Tanzania nchi yetu bado tuko mbali sana! Hivi tutaendelea lini ndugu zangu watanzania? Ukiacha wachache wanaofurahia maisha mazuri, je ni lini wananchi wengine wataacha kuteseka? ni nini hatima ya watoto wetu?
Ni lini watu walio madarakani watafanya kazi kwa niaba ya wananchi wote??
Ni lini wafanyakazi wataacha kufanya kazi kwa manufaa yao wenyewe?
Ni lini serikali itaacha kutegemea misaada kwa kuendesha nchi na kutegemea rasilimali yetu wenyewe?
Ni mpaka lini utaweza kufanikiwa kufanya jambo nchini bila kumjua mtu madarakani au kutoa rushwa? Ni lini ajali za barabarani zitaisha?
Ni lini wanafunzi wanaosomea udaktari, ungineering na masomo mengine nje ya nchi watapata hamu kurudi kufanya kazi nyumbani badala ya kung’ang’ani nchi nyingine?
Ni lini viongozi wataacha kuoneana aibu na kulindana wakifanya makosa??
inauma sana moyoni ukifikiria, nchi nzuri yenye kila aina ya Baraka; mlima mrefu Africa uko kwetu, mbuga kubwa za wanyama zipo kwetu, maziwa na mito mirefu ipo kwetu, madini kama tanzanite, almasi, gold tunazo, ardhi nzuri kwa mazao tunayo, nchi ipo kwenye pwani ya bahari ya hindi, population karibia million arobaini, ni nini zaidi Mwenyezi Mungu atupe??????
Ni laana au uvivu na uzembe?
Demokrasia ya kweli itakuja lini kwetu Africa?

I’m pledge to my fellow youths of Tanzania, we are the only one’s who can rescue our country. I agree it is going to be a hard work but we don’t have a choice! The future of our country is in our hands. It is time to take action, to make a change, to take a stance and believe in ourselves in order for us too build a strong and empowering nation that we truly are, not only for ourselves but for our future generations, generations that will look back to this very day this day we made the decision to make a change.
We are to stop blaming each other instead let’s come together, support each other and come up with a solution to the problems that have somehow managed to manifest the ugly and undeniable truth of a nation that has fallen behind! A nation that has allowed greed, money and power to take over and therefore take control of us we must open our eyes and look and see that we as a nation cannot ignore the truth anymore.
There so many smart Tanzanian all over the world and if we can come up together, we can change our country for better beyond our wildest dreams! It can be done, I know it can.
I have been in Australia studying and I can see how this country operates, some of things that make Australia great are as simple as anyone can imagine but needed dedications from people of the country. As president Obama said in Ghana, that African nations should solve their own problems and not depending on western countries for their own developments.

Rais wa nchi peke yake awezi kuleta maendeleo kama wananchi hatuwezi kusaidia. Kila mwananchi kwa njia moja au nyingine ana wajibu wa kusaidia kuendeleza taifa. Maendeleo ya nchi yeyote yanaanzia na kitu kidogo kama idea.
Ideas ndiyo ufumbuzi pekee tulionao sisi vijana katika kuendeleza nchi, tukianzisha chombo ambapo tutaangalia matatizo makubwa tuliyonayo na kila mtu alipo akija na njia ya kutatua tatizo nina uhakika tutafanikiwa.
Kwa mfano
(1) tatizo la ajali barabarani serikali ingeanzisha point system kwa madereva wote waopakia abiria wawe na special licence yenye point kumi, kila akifanya kosa anaondolewa point mbili na kupata faini kubwa na askari anayemshika anapata percentage ya faini aliyopewa na pia kupata point kwenye kuongeza cheo au kupata mkopo (win win situation, abiria wanasafiri salama na askari wanapata faida badala ya kuchukua rushwa) .
(2) Utalii ni moja ya sector kubwa ambayo Tanzania inaweza kujivunia lakini bado utufanyi vizuri kama vile tungeweza, Nchi kama Kenya, Angola, Namibia wanajitangaza kwenye CNN sisi bado tumelala.
(3) Traffic violation in cities, watu wanashindwa kufuata sheria za barabarani kama kusimama kwenye traffic lights, drink driving hii ni opportunity kwa jeshi la polisi kutengeneza pesa kwa kufaini watu wa namna hii seriously.
(4) tatizo la foleni dar ni suala ambalo linahitaji ufumbuzi mkubwa, watu wanaongezeka na magari yanaongezeka lakini barabara zipo bado vilevile labda umefikia wakati ambapo city council itahitaji kupunguza idadi ya magari yanayokwenda city centre kwa kutoza ada ya kwenda jijini na gari lako.
These are some of many ideas that I have got on how we can move forward and I’m sure their many Tanzania elsewhere with even better ideas, so if we all can contribute our views we can somehow help our lovely nation. I know there are few people that will criticize my opinion but that is our biggest problem that we have as people!! Moreover being positive is all we need to achieving our dreams!
Thank you for your time and hopefully youths of Tanzania we can work together.
J. KIONGOLI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. jafari kiongoli ni wewe wa ifunda
    naomba tuwasiliane basi kama ni wewe ni mdau wa ifunda miaka hiyo

    ReplyDelete
  2. Kiongoli, nashukuru kukusoma na kufahamu kuwa kumbe wapo wenye uchungu na hasira na nchi hii na wangetamani sana kuiendeleza tufikie mahali tujihesabu nasi wabarikiwa katika dunia hii.
    Nafurahi sana kusoma na kufahamu kuwa watu wameamka na wana HASIRA ya kimaendeleo. Ninafurahi na kutiwa moyo sana sana.
    Penye nia pana njia, huu ndiyo mwamko wa mageuzi.
    Huanza kwa kuwaza, baadaye kunena na kisha kutenda.
    Naam, la mgambo linalia... ajidhaniaye amesimama aangalie asianguke.

    ReplyDelete
  3. J. Kingoli umenena ukweli nakuunga mkono Tanzania inatia huruma.
    Haionyeshi matumaini yeyote, viongozi tuliowachagua wanasikitisha.
    Ni muhimu viongozi wakawa mfano wa kubadili fikra za wananchi kutoka hapa tuliko kwenda kwenye neema.
    Sasa hivi asilimia kubwa ya watumishi ni wezi, kila mtu akiingia kazini anafikiria aibe vipi na kiasi gani kwa manufaa yake binafsi.
    Namna hii tunaliangamiza taifa

    UKWELI JE TUNAZAA WATOTO ILI WAJE WARITHI UMASKINI USIO NA TIJA KATIKA NCHI ILIYOJAA NEEMA. NA WATOTO KUWARITHISHA TABIA ZA WIZI, UMABAVU, UONGO...NDIO TUNACHOTAKA??

    INABIDI UTUMISHI WETU TUFIKIRIE VIZAZI VIJAVYO NA TUSIJIFIKIRIE WENYEWE

    KWA KUSEMA HIVYO, NAKUSUPPORT MIA KWA MIA WE REALLY NEED CHANGE..

    ReplyDelete
  4. TANZANIA KILA UKIAMKA KUNA HADITHI MPYA AMBAYO ITAPATIKA TANZANIA TU.

    1.HIVI MAJUZI MBUNGE JOSEPH MUNGAI,ANASEMA BUNGENI HAONI LOGIC YA KUKATALIA ARDHI KWA WANANCHI WA EAST AFRICA KAMA HIYO ARDHI HAITUMIKI.MTU KAMA HUYU ALIKUA WAZIRI,LAKINI BADO HAJUI THAMANI YA ARDHI YETU,ANATAKA NA WAGENI WARUHUSIWE KUMILIKI ARDHI.

    2.MKURUGENZI WA TANESCO KATUMIA MILIONI 600 KUKARABATI NYUMBA YA TANESCO ILI AINUNUE KWA MILIONI 60.HIVI INAINGIA AKILINI?

    3.WATU WA TRA MAKADIRIO YA KUTOZA KODI PALE BANDARINI HAWATOFAUTI NA WAGANGA WA KIENYEJI(WAPIGA RAMLI),HAWAFUATI SHERIA,WANAJIPANGIA WENYEWE,RUSHWA NDO USISEME.

    4,HIVI HATUWEZI KUANDAA MGOMO NCHI NZIMA SIKU MOJA?

    5.NASIKIA SASA HIVI HELA YA UCHAGUZI WA MWAKANI INATAFUTWA MNO.

    6.MICHUZI USIBANIE COMMENTS HII,NADHANI NA WEWE NI NJAA KALI,HUNA HAJA YA KUFICHA UKWELI,ACHA BLOG YA JAMII IWE YA JAMII.

    ReplyDelete
  5. Kaka mawazo yako yamesimama sana, uliyoyaongea yooote ni ukweli mtupu, sisi wadau wenzio tunakuelewa vizuri sana, ila swali ni je wahusika unadhani hawayajui haya??
    Hapa kaka ni kama kuwapigia mbuzi gitaa, inaingia sikio moja, inatokea kushoto, kwa kuwa wengi waliopo kwenye system wanawaza ni vipi watajenga majumba ya kifahari, ni vipi watoto wao wataenda kusoma nje, nk, hivo hawawezi kupata mda wa kukufikiria wewe na mawazo yako mazuri.
    Tatizo lingine ni kuwa, vijana wenzetu wamekua wakiingia kwenye system, na tunapata matumaini kuwa labda mambo yatabadilika, ila kwa kuwa systme zote ziko corrupt, basi na wao aidha kwa kupenda au kutokupenda wanajikuta wamefata mkumbo!
    Mi ntazidi kusisitiza tu kuwa, hii nchi ipewe jeshi lituongoze hata kwa miaka 10 tu! nadhani watu waliojisahau watakaa sawa.

    ReplyDelete
  6. unalosema ni kweli kabisa,nitakupa mfano wa kweli uwanja wa Ndege-JNIA siku moja natoka Ughaibuni nilikuta nimeobiwa simu nne kwenye Begi langu na lilikuwa limebomolewa upande mmoja.
    Nikaomba msaada zirudishwe mara moja nikaona zinacheleweshwa, ndipo mfanyakazi akaanza maswali mengi mara umebeba nini kwenye hand lugagge mara mara aniulize hizo Laptop umepata wapi Nzuri hebu washa tuone kuna nini ndani?,nikaangalia mstachi wake, na mwanamke mmoja bonge alikuwa Pembeni na majibu ya dharau.
    Basi mwishowe nikawatolea uvivu nikawaambia wazi wazi, naam mimi ni mtoto wa kigogo fulani kama hujui, naam jamaa alitetemeka, akesema basi basi zima, bosi tunashugulikia upotevu usiwe na shaka.
    Nikwambie ndani ya lisaa limoja simu zote zikapatikana.
    Unajua saa nyingine inabidi kutumia vyeo sio kama unapenda ila unalazimika kutokana na maudhi yanavyozidi.
    Mdau
    Mtoto wa kigogo
    asiyependa longolongo.

    ReplyDelete
  7. kaka michuzi habari za kazi!!!
    Mdau wa australia amenigusa sana na hata imebidi nilie tu, mimi ni mfanyakazi wa serikali na nasoma kwa sasa katika nchi mojawapo iliyoanza mabadiliko ya kimaendeleo katika kipindi cha kuanzia miaka ya 1970s. Huyu mdau ameona wenzetu walivyo makini na mambo muhimu. Nilichokiona mimi bila kubadili mfumo mzima wa kupeana kazi kwa kujuana hatuwezi kuendelea hata hadi yesu anarudi. Mawazo ya mdau yanafaa lakini ni nani ambaye ata enforce those regulations and rules? kama ni serikali hii ambayo mtu anafanya kosa then in mtetea mie sidhani kama tutafika huko.
    Cha msingi ni kujaribu kubadili uongozi ili hata kama ni mara kumi lakini tutapata watu wenye uchungu na nchi yetu iliyojaliwa kila aina ya utajili. Kaka nina mengi sana lakini naomba uniwekee hii taarifa ili niendelee kuchangia.
    Ni mdau mchumi wa Tanzania

    ReplyDelete
  8. We will get there if and only if the following are considered carefully,NOTE:not all though,this is on my perspectives.

    -Foreign Direct Investments in infrastructures,factories etc

    -Subsistence agriculture to financial globalization

    -Goverment should think and act strategically.From Socialism back to capitalism.

    -Corporate social responsibilities

    -National competativeness in businesses.There are factors to consider, demand,extent of rivarly etc

    -enterpreneurship.Most SME (small and Medium sizes entities)contribute heavly in counrty GDP

    -Invest in education,train more teachers and pay them adequately,build more schools.

    -Invest in healthcare system,train more doctors,nurses.

    -Political issues.Notionally,TZ is multiparty state but is effectively monoparty.

    -effective distributed leadership.
    -Implications of microfinance,microsaving,microcredits,does it real work?

    -Property market.People in the west thought property ownnership is one way betting-is it?Not really,most now are in negative equity.

    -General security of the country.it is not safe,need to be secured against crimes even cybercrime- fibre optics??

    -Infrastructures,scale public systems,services,facilities,power and water supplies ,transpotation,telecommunications,roads etc.

    -Fighting corruption,bribery, UFISADI though Forensic accounting etc
    -Reducing over dependence on IMF and World bank as They seek to represent Africa in major meetings such as G20.Making sure though,dependent aid meets requirements.

    -Public servicing organizations to provide VFM(value for money)services,which is Efficiency,Economy,and effectiveness.

    There are several more solutions to consider to ensure prosperous future,I will write them down to email Kaka MICHUZI.

    I heard your call,I need to see collective action first rather than risking my life.I need Dr Shayo,Mr John Mashaka, C Mukuru,Mr US Blogger and many others on board.

    Mdau ( John ) UK

    ReplyDelete
  9. Wadau sasa inabidi kweli tuamke, namaanisha tuweze kutetea haki zetu, hivi tunashindwa hata na RWANDA nchi yenye nyani tu ila inaingiza wageni 910,000 wakati sisi tuna kila kitu tunaingiza 600,000 HIVI TUMELAANIWA? NILINI JAMANI TUTAFAIDI UTAJIRI WETU?

    HIVI HATUWeZI KUIGA HATA WANZETU KENYA, ANGALIA MAMBO YAO YANAVYOKWENDA BOMBA, SHIRIKA LA NDEGE,MABENKI, VIWANDA, SISI WADANGANYIKA TUMEZIDI UWOGA, MTU ANAONA KITU KABISA LAKINI HASEMI MPAKALINI JAMANI??????? WATANZANIA TUAMKE, VIONGOZI WA DINI ITISHENI DUA YA KUOMBEA NCHI VIONGOZI WOTE WANAONGALIA MASILAHI YAO BINAFSI WAONDOLEWE NA MUNGU MWENYEWE, JAMANI HII INATISA TUNA KILA KITU ILA UMASIKINI UNAZIDI TUUUU

    Nkya
    A-town

    ReplyDelete
  10. Wadau, mkiajiriwa TRA kwa mshahara wa laki nne, halafu akaja mfanyabiashara ana kontena zake 3 akakuambia Mdau nitolee mizigo yangu katika siku 2 kuna milioni 2. Kama wewe ndio decision maker utamfanyia usichukue hela au utachukua?
    Mchangiaji.

    ReplyDelete
  11. ... yote ni kweli...
    na ni kweli labda tupate jeshi na likatawale ili watu wote tuwe katika mstari, 'law and orders!!'
    Jamani nchi yetu imebalikiwa kila kona, tunavyo vyanzo vya kumpatia kila mtanzania maisha bora, iwapo viongozi wetu na pia sisi wenyewe tutafanya kazi au kuendesha shughuli inavyotakikana!
    Tunayo bahari, bandari, mbuga za wanyama, maziwa makubwa, migodi ya madini, nishati za gesi, madini ya vyuma,n.k. Kweli mapato kutoka katika hizo sources yanaenda wapi?
    Mimi nadhani tuache ubinafsi na badala yake tuwe na roho ya manufaa kwa wote. Tuendeshe nchi na pia kutoa huduma kwa kulifikiria na taifa la kesho badala ya matumizi ya palepale au ya muda mfupi, hii ni pamoja na pale watu wanaposainisha mikataba ya aina yoyote ile! Tufanye kwanza research kabla ya kufikia hatua ya kuhamua jambo! Nchi yetu inao uwezo wa kujiendesha bila ya kutegemea mikopo! Viongozi wanaosaini mikataba feki wapelekwe mahakamani. Sheria za kizamani zifutwe. Wanaotetea masilai ya jamii walindwe na serikali! Viongozi wetu waache ubinafsi na kuendesha au kuitawala serikali kwa njia na imani za uchawi!... ntaendelea baadae kidogo

    ReplyDelete
  12. mimi nadhani watanzania wenzangu inabidi tubadilike sana!!!! napenda kuchangia mawazo kuhusu mdau alietuma mapendekezo yake kwamba:

    (1) suala la kutoza ada kubwa kwa watu wanaotaka kuingia katikati ya jiji na magari yao ni zuri. Lakini watu wanye pesa zao watatoa tu!! Je? vipi kwa mwananchi wa hali ya kawaida atamudu? jibu nu HAPANA. Natoa ushauri kwa manispaa kwamba wakati sasa umefika wa kupanua barabara si kwa kuongeza ukubwa wa barabara!! bali wa kuongeza 'root' nyingi! mradi huu unahitaji mtaji kwani barabara inabidi zihandisiwe juu na chini kiasi kwamba zirahisishe usafirishaji. Pia serikali ingeanzisha mradi wa city train (metro) za juu na chini ya ardhi kuzunguka jiji/miji mikubwa kama Dar, Arusha, Mwanza n.k

    (2) Tukumbuke kwamba ongezeko la magari nchini/mijini linachangia kwa kiasi kikubwa sana katika ongezeko la hewa chafu kama carbondioxide (CO2), methene (CH4) etc. Gesi hizi zinachangia sana katika ongezeko la joto duniani ambalo linachangia katika kuharibu mabadiriko ya hali ya hewa kama mvua nyingi (mafuriko), joto kali na hata matatizo makubwa kama tsunami ya mwaka 2007. hivyo serikali haina budi kuwatoza watumiaji wa magari 'kodi' ambayo ni ya 'uchafuzi wa mazingira' i.e carbon tax.

    (3) Serikali ingehimiza utumiwaji wa benzene (C6H6), CNG (compressed natural gas) na LPG(liquefied petroleum gas)kuwa/kama chanzo cha nishati kwa watumiaji magari. Tunajua magari mengi yanatengenezwa ili yatumie gasoline (petroli) au diesel; hivyo serikali ifanye mpango wa kununua teknologia kutoka katika nchi zilizo endelea kuhusu uundwaji wa vifaa ambavyo vitafungwa kwenye magari yatumiyao petroli au diesel ili yatumie nishati mbadala kama CNG, LPG, Benzene kwani hazina mkusanyiko mkubwa wa hewa chafu!

    (4) Ifahamike kwamba gharama za mwanzo za vifaa hivyo ni ghali kwa mwananchi wa kawaida!! hivyo serikali haina budi ku 'subsidy' vifaa hivyo ili vipatikane kwa mwananchi wa kawaida. Hii inaweza ikatumiwa kama sera mbadala ili kulinda mazingira yetu. Angalia nchi ambazo zimeendelea; serikali zao zimeweza kufanikisha suala hili kwa zaidi ya asilimia 75.

    (5) serikali haina budi kuwaelimisha wananchi wapendao kununua magari kwamba wanunue magari ambayo ni energy efficient. Hii itasaidia kupunguza idadi ya nishati ambayo hutumika kuendeshea magari hayo katika muda fulani. kwa mfano gari ambalo linatumia lita 1 kusafiri kilomita 20-22 ni bora kuliko gari ambalo linatumia lita 1 kusafiri kilomita 17. hii itapunguza sana hewa chafu kutoka katika magari.

    (6) serikali haina budi kuanzisha mradi wa mabasi ya jiji ambayo yatasafirisha wananchi kwa gharama nafuu hivyo kuwafanya watu wengi kutumia mabasi ya jumuiya na kupunguza idadi ya magari mijini ambayo itapunguza kwa kiasi kikubwa katika kupunguza ongezeko la hewa chafu jijini na nchini kwa ujumla.

    ReplyDelete
  13. inauma sana watanzania wenzungu,siku moja nilikua kwenye harakati za kukata Air ticket yakurudi nyumbani kwa mapumziko nikutana na vipeperushi na journal za moja ya tour company vinaonyesha mlima kilimanjaro upo kenya , yaliyoandikwa humu yalikuwa yanavutia sana watalii kwenda kenya nakupanda mlimani, roho iliniuma sana. sasa watanzania wenzangu kiongozi kama joseph mungai anaweza kweli kusimamia na kutetea masilahi ya taifa according to his vision , jamani machafuko zibwabwe yalisababishwa nanini? jamani hata ili mungai alijuhi, kenya na uganda walikuwa wanavutania nini juu kile kisiwa?

    ReplyDelete
  14. Hayo ndiyo mawazo yaliyoenda shule.
    Yaani Mungu katupa kila kitu.Kuna siku Mgeni mmoja kutoka nchi za magharibi alisema kama kungekuwa na sheria ya kubadilishana nchi basi Wangeomba kubadilishana na Tanzania.
    Yaani wa Ulaya waje kuishi Tanzania na walio Tanzania waje kuishi Ulaya.
    Watuachie mali zote walizo nazo na sisi tuwaachie walichonacho.
    Nchi yetu inakila kitu cha kujivunia,huu ni wakati wa kusaidiana kujenga nchi haswa swala la kilimo.
    Hongera bwana Kiongoli kwa kuweka hilo bayana.
    Mungu akubariki.

    ReplyDelete
  15. Dah! YAANI WEWE NDUGU YANGU UPO PAMOJA NA MIMI KABISA, SABABU HAYO ULIYOYAELEZEA NDIYO NAYOTAFAKARI KARIBU KILA SIKU IITWAYO LEO. UNAJUA WATANZANIA TUNATIA AIBU SANA! NINGEPENDA TU KUSHAURI LIANZISHWE SOMO LA USTAHABU KWA VIONGOZI NA WANANCHI WOTE NA TUPATE WATAALAMU LABDA TOKA NORTH KOREA AU SOUTH KOREA NA PENGINE CHINA MANAKE HAWA WATU NI KIBOKO KWENYE MAMBO YA NIDHAMU NA KUJITEGEMEA, WATUPE DICIPLINE WEEE MPAKA KIELEWEKE. TANZANIA TUMEJALIWA MENGI JAMANI LAKINI NASHINDWA KUELEWA HAWA VIONGOZI WANAFANYA KAZI IPI?

    ReplyDelete
  16. Amina (lisbon)August 01, 2009

    kinachonifurahisha ni kuwa sasa naona vijana mmekubaliana na mchango na mwanzo wa mawazo ambayo yamekuwa yakitolewa na waasisi wa kuijenga upya tanzania. Haya yote ni matunda ya akina mashaka na dr shayo ambao siku zote wamekuwa chachu ya kizazi kipya. lazima vijana tuwe ngangari. nchi ni yetu. hongera kwa mchango huu.

    ReplyDelete
  17. wadau kweli haya mambo ni muhimu yafanyiwe kazi.naona mbinu mbalimbali mmezitaja na dhani ni wakati wa kuact.kina Mashaka,Shayo,Us blogger,mdau john uk,mukuru,michuzi,nawewe pia woooooote mnalalamika ingawa mnapambana pia.Sasa inakuwa kuandika Tuuu?au kuna njia yoyote au action yoyote itatokea?niandikieni kuhusu mnataka iweje.Lawaaamaaaaaaaaaaa,siasaaaaaa,watu nchi zao wametumia miaka 200 kuwa civilaizdi,TZ?na kila kitu tunacho
    Nimechokaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  18. Nakubaliana na wewe mdau Kiongoli. Hayo uliyosema yote kweli. Kila mtu anafahamu hayo. Mimi,yule, hawa, wale, na wewe unayesoma comment hii wote tunajua hayo. Tatizo hatutaki kuyafanyia kazi haya matatizo. Tuna kaugonjwa flani tulichorithishwa na system zilizopita. Unaweza kusema tutaanzia wapi kudeal na haya mambo--Ni ngumu sana kwani hapa ni system nzima ya nchi ndio inahusika. Mi nikibadilika leo hii, wenzangu wataniangusha. Sasa nani abadilike? Viongozi? Viongozi ni miongoni mwetu, kiongozi 1 anamlaumu mwingine, au analaumu system ambayo yeye ni mmoja wapo. Ni ngumu sana. Ila ninachojua, japo maswala haya ni mazito, ila Rais, kwa initiatives zake mwenyewe anaweza kusolve idadi kubwa ya matatizo haya. Tumeona maraisi wanye influence na mistakabali ya nchi zao, tusisingizie eti rais anaangangushwa na watendaji wake. Kama wanachemsha waondolewe wawekwe wale wenye uchungu kama mdau Kilongoli.

    Kitogo

    ReplyDelete
  19. KUHUSU TATIZO LA USAFIRI WA DAR KWA SASA HALI YA UCHUMI HAIRUHUSU KUJENGA SUBWAYS AND RAMPS KATIKA BARABARA ZATU ZA KAWAIDA.
    KINACHOTAKIWA KADIRI YA MANG'AMUZI YANGU NI KUWA
    MFUMO WA BARABARA DAR NI ULE ULE TANGU WAKATI WA UKOLONI. HAZIJAONGEZWA BARABARA MPYA
    BARABARA ZINAZOJULIKANA NI MOROGORO, BAGAMOY0 (alhasan Mwinyi), PUGU ROAD (Nyerere Road), Kilwa na Mandela na kuongezea kidogo ya kawawa.
    Ili kupunguza msongamano wa magari ni muhimu kwanza kuongeza barabara nyingine za kawaida katikati ya jiji ili kuwapa madereva alternative badala ya wote kujazana kwenye barabara moja tu.

    Na hakika ongezeko la barabara litapunguza msongamno wa traffic na gharama za kuongeza mfumo wa barabara za kawaida ni gharama nafuu kuliko kufikiria subways nd tunnels wakati daraja la kigamboni tu linatuchanganya akili
    Candid Scope

    ReplyDelete
  20. ALBINO NO. 1August 01, 2009

    ETI RUDINI NYUMBANI MKAIJENGE NCHI SASA HAYA MABOMU MENGINE TUPIGWE NA SERIKALI MBAGALA MENGINE TUPIGWE NA RAIA WANAOTAKA PESA KILAHISI MAANA WAMECHOKA KUTAPELIWA NA SERIKALI YAO AMA HAWAWEZI KUTOA RUSHWA ILI WAFAIDI KAMA VIONGOZI WALIOMADARAKANI. TATIZO MAFISADI NI MACHACHE LAKINI YAMEWAMEZA WENGI MASKINI MATOKEYO YAKE NI KUPIGWA MABOMU NA SASA KUNA MAJITU YANAUZA MIILI YA BINADAMU ALBINO NAYO YANAWASAKA ALBINO KAMA ALMASI. SASA WEWE MDAU UNAYEDAI TURUDI BONGO RUDI MWENYEWE HUJASHIKWA SHATI, KWANI ULIPOKUJA ULITANGAZA UNAKUJA KIWANJA? RUDI MWENYEWE KIMYA KIMYA KAMA ULIVYOKUJA HUKU.KAPIGWE BOMU USIKIE HABARI YAKE. MAJITU MENGINE BWANA KARAHA TU...SIJUI NDIYO KUCHANGANYIKIWA? UK TUTAENDELEA KUDUNDA MDUNDIKO MDUNDIKO HATA KAMA KUNA SHIDA HATUTAKI UFISADI WALA KUPIGWA MABOMU.

    ReplyDelete
  21. Safi mtoa hii hoja hakika una uchungu na nchi yako,mimi ntatoa hoja ya foleni nchi nyingi za ulaya zinazoendelea wanajaribu ktuzoa kiasi cha PESA KWA GARI ZOTE AMBAZO SI ZA ABILIA.na barabara zao nyingi zinazoelekea mjini ziko kubwa za kwa magari yanayokwenda na nyengine upande wa mtaa mwengine ni za kutoka tuu ikiwa watalijaribu hili nafikili kiasi tunaweza kupunguza asilimia fulani au yote

    ReplyDelete
  22. SASA U R SO FUNNY. UNA POINT NYINGI NA NZURI SANA ILA NIMESHANGAZWA NA MTINDO WA KUCHANA MISTARI ULIOAMUA KUUTUMIA. YAANI UMEANZA KU-FLOW KWA KISWAHILI SAFI KABISA NA MA-POINT MAZURI KIKWELIKWELI, NIMESOMAA WEE KUFIKA KATIKATI NASHTUKA MTAALAM UME-SWITCH KWENYE ENGLISH NA KUENDELEZA LIBENEKE LA MA-POINTS UKACHANA MISTARI KWA ENGLISH WEE MARA UKAJIMUVUZISHA TENA KWENYE KISWAHILI FASAHA UKACHANA MISTARI MIWILI MITATU MWANAWANE UKAJIMUVUZISHA TENA KWENYE LI-KIINGEREZA!! DUH. NIMEPENDA MAMBO 2. KWANZA KABISA MA-POINTS ULIYOYAMWAGA NA PILI HIYOOO STAILI YA KU-SWITCH BETWEEN LANGUAGES KATIKA KUCHANA MISTARI, ha ha ha.
    nitafurahi siku nyingine nikikutana na article yako itakayokuwa katika staili hii.

    ReplyDelete
  23. Mdau Australia,
    Nimekupata vizuri, vitu unavyoongea ni stori za kila siku. Mimi nikiwa mtoto mdogo nasoma the same stories kutoka magezeti ya Bongo, kina Ulimwengu wameandika saana kuhusu kila kitu unachosema. Na hata humuhumu kwa brother Michuzi people have cried out, the Mashakas, Mukurus, Shayos, na wadau kibao.
    Kila unacho-recommend kipo, ila bahati mbaya the majority of Tanzanian's mind is rotten, completely.
    Nasema, na narudia tena nasupport yule aliyesema tunahitaji Dictator. Yeah, kuna watu hawatapenda, ila we have to.
    Kwanini? kwasababu the network of fisadis is so wide and you can't untangle it with words only, except with iron fist.
    those are my two cents, I applaud you for speaking out

    Nawakilisha,
    Makwanga

    ReplyDelete
  24. YANI NCHI YETU ITAKUJA KUPATA MAENDELEO WANANCHI NA VIONGOZI WAKE WAKIACHA UNAFKI,WIZI,UKABILA NA UDINI ULIOZUKA HIVI KARIBUNI BUNGENI.
    WABUNGE WAMEANZA KUTUPELEKA PABAYA KUHUBILI UDINI BUNGENI.
    PIA MTU KAMA MUNGAI WALA MSISHANGAZWE NAE HUYU JAMAA SIO MTANZANIA HALISI BABA YAKE ALIKUA MHAMIAJI KUTOKA KENYA NA NDIO MAANA HANA UCHUNGU NA WATANZANIA KUTOKANA IDADI KUBWA YA FAMILIA YAKE KUTOKA KENYA WATAFAIDIKA.
    HAYA NI MABABILONI WACHACHE ALIOFAIDIKA NA UKOLONI UKIMWAMWAMBIA UKOLONI URUDI ATASHANGILIA.
    TUKITAKA TUENDELEE INABIDI TUACHE UNAFKI WA KUSAPOTI UKABILI NA INTEREST BINAFSI

    ReplyDelete
  25. mnataka nini tanzania,ukimwi mnao,ujambazi upo
    udini uko njiani,ukabila kila leo.
    tanzania izidi lulaaniwa,ndio maoni yangu,sirudi ngó!

    Mheshimiwa naomba uipost oni langu hili,sababu najua wewe ni fair kwa maoni yote.
    asante.

    ReplyDelete
  26. Kiongoli brother, your concern is very valid. I second you in all the matters you listed and all these questions am sure will be well discussed in the coming Diaspora meeting organised by TPN in December. Let us all diarise it now, kufika tutafika tu kwani muamko si huu tunao jama. Nyumbani ni Nyumbani, wapi kama Bongo jama!

    -- Proud Tanzanian!!

    ReplyDelete
  27. "I know there are few people that will criticize my opinion but that is our biggest problem that we have as people!!"

    NIMESOMA VIZURI TOKA MWANZO LAKINI NILIPOFIKA HAPO KWENYE MANENO NILIYOYANUKUU HAPO JUU, NIKAISHIWA NGUVU KWA MAANA KIONGOLI ANATAKA TUENDE MBELE LAKINI HUKU AMEWEKA HAND BREAK. MTOA MADA ANA IMANI ZA 'UMIMI' KWAMBA ANACHOKIONGEA NI SAHIHI NA ASINGEPENDA KUKOSOLEWA NA ZAIDI YA HAPO ANAONA KUKOSOLEWA NDIYO TATIZO WALILONALO WATU WA NCHI HII.
    KIONGOLI THINK TWICE AND IF POSSIBLE RE-PHRASE YOUR STATEMENT. WATOA MAONI NI SAWA NA WALE WALIOKUWA WAKIKUFANYIA PEER EDITING ULIPOKUWA DARASANI.

    ReplyDelete
  28. Sasa watanzania tunaanza kuamka!!!well done.Ideas first,implementation follows.nachotaka kujua mikutano ya tpn inajumuisha the targeted individuals kama politicians,intellectuals i.e. economists/drs/professors/general managers,bussiness men/women, farmers etc wahusika amba ndio wataleta mabadiliko??au ???tusisahau constitutions/policy making should be reviewed and improved to avoid all misunderstandings.Wenzetu wa first world,bunge linakutana kila siku kwa mwaka mzima,sheria zinabadilishwa kutokana na time/changes towards public needs. lini tutafika huko???i wish siku moja waliomadarakani watasikiliza new ideas toka wasomi wetu wa pembe zote duniani,ili tutunge policies za kutuletea maendeleo sio kuwa na negative attitude kwamba watoka mbali watatueleza nini wakati sisi ndio tupo hapa??!!!please kama wote tunaitakia mema nchi yetu,tunaomba mliomadarakani mtoe chngamoto kwa wasomi wenu popote walipo kuwa mko tayari kusikiliza new ideas ziendazo na wakati karne ya 21.

    ReplyDelete
  29. it is just the matter of us putting things together.
    1. Hivi hatuwezi toa maoni kwa rais. Kwa mfano tu reli ya kati ama TAZARA. Rais ama ofisi ya mipango wangefunga ile station mjini halafu reli kuanzia ubungo ingekuwa nachukua abiria kwenda makazini. Trains ziboreshwe,so TAZARA should be there to replace the reli ya kati if possible.
    2. Parking fees ipandishwe ili kufanya wananchi wawe wanapanda mabasi. Tukitegemea mabasi yanayoenda kasi yatafanya vizuri kama inavyotarajiwa.
    3. Hiace al maharuf km vipanya ziwe zinaishia Ubungo tu, kwenda mjini tupande City Buses, huko kwingine Hiace.
    4. Utunzaji mazingira uboreshwe bado sana hatujaelimika, sehemu zinazofaa kupandwa maua, manispaa zihakikishe yanapata maji ili kukua. Dar joto litatuua tusipo angalia. Km mkikumbuka siku ya mazingira duni, chanzo kutoka BBC Sahili hali ya hewa na mchafuko wa mzingira ni mbaya sana ulimwenguni, Tanzania ikiwa moja wapo hasa kwa kupanda kwa joto ambalo ninzuri sana na mazalio ya mbu. Which means malaria itakuwa hatari sana.

    Naishia hapo kwa leo.....ni maoni kwa nionavyo mimi si lazima hiwe hivyo, tufunguke mawazo tujenge Tanzania Mungu Ibariki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...