MADEREVA WA MABASI YAENDAYO MIKOANI KUTOKEA KITUO KIKUU CHA UBUNGO, DAR, WAMEGOMA KUFANYA KAZI KWA KILE KINACHOSADIKIKA KUWA WANAPINGA HUKUMU YA KIFUNGO CHA MIAKA 30 JELA ALICHOPEWA DEREVA MWENZAO ALIYEKUWA ANAFANYA KAZI KATIKA BASI LA MOHAMED TRANS, LILILOPATA AJALI NA KUUA ABIRIA TAKRIBAN 25 SIKU KADHAA ZILIZOPITA,MAENEO YA KOROGWE MKOANI TANGA.
BASI HILO LA MOHAMED TRANS LILILOKUWA LIKITOKEA MWANZA KUJA DAR,LILIGONGANA USO KWA USO NA LORI LA MIZIGO .
HIVI TUNAVYOONGEA HAKUNA BASI LILILOONDOKA UBUNGO TOKEA ALFAJIRI NA ABIRIA WAMEBAKI KURUNDIKANA KILA PEMBE YA KITUO HICHO KIKUU CHA MABASI YA MIKOANI. YAANI NI TAFRANI TUPU.
GLOBU YA JAMII IPO ENEO LA TUKIO NA KAA MKAO WA KULA KWA HABARI NA TASWIRA ZAIDI BAADAYE KIDOOOOOGOOOO..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. michuzi bora wagome kwasababu mbona dereva wa treni wanaua hawa kamatwi na miaka yote hiyo kwani kabaka wangempa hata 3au 2 afadhali hakuna anaependa kuua ni ajali huwezi kuzuia.tairi likipasuka ujue miaka 30 hii aiji mbona wamemhukumu araka wakati kuna kesi za epa na wengine kesi zao haziendi wanaonea wanyonge mi sipendi uonevu huu ana familia yake ameiacha haina mbele wala nyuma.wanakurupuka sheria gani hiyo inatungwa hapohapo badala wahangaikie mafisadi wanahukumu vitu vidogo wafanye kwanza hizo za mafisadi sio kuonea wadogo.treni zimeua mara nyingi bajaji,pikipiki hawafungwi hivi,na dereva ni dereva,haijalishi anaendesha nini.hukumu iwe sawa lakini sio hiyo jamanii.

    ReplyDelete
  2. Bora wamegoma,kwani hizi mahakama zimekuwa zikiwaonea wanyonge tu,kwani mzee wa vijisent kesi yake mbona hatuisikii baada ya kuwauwa kina dada wawili kwenye bajaji? Si na yeye ahukumiwe miaka 30 basi.

    ReplyDelete
  3. Kauhukumiwa kwa kuonewa kabisaaa. Inaonyesha Serikali yetu jinsi gani inaovyoonea wasiokuwa na kitu. Mbona Chenge ameua tena yeye ni kwakosa la kizembe speed zimesababisha Eti kesi yake ipo inaguruma hadi leo bado uchunguzi unafanyika Iweje huyu aliyesababisha ajali kwa bahati mbaya ahukumiwe haraka hivi? Huu ni uonevu. Haki zitendwe kwa wote.

    Hatutatki tena wakicheza Watanzania wooote tutagoma. Vyombo vya Sheria hasa MAHAKAMA imetawala Ufisadi na Rushwa.

    ReplyDelete
  4. Asante michuzi kwa taarifa hiyo kwa mimi binafsi nasikitishwa na kitendo cha Mahakama kuchukua maamuzi hayo sita pingana sana na mchangiaji wa kwanza, Madereva wenzangu tuendelee hivyohivyo mpaka kieleweke tunaangalia sana tunapokuwa barabarani lakini ajari ni matokeo tu ambayo hayawezi kukwepeka mbona kesi zingine za wakubwa haishughurikiwi hivi Juzujuzi MH. Chenge kaua watu wawili lakini hakuna tunachoona kinaendelea jamani watanzania wenzangu tusiwe kama tunavyoitwa WATANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU tufuatilie mambo mpaka kuona mwisho wake Aksanten

    ReplyDelete
  5. Huyu dereva itakuwa hakuwa na leseni, hivyo ameshitakiwa kama yeye binafsi; kufungwa miaka 30 jela kwa kusababisha ajali ya barabarani haijapata kutokea..!!

    Mahakama ndio imeamua, sasa hao madereva wanagoma ili iwe nini au wanadhani Mahakama ni chama cha siasa?

    ReplyDelete
  6. wajiinga hao mtu auwe watu 25 halafu aachiwe nyie wajinga kweli, kwani alitakiwa ahukumiwe kifo miaka 30 ni michache sana, na na wewe wa hapo juu unachemsha wezi wa epa na kuuwa watu kwa uzembe ipi bora, kwa kweli wagome tu ila miaka 30 bado ni michache sana, watu wazembe kama haowanatakiwa wahukumiwe kifo, au kifungo cha maisha

    ReplyDelete
  7. Mbona mzee wa vijisenti kaua zamani sana hajahukumiwa au sheria inaendeje nielewesheni? Mimi kama mzee wa vijisenti atapewa naye mvua 30 sina tatizo kabisa na hilo.

    ReplyDelete
  8. Kugoma maana yake ni kuwa sheria zilizokuwepo zilikuwa legelege kiasi ya kuwa walikuwa awana woga nazo. walijua wakisababisha ajali hata kwa makusudi tu watalipishwa faini tu ama miezi mitatu kifungoni. imefika wakati kwa sheria hizi kutazamwa upya ili madereva wa mabasi wawe makini sana kwenye kazi zao.
    Ni kweli kuwa ajali aina kinga, lakini ni kweli pia kuwa baadhi za ajali zinasababishwa na madereva kwenda kasi sana. utakuta dereva analishusha basi kitonga kana kwamba hakuna kilima wala gema!!! ni ajabu sana. pia anataka kulipita basi lingine uku akiona kabisa kuwa mbele yake kuna gari linakuja tena kwa mwendo mkali.siungi mkono sana kifungo cha miaka 30 ila ni afadhali ili kiwe ni mfano kwa madereva wasiojali uhai wa abilia wao.

    ReplyDelete
  9. Hawa madreva ukiwasikiliza wana madai mengi ya msingi kama barabara mbovu, maslahi, karaha za askari barabarani n.k. lakini hili la dreva aliyefungwa ni la kipuuzi maana taratibu zote za kimahakama vilifuatwa na hukumu ikatolewa na hakuna anayeweza kubadilisha bila kufuata taratibu za kimahakama. Ila hii ni indicator mbaya kwa viongozi wetu maana karibu kila secta ya huduma inagoma maana yake nini?

    ReplyDelete
  10. SERIKALI HONGERA SANA!
    HUO NDIO MWANZO KAMA SHERIA LAZIMA IFANYE KAZI, KAMA SERIKALI ITABADILI MSIMAMO BASI WAO NI WAOGA, ILA KILICHOFANYIKA NI HAKI NA SHERIA KILA KAZI INA FAIDA NA HASARA INAYOSABABISHWA NA MWAJIRIWA NA SHERIA LAZIMA IFUATWE. TUTAKAA KWENYE UBABAISHAJI HADI LINI.

    SHERIA IFANYE KAZI, KILA MTU ATAHUKUMIWA KWA KOSA LAKE.

    ReplyDelete
  11. basi mzee wa vijisenti basi nae apigwe mvua hata 5 maana yeye ni muheshimiwa,kaa jamani!

    ReplyDelete
  12. kesi hiyo imewahi kupewa hukumu kuliko hata ya Chenge aliyegonga watu wawili na kufa

    ReplyDelete
  13. Hawa jamaa wanatuchinjachinja mno. Umefika wakati wa kutoa adhabu kali. Yaani ukikaa viti vya mbele vya mabasi utafika ukiwa umekwishateseka kisaikolojia. Yaani unamwona dereva ana-overtake kwenye kilima wakati haoni upande wa pili. Mwingine analiona gari upande wa ku-overtake lkn bado analifuata huko huko akiliwashia taa! Kama kweli wamegoma basi huo ni ushahidi kuwa adhabu imewagusa na watakuwa makini barabarani. Hapo ndo serikali inabidi ishikirie. Kwa vile panauma, watakuwa makini tu.

    Ukweli ni kwamba, kila atakayepata ajali atafungwa miaka 30. Mahakama lazima inaangalia kama kuna uzembe au la. Kama ajali imetokea kwa bahati mbaya basi mahakama itamwachia mtu huru. Kama ni uzembe basi unachukuwa 30 au zaidi.

    Kweli hawa jamaa waliishia darasa la 7. Badala ya kumchangia mwenzao akate rufaa mahakama ya juu wao wanagoma kuendesha mabasi! Sijawahi kusikia mahakama ikibadilisha hukumu kwa vile watu wamegoma sehemu fulani.

    ReplyDelete
  14. We Anon wa 10:49 na wengine mnaoona halali mahakama kumfunga dereva miaka 30, sijui kama mnajua jinsi nchi hii inavyokwenda, Laiti kama angekuwa yeye si wa kwanza kufungwa miaka yote hiyo wala tusingestaajabu, hebu fikiria mauaji aliyoyafanya chenge kwa kutembes service road, kibaya zaidi footage ya ITV inaonesha gari ya chenge insurance ime-expire muda mrefu, sasa kama sheria ni kwa wote iweje dereva achukuliwe hatua no sooner, ilhali Chenge lake limezimwa! KAMA NI SHERIA BASI IWE KWA WOTE!

    ReplyDelete
  15. Kila kazi ina ajali yake japokuwa wanauwa lakini kwa upande mwingine makosa ni matajiri zao ambao wanawatuma na kwa upande wa hao TRAFIC kila nikifikiria hizo sheria sijui wamezipata wapi za kujificha sehemu alafu kuanza kumulika tochi zao kwajili ya kupima mwendo wa basi sasa kwanini msiweke alama ya kuonyesha kuwa mahali hapo kuna trafic wa kupima mwendo mtu akiongeza mwendo ni haki yake kushtakiwa sasa mkijificha si kuwatafutia makosa madereva huku ugaibuni huwezi kuweka camera sehemu bila kutoa ishara watu wakaiona kwani ni makosa kuweka camera sehemu kwa siri ndio maana sehemu zote za camera zina ishara alafu mnawafunga madereva miaka 30 mtu ana mke na watoto kazi yake ni hiyo ikitokea bahati mbaya ameuwa basi akafungwe hebu niambieni kuna kazi isiyokuwa na ajali????? wataendesha maisha yao yote bila ajali????? acheni sheria za kimabavu fateni sheria za kweli tusonge mbele sio kila siku tunarudi nyuma rushwaaaaaa mpaka kutoa maiti muhimbili kama hujatoa rushwa jamaa hawakuonyeshi maiti yako TUNAMUOMBA MUNGU TUPIGE TAA UTUWAKISHIE MWANGA NDANI YA MIOYO YETU TUPATE ALAU IMANI KIDOGO KWA MAANA IMEKUWA BALAAA KUBWA SANA TUMECHOKAAAAAAAAA TUTAKUJA KULANA MISHIKAKI WENYEWE KWA WENYEWE OHOOOO...mdau uholanzi niwekeeni huu ujumbe kwani inaniuma sana .

    ReplyDelete
  16. Ndugu zangu mimi naona hii issue iko complicated, kwasababu kila mtu ana makosa yake.
    Barabara ni mbovu na zinachangia kiasi kikubwa kutokea kwa ajali.
    Madreva wetu vile vile kwa asilimia kubwa sio makini. Ni mara nyingi saana tumeambiwa madreva wamelewa na bado wanaendesha masafa marefu sana.
    Rushwa inachangia sana tena sana, kwa ufupi sheria ni kama hazipo kwani hakuna kinachofuatwa kwasababu fedha inaongea badala ya sheria.
    Sasa issue ni nini kifanyike ili kupunguza ajali?...Hakuna solution moja. it is a combination of everything....as so long as the system is broken we will keep losing people

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...