaya.

    ReplyDelete
  18. usafiri wa bongo ni mafunzo ya JKT

    ReplyDelete
  19. nitarudi bongo nikinunua gari langu unless otherwise siji

    ReplyDelete
  20. kabla sijachangia naomba nieleweshwe hii imetokea bahati mbaya?au ni mambo ya kila siku?je raisi kikwete anafahamu hili?au ni sehemu ya maisha bora kwa kila mtz?

    ReplyDelete
  21. tunaomba serikali ijifikirie mara mbili mbili je watu wanawezaje kuruka kama nyani au tumbili?

    ReplyDelete
  22. Haha nimekumbuka home jamani,kuwahi kazini hata kule Ukonga basi lolote kwenda Posta,Ubungo,Mwenge yote kama hujui kupita dirishani ujue kazini au shuleni utachelewa kila siku.Mara moja nilipita dirishani then ikawa mwendo wa kutoka saa 11 alfajiri.Mh Bongo tambarare.

    kris

    Netherlands

    ReplyDelete
  23. Kama sikosei hii picha ilitoka katika gazeti la Rai la mwaka 2006. Nadhani ilikuwa inaonyesha wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam wanaokaa hosteli ya Mabibo wakigombania daladala ili kuwahi darasani. Title yake ilisema "JAMANI WASOMI WETU". Nikipekua makabrasha yangu naweza kuipata!

    ReplyDelete
  24. Jeff Jeff Jeff Jeff...... bado hujanunua ki Bajaji tu?

    ReplyDelete
  25. dar es salaam ndio mji mkubwa na ambao umeendelea kwa kiasi fulani ukilinganisha na miji mingine tanzania lakini sijawahi ona kwa sasa watu wanapitia dirishani ila dar tu.

    ReplyDelete
  26. kweli bong tambarare!

    ReplyDelete
  27. Wabongo kwa kukana mambo, yaani hii ni tabia ayotufanya tushindwe kabisa kutatua matatizo yetu. Yaani, hii ni hali ya kawaida kabisa kwa maisha ya wasafiri wa dar na sehemu nyingine tanzania, halafu tunajifanya hatujui au hatuamini, huu ni unafiki.

    Bwana hiyo ndo hali halisi ya maisha ya bongo. Na hayo ndo maisha bora kwa kila mtanzania.Hakuna mengine zaidi ya hayo.

    ReplyDelete
  28. "AJALI INAYO KINGA"

    ReplyDelete
  29. Masangu asante sana kwa kufafanua, maana watu humu walishaanza hao wanaenda Mbagala, hebu jiulize kama wazijua daladala za Dar na mistari yake kabla ya kusema.

    ReplyDelete
  30. Hamna excuse hapa. Wenzenu hata kama ni kwenye mdomo wa kifo wanaanza kuokolewa wanawake na watoto kwanza, senior citizens, halafu minjemba ni baadaye. Sasa hapa ni usafiri tu kama ingekuwa ni kwenye kufa itakuwaje?
    Learn something from TITANIC

    ReplyDelete
  31. Hio tabia ni mbaya sana..... kuna watu wameshaizoea hata aibu hawana maana hata kama basi halina mtu lazima wadandie madirishani. Mtu yuko radhi hata akupige teke kama anaona umekinga njia ili mradi apate nafasi ya kupitia dirishani. Wakati mwingine hata kushuka utakuta mtu huyo anashukia dirishani na usipoangalia vizuri utakuta hata simu yako imekwenda.
    Tatizo ni kukosa tu ustaarabu.

    ReplyDelete
  32. Iyo ni Mabibo Hostel...Asubuhi kama una lecture saa 1 usafiri unakuwa wa shida sana,kwa iyo mambo hayo ya kupitia dirishani yanatokea sana.Nimeishi maisha hayo miaka 3 wakati nahangaikia nondo yangu ya B.com.Labda saiv mambo yamebadilika maana ni siku nyingi kidogo tangu nitoke maeneo hayo.Mambo yanabadilika saiv nimepewa Mitsubish na Kampuni kwa iyo full kipupwe...ELIMU OYEEEEEEE

    ReplyDelete
  33. Wa'bongo wa ughaibuni nyie tengenezeni vitambi tu huko mlipo,mkirudi Bongo shughuli ndo kama hii na huu ni utaratibu wa kawaida kabisa

    ReplyDelete
  34. KAKA MICHUZI NADHANI HAPO SIO DAR,AU KAMA NI DARNI MIAKA YA NYUMA AMBAPO MABASI YALIKUWA HAYAJAPIGWA MISTARI,KWA SASA MABASI YOTEEE YANA MISTARI UBAVUNI! JAMANI MSILOPOKE TUU BILA YA KUFANYA ANALYSIS!

    ReplyDelete
  35. HAPO MPAKA UNUNUE HAMMER YAKO NDUGU UMESOTA SANA NA NGWAMBARA UMETOKA.
    SERIKALI DOOOOOOOOOOOOOOO SOME THING PLIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIIZ!!!!!!!!!!!!!!!!!1

    ReplyDelete
  36. ha ha haaa uuwiii we mangi wa kariakoo mbavu zangu zinauma nimecheka sana na bado na kwi kwi ya kucheka BLOG YA JAMII IDUMU!!!
    mdau canada

    ReplyDelete
  37. Picha hizi nadhani zinapatikana kwenye blog ya jamii tu,na sidhani kama zinawekwa kwenye magazeti yetu ya nyumbani! Nadhani tunahitaji picha nyingi zaidi kwenye magazeti za style hii labda Wahusika watafunfua macho! 2010? CCM na ushindi wa Mafuriko tena! kaah!

    ReplyDelete
  38. Nyinyi waosha vinywa wabeba mabox mnaojidai na nchi za makabaila eti usafiri tambarare, waulizeni wenzenu walipotokea mpaka wakafika hapo. Mmesahau ule usemi wa cha mtu mavi.... Hivyo basi fungasheni virago vyenu mrudi bongo mtuletee mabadiliko kwani mcheza kwao.... Mkome kuicheka bongo, ni kama kujianika uchi wenu! We michuzi usinibanie hii!

    ReplyDelete
  39. Vipi Anon wa 01:22:00 Frid Aug 28 mbona hamasa na hamaki nyingi????!

    ReplyDelete
  40. we mdau hapo juu hata tukileta msaada utaisha kijuu juu tu wahanga wa mabomu kule mbangala walikuwa wanalalamika vyakula magodoro haviwafikii walengwa sembuse limsaada likuubwa nchi yetu kuna viongozi ambao ni wamimi sana ina mijicho mikubwa kwa tamaa na hii inatia kinyaa ebu fikiri lile limashine la kupimia ugonjwa wa moyo lilivyolala mbele pale muhimbili wakati ilikuwa ni moja tu pale hospital lol?! haiingi akilini hapo ndo tuseme huo ni msaada umejinyimaaa umehangaika huku na kule kutafuta mdhamini ili kuleta maendeleo kwenu then nyang'au mmoja anajikwapulia kwa manufaa yake binafsi nchi yetu kwa umimi acha tu ipo kwenye top 3 kwa msisitizo tatu bora duniani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...