Anko nanihii,
naomba unisaidie kuniwekea
haya maoni yangu kwenye global yetu ya jamii.
T.F.F. NAOMBA MWONGOZO...
Kwanza nianze kwa kusema kwa wale wataalamu wakukimbilia kutoa matamko ya kulaani kila wanaloona haliwapendezi,wale wenye uchu wa madaraka na wale ambao hawapendi kukosolewa naomba radhi kwa hili.Lakini ni imani yangu Tf.f. mtanipa mwongozo .
Waraka wangu huu unahusu jambo moja ambalo kama si mimi peke yangu basi kuna watanzania kama mimi ambao lina sumbua vichwani mwetu.
Mimi ni mmoja kati ya wapenzi wazuri wa soka la nyumbani hasa baada ya mabadiliko ya uongozi wa juu kutoka iliyokuwa FAT na sasa T.f.f iliyokuwa chizi ya Ndugu Tenga.Lakini kuna swala moja ambalo kama wanaweza kunisaidia ili niwezekupata jibu,KWANINI TIMU YA TAIFA IVAE JEZI YENYE AIDHA RANGI NYEUPE AU YENYE MICHIRIZI MEUPE?
mimi hapa napata taabu kidogo kuelewa ilikuaje mmeamua kutumia nyeupe ambayo haipo kwenywe bendera yetu ya nchi,kama taifa stars ni ya watanzania wote wanaopenda soka na wasio penda soka ikiwa inawakilisha watanzania wote.
Hebu tukumbushane kidogo leo hii ukiingia kwenye tovuti ya Tff ambayo bado ina nembo ya FAThili nalo ni kosa,utakuta kuna jezi za aina mbili nyumbani inaonyesha buluu na njano ukicheza ugenini ni kijani na buluu kama sikosei na soksi na bukta ni nyeusi ambazo zote hizi zinawakilisha rangi zetu kitaifa,sasa hii nyeupe imetoka wapi labda nikumbushe Bendera ya nchi yetu ina rangi nne ambazo kila rangi inamaana mfano;
RANGI YA KIJANI-mazao yetu,
RANGI YA NJANO-madini yetu,
RANGI YA NYEUSI-asili yetu,
RANGI YA BULUU-bahari yetu.
Sasa hii nyeupe imetokana na nini?hebu nisaidieni ili nielewe.Sina ugomvi na Tff namheshimu sana Rais Tenga ni mtu mwadilifu,mcheshi,mchapa kazi mpenda maendeleo ya soka,lakini kwa hili sipendi wanaotakakumchafua wafanye ndio sababu,kumbuka uncle Tenga ukiwa unagombea nafasi fulani unatangaza sera na unapo pata hiyo nafasi unaendeleza sera zako.
Sitarajii malumbano wala ugomvi nimatarajio yangu kama mtanzania nimeliona hili naomba mwongozo kutoka kwenu Tff.
Kumbukeni leo hii kuna mchakato wa kutafuta vazi la taifa sio kwamba tulikuwa hatuna lilikuwepe lkn limepotea,sasa hatutaki rangi ya timu ya taifa(jezi)ipotee.
Najua Tff mmefanyakazi kubwa sana kuwafanya watanzania kuvaa jezi yao tofauti na huko nyuma tulishaona timu ya taifa ikivaa jezi ya Agentina kwale wapenda soka watakubaliana nami.Ndio maana mimi nataka kujua kulikoni taifa stars kuvaa jezi nyeupe?
FAT ya Ndolanga iliweka au ilikuta hizo jezi ambazo tuna ziona kwenye tovuti yenu ,leo FAT haipo lakini kuna mambo mazuri ambayo wameyaacha ya chukueni mfano hili la jezi,sio lazima ziwe zile walizo acha lakini ziwe na rangi ya kitaifa.
Ndugu zangu timu ya taifa sio timu ya mtaa,wilaya,au mkoa timu ya taifa sio chama cha siasa ndio maana Rais wetu mpendwa Ndugu J. Kikwete ameweza kutuletea kocha wa mafanikio ambaya anamlipa.Sasa kama bendera yetu ina rangi nne lakini hamna nyeupe ila kuna mtu au kikundi kinataka kufurahishwa sio kwenye timu ya watanzania wote(Taifa stars) msilipe nafasi.Tusiige mataifa yaliyo endelea turingie utaifa wetu rangi za uridhi alizotuachia Baba wa Taifa(mwl j.k. nyerere)ni nzuri na zina sura ya utaifa.
Ushauri wangu kuna jezi ambayo ilitengenezwa na Zizzou Fashion ina rangi zote za taifa ila ina rangi nyeusi mabegani buluu hii inafaa kama inge boroshwa kidogo.Najua kila kitu kina historia hapa duniani lakini hii rangi nyeupe ina historia gani kwenye nchi yetu.
Nawaheshimu watendaji wote waTff ni imani yangu mtayafania kazi haya nilioomba mwongozo na niliojaribu kuwashauri.tunataka taifa letu liwe na rangi moja kuanzia riadha ambao una watambua bila kusoma jina,hasa sisi tuliombali na nyumbani.
Mungu ibariki Tff
Mungu ibariki Tanzania
BABAvickAlicE
TAFADHALI MKUU WA NANIIII NILINDE E-MAIL YANGU USIIWEKE PEUPE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. MDAU NA MIMI KABLA HUJAJIBIWA KERO YAKO NINA SAHIHISHO LANGU KWAKO KIDOGO NAAMINI HUTAKUWA NI WEWE PEKE YAKO TU HATA MIMI NILIKUWA HIVYO PIA NA WENGINE KIBAO UTAWAONA WAKIJITOKEZA HAPA AMBAO NAO BADO WAKO HIVYO,SI NIA YNG KUWALAUMU ILA NITALAUMU ELIMU TUNAYOPEWA SHULENI KUHUSU MOJA YA RANGI ZILIZOKUWEPO KWENYE HIO BENDERA YETU YA TAIFA AMBAYO NI "BLUU"(BLUE)KWA MTAZAMO WNG MIMI. RANGI YA BLUE NI MAKOSA KUSEMA INAWAKILISHA BAHARI YETU NA MITO NA MAZIWA KWAVILE BAHARI,MITO NA MAZIWA NI MAJI NA MAJI HAYANA RANGI YA BLUE MAJI NI COLOURLESS HIVYO NI VYEMA TUNGESEMA LABDA BLUE IWE NI MAWINGU AU ANGA NA KAMA SIKOSEI ILE RANGI INAYOAMBIWA NI BLUE KWENYE BAHARI NI RANGI YA ANGA (SKY)ILE.
    ASANTENI/KARIBUNI

    ReplyDelete
  2. Acha longolongo wewe hiyo rangi nyeupe haibadilishi bendera ya TZ kama rangi zilizopo kwenye bendera yetu zinawakilishwa! kuna mambo ya maana ya kujadili kama jinsi ya kuboresha ranks na league kiujumla labda tujiulize kwanini hamna au TFF website haiwi updated au haina mvuto au viwango duni?

    ReplyDelete
  3. NI VIZURI KUWA NA JEZI ZA TIMU YA TAIFA AMBAZO ZINA MCHANGANYIKO WA RANGI AMBAZO ZINAFANANA AU ZIPO KWENYE BENDERA YA TAIFA HASA KWA JEZI ZA MECHI ZA NYUMBANI(HOME KIT).

    KWA JEZI ZA MECHI ZA UGENINI(AWAY KIT) MNAWEZA KUCHAGUA MCHANGANYIKO WOWOTE WA RANGI UTAKAOWAPENDEZA AU KWA MALENGO YA MNACHOAMUA KUONYESHA AU KUTANGAZA.

    LAKINI KAMA HAPO NYUMBANI TUNACHAGUA CHAGUA TU RANGI BASI RANGI NYEKUNDU PIA TUJALIBU KUITUMIA, HAPA SIMAANISHI ILI WATU WA SIMBA WAIITE TAIFA STARS KUWA YAO AU WATU WA YANGA WASEME STARS IKIFUNGWA BASI IMEFUNGWA SIMBA LA HASHA ILA KWA SABABU ZA KISAYANSI AMBAZO ZIMETOKA HIVI KARIBUNI KUWA TIMU ZINAZOFAA JEZI YA RANGI NYEKUNDU ZINA NAFASI KUBWA YA KUPATA MAFANIKIO UKIRINGANISHA NA RANGI NYEUSI. HUU NI UTAFITI NA SABABU ZIMETOLEWA KWA NINI ILA SINA HAKIKA KAMA WENZETU WA TFF WAMESHAPATA HABARI HII.

    ReplyDelete
  4. Acheni ujinga nyie...rangi ni rangi tuu.mbona Italy jezi yao siku zote ni BLUE na haipo kwenye bendera yao???Ili mradi rangi imependeza hamna shida...BONGO TAMBARAREEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  5. sasa ndo nini kuandika article ndefu kama gazeti!! tukishaona urefu wa article, hata kusoma wengine hatusomi, kwanini usifupishe barua yako!! argh! watu wengine bwana!munataka mufunzwe kila kitu, kwanini isiwe logic!!
    nana

    ReplyDelete
  6. Wewe acha zako wewe...mbona unatoa mfano wa Argentina ambao utakukaba?Argentina jezi nyeusi wanaitumia sana tu kama away kit... Jezi ya Taifa Stars ile nyeupe ni away kit...huitumia kama kwenye mechi ya kirafiki na kongo kwasababu congo walikuwa na Blue...kama unataka kujua tunawakilisha kitu gani kwa nyeupe, basi tunawakilisha maziwa ya ng'ombe, si ni meupe...tehetehetehe...ni hayo TU!

    PS:SIJAIPENDA JEZI YA TAIFA STARS KWASABABU YA MIRANGIRANGI KWENYE UBAVU, OVYO SANA NA WALA SIWEZI KUINUNUA, WABADILISHE JEZI ANGALAU WARUDIE ZILE JEZI AMBAZO ZILIMFANYA NADIR CANAVARO ADAIWE...ZILE NDIO JEZI ZA UHAKIKA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...