---------------------------------
Asalaam aleikum Mdau mkuu wa libeneke,
kama kijana wa zamani kikosi cha taifa kubwa enzi za Mwalimu kilikuwa kama ifuatavyoGolini alikuwa ni Athumani Mambosasa (2) Shaaban Baraza (3) Mohamed Kajole (4)Athur Mwambeta (5) Omari Chogo (6) Khalid Abeid (7) Willy Mwaijibe (8) Haidar Abeid (9) Adam Sabu (10) Abdallah Kibadeni (11) Abbas DilungaKikosi hichi ndicho kilichowafunga watani wao wa jadi 1973 baada ya Yanga kuwa mabingwa kwa miaka mitano mfululizo 1968- 1972 na ni kikosi hicho ndicho kilichochukua ubingwa wa Africa mashariki kwa mara ya kwanza 1974.
Wanaonekana katika picha hiyo kutoka kushoto ni Haidari Abeid,Shabani Baraza,Abdallah Kibadeni,Willy mwaijibe , Abbas Dilunga,Mohamed Kajole ,Mwambeta ,Omari Chogo ,Makipa ni Hassan Mlapakolo na Mambosasa.
Mdau Profesa
Tumetoka mbali sana duh...
ReplyDeletekweli mbali ilikuwa enzi za MWALIMU SIO RUKSA.SIKU HIZO MPIRA KWELI SIO SASA PESA
ReplyDeleteAsante Mzee Nanihii,hizo ndio enzi zangu!.Hapo namuona(bila kufuata mstari)Haidari Abeid,Shaban Baraza,Abdallah Kibadeni,Abas Dilunga"sungura",Mohamed Kajole na Omari Chogo"Mluhya".
ReplyDeleteFirst left Haidar Abeid, third Abdallah Kibaden and the lad holding the ball Athumani Mambosasa. That is as far as I can go...
ReplyDeleteHuyo wa kwanza ni Mohamed ali kwi kwikwikwi..........
ReplyDeletehivi mbona wachezaji wa zamani walikuwa na miili mikubwa inayoweza kushindana kwenye mpira? leo hii hawa tulionao mbona vidogodogo sana? duh!
ReplyDeleteWa kwanza ni Haidar Abeid,Maulid Dilunga,King Kibaden,Aliye inama simjui anayefuata ni Abbas Dilunga,Mohamed Kojole,anaye piga danadana simjui anayefuatia ni Omary Chogo na hao makipa kwa kweli nimewasahau lakini nakumbuka kipindi hicho Athuman Mambosasa alikuwepo alikuwa kipa mkali sana pamoja na Hassan Mlapakolo.Mambosasa alikuwa na tabia ya kuwaibia wenzake nguo wanapokuwa kambini akimuona mwenzake kavaa shati zuri anamwambia ninalo shati kama hilo basi kama siku huyo mwenzake hajalivaa lazima ataliiba.
ReplyDeleteHapo Michuzi umecheza.Hapo nawakumbuka wachache. Kutoka kushoto Haidary Abeid (Muchacho), Shaban Baraza, Kibaden, Omary Gumbo, Abbas Dilunga, Mohamed Kajole, anaefuata simkumbuki, Omary Chogo, Adam Sabu, wengine siwakumbuki. Nakumbuka hili chama lilikuwa la mwaka 1973/74, lilikuwa moto si mchezo.Ee bwana Michuzi hizi picha ni bomba sana inafaa uziweke mara kwa mara, zinatukumbusha mbali.
ReplyDeleteWa tatu toka kushoto ni Abdallah Kibaden. Enzi hizo (miaka ya 70) alikuwa (kwetu Bongo) kama akina Kaka, Cristiano Ronaldo na Samuel Eto'o, leo...
ReplyDeletekutoka kushoto bila utaratibu: Muchacho, Sabu, King,Machela, Mwitu, Bruce Lee, Chuma, Kapera, Jujuman,Badi, Mambosasa.
ReplyDeleteWa tatu kutoka kushoto namkumbuka ni Abdallah Kibadeni, ambaye alisukuma gozi timu ya simba na kisha kuitwa Kibaden Mputa ipokuwa hazina katika timu ya majimaji
ReplyDeleteKAMA HAMJUI WATU ACHENI,TANGU LINI MAULIDI DILUNGA ALIWAHI KUCHEZEA SIMBA?
ReplyDeletekeff hapo umeongea bora ss wengine tupo kimya hatutii neno
ReplyDeletekuna mauridi dilunga na abbasi dilunga??? mbona siwaelewi. kule juu mshkaji kaandika abbasi dilunga, wewe keff unasema maulidi dilunga. pengine mmoja wenu kachemsha, au walikuwepo wachezaji wawili tofauti wenye sir name moja dilunga, in which case bwana keff ndo utakuwa umechemka au mtoa jibu kachemsha. hebu tufafanulieni mana mi wakati huo ilikuwa hata bado baba hajampandilia mama kwa zamu yangu, ilikuwa bado zamu ya kaka zangu
ReplyDeleteKWELI WENZETU WASICHANA WA ENZI HIZO MLIFAIDI KWELIKWELI!! HEBU ANGALIA MIDUME ILIVYO NA MISURI NA NGUVU ASILIA. HIKI KIPANDE CHA MTU KWA MFANO HUYO WA KWANZA MNAYEMUITA SIJUI HAIDAR HEBU MUANGALIENI ALIVYOTULIA KAMA MWANAUME, HUYO AKIKUPA KITU NA BOX NI MASAA SITA HAJASHUKA KIFUANI ANAVYOONYESHA. LAKINI HAWA TULIONAO SIKU HIZI MHH KESHAJILIA VIJICHIPSI VYAKE HUKO AU KFC ONE MINUTE MAN ANAKOROMA
ReplyDeleteMaulidi dilunga alikuwa Yanga Abassi (Sungura) alikuwa Simba, winga anakimbia na mpira spidi nusu centimita pembeni ya chaki toka kati ya uwanja.
ReplyDeleteSamahani wadau mimi ndiyo niliye andika kimekosa kuhusu Maulidi Dilunga kweli Maulidi Dilunga alikuwa mchezaji wa Yanga,samahani sana unajuwa tena mambo ya kusahau kwani ni miaka mingi imepita.
ReplyDeleteJe unajua kama Haidari Abedi na Saleh Jabir mfalme wa bongo flava mama zao ndugu?
ReplyDeleteHivi George Best Kulagwa , Danny Mwalusamba, na Wengine Waliingia Baada ya 1975 Sio? Na Kina Jumanne Hassan Masimenti ?
ReplyDeleteKumbukumbu Zinapotea UTU Uzima ...