Kaka nanihii huwezi amini. Hiki chuma kimepigana vita miaka ya 1939/1945 kikiwa na KAR. Kinaitwa Mzee H.Ndasikio Nkya. Bado kiko fiti kinoma, enzi zake kimekata na kufunua sana maadui. Pembeni ni kitukuu wake Papa Nkya. Naomba umrushe hewani watu wajionee.Mzee anapikana na maeneo ya Machame.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hongera babu Nkya tafadhalini wajukuu/vitukuu mpelekeni babu yetu huyu (Mjeshi wa zamani - KAR) kwa mkuu wa wilaya au kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro aweze kuwekewa kumbukumbu zake sahihi ni tangazo ambalo limetolewa kwenye maadhimisho ya miaka 45 ya JWTZ kuwa wazee wote waliopigana vita vya pili vya dunia 'AMBAO WAKO HAI' majina yao yote yanapatikana katika ofisi zote za wakuu wa wilaya au ofisi za wakuu wa mikoa Tanzania kwa maelekezo zaidi -Tafadhalini sana huenda kuna BINGOOOOOOOO!!!!!!!!!!!!

    Mdau Muddy

    ReplyDelete
  2. kufwenda mbee hongera nnuu
    mdau cadana

    ReplyDelete
  3. Mungu azidi kumuwekana namtakia afya njema

    ReplyDelete
  4. Neekya babu!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Wewe mangi unashangaa tu kwenye pisha. Mpeleke msee kwa mkuu wa wulaya anawekwe kwenye kumbuku za taifa. Kuna hela inapatikana ati kule. Changamka ati mangi

    Halafu hakikisha msee anaendelea kupata kamtori na kanyama mara kwa mara.

    ReplyDelete
  6. mpeleke mzee kwa mkuu wa wilaya aandikishwe ili alipwe haki zake.vilevile nilikutana na wazee wengi maeneo ya Machame,Hai,Uswaa wenye issues za pension miaka ya nyuma nao wapatie taarifa tafadhali.

    ReplyDelete
  7. tunatarajia kusikia hawa wazee wamehojiwa na vyombo vya habari ili tupate hisia zao juu ya historia ya vita na pia tunatarajia kuona kwamba serikali inawaanzishia foundation ambayo itasaidia kutunza historia na kumbukumbu zao katika maktaba na makumbusho ya taifa..hima jamani kabla hawajatangulia mbele za haki tukabaki kutunga hadithi njooooo utamu koleaaaaa mara mimi sikushauriwa hivyo mara ooooh jamani mimi sikuwemo nyakati hizo.....tufanye sasa hivi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...