Miss Kinondoni 2009 Lulu Ibrahim (kati) akipunga mkono baada ya kuvishwa taji usiku wa kuamkia leo ukumbi wa Mlimani City jijini Dar. shoto ni mshindi wa pili Yvonne Bigilo na kulia ni mshindi wa tatu Aloyce Innocent
Mgeni rasmi wa Redds Miss Kinondoni 2009,Waziri wa mambo ya ndani Mh Lawrence Masha akiwa amepozi na tatu bora katika onesho hilo lililoandaliwa na kampuni ya Boy George Promotions chini ya Mkurugenzi wake Bw.Yusuph George.

Tano bora ya Redds Miss Kinondoni 2009
Miss Kinobdoni aliyemaliza muda wake ambaye pia alikuwa Miss TZ 2008, Richa Adhia akila pozi kabla ya kukabidhi taji kwa Lulu






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hongera sana Lulu unastahili taji. Pia huyo wa nguo ya Red angetakiwa kuwa wa pili mzuri kweli Lakini vyovyote kila mtu anaupeo wake wa macho.

    ReplyDelete
  2. ..Mitihani ya Taifa toka Baraza la Mitihani Tanzania huchomolewa na kupewa watahiniwa kwa pesa hongo kidogo tu ili wafauru.

    Je, haya mambo ya Ma-miss yako "Fair" ki kweli kweli kumtoa mshindi?????

    ReplyDelete
  3. duh naona Masha anameamua kujibinafsisha kwa huyo mshindi na kuamua kumpa mgongo huyo mwingine. angali picha vzr utagundua hilo

    ReplyDelete
  4. Mh. jamani mi sijaelewa hapa? kwani Nasreen si ndio Miss TZ 2008/2009? na huyu alikua 2007/2008? ss kama kweli Miss kinondoni 2008/2009 yuko wapi?

    Hebu nambieni.

    ReplyDelete
  5. haya ndiyo huwa wachangiaji tuna yazungumzia,viongozi wakubwa wa serikali ktk nchi zilizo endelea sio rahisi kumkuta katika mashindano ya level hii. lakini nchini kwetu haya ni mambo ya kwaida yaani minuso inayoambatana na mambo yasiyo ya kipaumbele ktk jamii,na wakienda bungeni wanakwenda kujadili mambo ya ajabu ajabu,eti kuvaa wigi n.k wakati kuna mambo ya msingi ambayo mwananchi anapaswa kusaidiwa kwayo. nina mengi ya kuongea lakini hapa sio mahali pake. anyway kama alikuwepo weekend kwa raha zake binabsi sina tatizo nae. lakini kama kweli ni sehemu ya kufanya kazi kiofisi, nasikitika.

    ReplyDelete
  6. JAMANI RICHA SI ALIACHIA TAJI LAKE LAST YEAR NA ALIKUWA MISS 2007/2008.MICHUZI VIPI TENA?

    ReplyDelete
  7. Masha Acha Kuuza Sura Cheo Chako Kikubwa Sana Hakina Hadhi Ya Kua Mgeni Rasmi Wa Hii Kitu . AIBU MOJA AI AIBU

    ReplyDelete
  8. Huyu ndio masha lawrence kwa ninyi musiomujua!

    ReplyDelete
  9. NCHI HII BWANA INA MAMBO,SIJUI KWA NINI NILIZALIWA TANZANIA
    WAKATI MAJAMBAZI WANAVAMIA BENKI TENA WAKIWA NA MABOMU MCHANA KWEUPE,WAZIRI ANAEHUSIKA NA WIZARA HIYO BWANA MASHA ANAACHA KUINGIA DORIA KAMA ALIVYOKUWA ANAFANYA LYATONGA,ANAENDA KUWA MGENI WA HESHIMA MASHINDANO YA UREMBO,TUTAFIKA KWELI!!!!!!!!!
    TANZANIA TANZANIA,NAKUPENDA ILA BASI TU,VIONGOZI NDO WANAFANYA NIKUCHUKIE
    NI HAYO TU

    ReplyDelete
  10. Watu mna matatizo sana, hivi mtu ukiwa kiongozi wa nchi kutakiwi kushiriki katika shughuli za kijamii. Yani wengine mnaona kosa kwa Waziri kuhudhuria dhifa hiyo, ambayo ni ya masaa machache sana. Sio rahisi kwa binadamu yoyote kila muda awe anafanya kazi tu. Acheni chuki binafsi na mtakufa nacho kijiba cha roho.....hahahhaha ovyo

    ReplyDelete
  11. Wee anony unayejuta kuzaliwa Tanzania, sheria inakuruhusu kuukana uraia wa nchi yako na kuchukua uraia wa nchi unayotaka.....and I wish yu ol the best

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...