Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mh. George Mkuchika akiongea na wanahabari wakati wa kusaini mkataba wa ushirikiano katika sekta ya Habari, Utamaduni na Michezo kati ya Tanzania na China leo jijini Dar. Kushoto ni Balozi wa China nchini Tanzania Mh. Liu Xinsheng.
Picha na habari na Aron msigwa wa MAELEZO.
CHINA KUONGEZA NAFASI
ZA MASOMO KWA WATANZANIA.
Tanzania na China zimekubaliana kuendeleza ushirikiano katika Sekta ya Habari, Utamaduni na Michezo.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati wa kusaini mkataba mpya wa ushirikiano wa miaka mitatu baina ya Tanzania na China Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo George Mkuchika amesema kusainiwa mkataba huo ni ishara ya uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi hizi.
Amesema kwa kipindi kirefu Tanzania imekuwa ikishirikiana na China katika Nyanja mbalimbali zikiwemo elimu, Utamaduni,sekta ya habari, Afya pamoja na mambo mengine ishara inayoonyesha uhusiano mzuri kati ya Tanzania na China.
Waziri Mkuchika amesema kwa kipindi kirefu toka mwaka 1964 Tanzania imekuwa ikipokea wataalam katika fani mbalimbali za ujenzi, wataalam wa afya,walimu katika fani mbalimbali na viwanda ambao wamekuwa msaada mkubwa sana katika kubadilishana uzoefu na wataalam wa ndani hapa nchni.
Ameongeza kuwa watanzania wengi wamekuwa wakienda nchini china kujifunza mambo mbalimbali ya kiutamaduni,kushiriki michezo mbalimbali, kupata nafasi za masomo katika fani mbalimbali na hivyo kukuza na kuleta maendeleo nchini.
Naye balozi wa China nchini Tanzania Liu Xinsheng akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo wa ushirikiano na Tanzania amesema kuwa ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na China utaendelea kudumishwa akitoa mfano wa nchi yake kuongeza maradufu nafasi za masomo kwa vijana kutoka Tanzania kwenda kimasomo nchini china toka mwaka 2006.
Ameongeza kuwa kwa mwaka huu 2009 watanzania wengi walipata nafasi zaidi ya kwenda nchini humo kwenda kujifunza mambo mbalimbali katika masomo ya udaktari, Nyanja ya utamaduni, kushiriki matamasha mbalimbali ya michezo pamoja na nafasi mbalimbali za waandishi wa habari kupata fursa ya kutembelea nchi hiyo.
Aidha amesema nchi yake itaendelea kuongeza nafasi zaidi kwa watanzania kila mwaka ili wapate nafasi ya kwenda nchini China kujifunza na kupata uzoefu katika mambo mbalimbali na hivyo kuleta maendeleo nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Prof. Hermas Mwansoko amesema kusiniwa kwa mkataba huo kutatoa fursa nzuri kwa watanzania kushiriki katika mambo mbalimbali yakiwemo matamasha ya kiutamaduni, kupata ujuzi na elimu katika uandaaji wa filamu na hivyo kukuza sekta ya Utamaduni hapa nchini.
Kuhusu elimu Prof. Mwansoko ameishukuru serikali ya China kwa kuendelea kutoa nafasi takribani 100 kila mwaka kwa vijana kutoka Tanzania kupata nafasi ya kwenda kusoma katika ngazi mbalimbali kuanzia sekondali, shahada za uzamili na uzamivu katika Nyanja mbalimbali.
Akitoa maelezo kuhusu faida ilizopata Tanzania katika mkataba wa awali kati ya Tanzania na China kabla ya kusainiwa kwa mkataba mpya Prof. Mwansoko amesema Tazania imenufaika kwa kiwango kikubwa sana katika sekta bya habari, Utamaduni na Michezo akitoa mfano wa ujenzi wa Uwanja mpya wa mpira ambao uko katika kiwango cha kimataifa.
Mbali na ujenzi huo amesema Tanzania imefaidika kwa kiwango kikubwa na kupata kasi ya kimaendeleo inayoridhisha kwa kuwapata madaktari wanaotoa huduma za afya, ujenzi wa miundombinu zikiwemo barabara na pia kazi mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na makampuni kutoka nchini china kutokana na zabuni zinazotolewa kwa utaratibu unaokubalika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. mi nawashauri watanzania wenzangu kutoenda china kusoma,mojawapo...ni kwamba,
    1.baada ya masomo hakuna kazi.
    2.Mtu ukipata bahati na kuja huku magharibi,kama umesoma china hawakuajiri...China ina jina baya sana huku West.

    ReplyDelete
  2. hongera tanzania kwa kuimarisha uhusiano na china kwani kwa sasa china ndio taifa tajiri kuliko mataifa yote duniani ILA TATIZO LAO KUBWA WANATENGENEZA FEKI HAO HADI BIDHAA AMBAZO ZINAHATARISHA MAISHA YA WANADAMU MFANO NYAYA ZA UMEME KWA KWELI WACHINA NI MABINGWA WA BIDHAA FEKI DUNIANI

    ReplyDelete
  3. Hakuna elimu huku, ni kusaka mahela tuuu.
    Mie shule ishanishinda huku
    Kichina ni kigumu balaa
    Maclass ya ngeli nayo longolongo nyingi, mateacher wanabana ujuzi.
    Njooni tutafute mahela, siyo elimu
    Hizi nafasi za kuja china waachie waliofeli wadugu.

    ReplyDelete
  4. Wantazania nafasi ndo hii.. bora uende china kuliko kukaaa bila elimu! wewe mdau wa kwanza hapo wapo vijana hawana uwezo wa kwenda nchi hizo ambazp wajidai marafiki zetu lakini hata nafasi za masomo hawatoi..
    mimi niliwahi kuwa china kuhusu bidhaa feki sawa ila inategemea.. nilipokuwa guanzhou unaenda dukani unataka simu ambayo bei ya ni labda milioni moja ya tanzania.. utaanza kuimba naye bei atakuleta nyingine ipo vilevile ya laki tatu hivi .. basi hiyo ni feki na wafanya biashara huwa tunaambiwa kabisa HII YA BEI RAHISI FEKI "waafika na akili zetu maskini twasema NANI ATAJUWA KULE"
    china ndo nchi tajiri iliyobaki ambayo haina mtikisiko wa kiuchumi ikifuatiwa na japan .... china verysoon itakuwa superpower propaganda za nchi za magharibi sisi nchi zetu za kimaskini tusisikilize twendeni tukapate elimu .. tusiwe wajinga twapewa vitabu na kuvifanya Mito ya kulalia eti havina kazi tutaja juta kama tukiwa na mawazo kama ya huyoo mdau wa kwanza
    ...

    ReplyDelete
  5. Mdau unayeshauri watu wasiende kusoma China unasahau kwamba hayo mataifa ya magharibi yamekopa China kujinusuru na matatizo yao ya kiuchumi. Jina baya la China huko magharibi linatokana na tofauti za kisera tu. Kwa muda mrefu Wachina walikuwa wanaendeleza ujamaa kwa hiyo ikawa hawajawapanulia soko mabepari wa magharibi. Magharibi walipata uchungu sana ukizingatia mabilioni ya watu wanaoishi China. Nchi zetu zina jina zuri magharibi kwa sababu tumewapanulia kama wanavyotaka.
    Isitoshe unapoenda kusoma unatafuta kazi baada ya masomo au kuelimika ili uweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi? Tubadili mtazamo. Tusiende kusoma ili tupate kazi baada ya masomo.

    ReplyDelete
  6. Nasikia tumesainishwa mkataba feki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...