BENDI ya muziki wa dansi ya K-Mondo imenyakua mwimbaji nyota nchini Mhina Panduka (akiwajibika pichani) maarufu kama Toto Tundu.

Mhina ambaye alianza kutamba na bendi ya Mwenge Jazz ‘Paselepa’ wakati alipoimba kibao Pole Mama James tayari amekwishaanza kazi na kundi hilo.

Kiongozi wa K-Mondo, Richard Mangustino ‘Teacher’ alisema mjini Dar es Salaam kwamba wamemchukua mwanamuziki huyo katika kuimarisha safu yao ya uimbaji.
“Tayari Mhina ameshaingiza sauti katika nyimbo mbili mpya ambazo kwa mara ya kwanza zimesikika Rainbow Jumapili na zinatarajiwa kuwemo kwenye albamu yetu ambayo bado tunairekodii,” alisema.

Kuingia kwa Mhina ambaye mara ya mwisho alikuwa katika bendi ya mkongwe Abdul Salvador, kunafanya K-Mondo kuwa na waimbaji watano kwa sasa wakiwepo kina dada wawili Vumilia Mwaipopo na Kire Kire.

Tayari K-Mondo imeachia nyimbo mbili redioni ambazo ni Magambo na Tatizo Umasikini.

Mhina amewahi kuziimbia bendi ya Washirika Tanzania Stars ‘Watunjatanjata’, Orchestra Safari Sound ‘Ndekule’, Mviko Sound, TOT Plus na DDC Mlimani Park Orchestra ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. hi teacher, carry on with your good music. god bless you.

    ReplyDelete
  2. hi teaher, carry on with your good music. god bless you.

    ReplyDelete
  3. Hi teacher, carry on with the good music, god bless you.

    ReplyDelete
  4. Ukiondoa marehemu waliotangulia mbele ya haki, huyu toto tundu ama double t kwa kweli ana sauti tamu kama ya Bitchuka na hana mpinzani. Double T fanya vitu vyako kijana.

    ReplyDelete
  5. mangustino tunaimani heshima yako itarudi,wataumwa na dawa hakuna.(washa moto)yooh lekiba'ngo

    ReplyDelete
  6. dada hapo unamependeza kweli,endeleeni kujitahidi jamani.

    ReplyDelete
  7. dada wakyela umekucha kweli wakomeshe wanga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...