Mkuu wa nani hii,
Sie wakazi wa Gongo la Mboto hapa Dar tunaomba utuulizie hawa jamaa zako wa TENESCO vipi mbona leo ya tatu LUKU huku kwetu ina kwikwi?
Leo wengine tumejilawa kuja mjini kununua LUKU mambo ni yale yale. Tena tumekuta wadau wa mjini wanapanga kuja Gongo la Mboto kutafuta LUKU. Tunaambiwa oooohh mtandao una kwikwi, sababu sijui TTCL wamefanya sijui madudu gani. Hebu tupigie chabo huko maana tunalala giza wenzio.
Au wewe hayajakukutaaaaa????
Wadau
Gongo la Mboto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Poleni sana kwa yaliyowakuta wandugu,je mmejaribu kutumia huduma ya Vodacom ya M-PESA kununua LUKU?
    Jaribuni kununua LUKU kwa huduma ya M-PESA kutoka kwenye simu yako , kama hujasajiliwa na M-PESA wahi sasa gharama yake ni bure kabisa.Gongolamboto wahi Vodashop airport ni jirani yako , kajisajili na M-PESA , deposit pesa yako , nunua LUKU ikiwa home raha mustarehe.

    MDAU : DODOMA

    ReplyDelete
  2. Ushauli kulala ngiza mbona ni jambo linaloshauriwa kiafya,Sioni sababu yoyote ya kuwa na mwanga unapo lala

    ReplyDelete
  3. samahani jamani ila GONGOLAMBOTO haikuwa planned kwa makazi ya watu maeneo yale ni mashamba nyie mmelazimisha tu kukaa mjini ili muonekane mpo dar na nyie so ni kosa lenu

    ReplyDelete
  4. Mhh mimi nimejaribu kutumia M-Pesa inasumbua na inachelewa sana sasa nimejiunga na ZAP ni bora zain unatuma hapohao na unapata majibu haraka sana

    Mbeya

    ReplyDelete
  5. mdau g/mboto mboni kawaida iyo?masaki umeme haufanyi ivo

    haki ya nani vile...sijawahi ona uwiii hii nchi Mungu asimamie kweli cardinal Pengo amesema "yani tusiongee sana tunazidi jaza hasira na jazba ndani mwisho tukabane koo"

    ivi kwanini twateseka ivi?LUKU kituko yan sept 09 twaanza katwa 3% ya "KUCHANGIA MRADI UMEME VIJIJINI"

    sina hamu sijui ni-mobilize watu vp 2010!!!!

    ReplyDelete
  6. inachelewa au haichelewi si zote unapata tu bora umepata Luku yako kwa njia rahisi, wa Zain atumie ZAP na WA voda atumie M-PESA, wewe anonomy hapo chini usilete ushabiki wa kibiashara hapa.

    ReplyDelete
  7. duh bongo kweli dunia ya tatu mpaka lini haya mambo yataisha?oops wacha niwahi kubeba box nikirudi tv uhakika maana huku umeme haukatiki.bongo tambarareeeeeeeeeeee!

    ReplyDelete
  8. Gongolamboto kila kitu tatizo,usafiri Mbagala wamesingiziwa, maji kwa kisima,umeme kwamgao,LUKU kupata kwa kwiki, mmmh, barabara za viungani utafikiri upo kijijini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...