UTUMIAJI WA TOVUTI YA WANANCHI
Nimesoma maoni ya mdau mmoja katika Blog hii akidai kuwa Tovuti ya Wananchi haina faida kwa wananchi na kwamba inajaribu kuchukua nafasi ya waheshimiwa Wabunge ambao ndio wenye dhamana ya kuwasilisha kero na maoni ya wananchi wao Serikalini.
Ukweli ni kwamba, tofauti na Tovuti nyingine, Tovuti hii inafanya kazi kwa mtindo wa barua, SMS au Simu. Mwananchi anapotuma barua yake, SMS yake au anapopiga simu ujumbe wake hauwekwi hadharani. Hivyo hivyo na mtumiaji wa Tovuti hii.
Kinachofanyika hapa ni kwamba, Mwananchi anaandika kero yake katika sehemu husika mara baada ya kuifungua kwa kufuata hatua zilizopo.
Jifunze Zaidi:
Wasilisha Hoja:
Fuatilia Majibu:
Kata Rufaa:
Kama unawasilisha ujumbe bonyeza WASILISHA.
Ukishawasilisha ujumbe wako katika eneo hili, utapewa TIN (Namba ya hoja yako wewe mwenyewe).
Taarifa unazoandika hapa hiziwezi kusomwa na mtu mwingine zaidi ya Wahusika wa Idara ya Habari (Maafisa Habari) wenye Namba za Siri ambao kila siku hufungua Tovuti hii na kujibu maoni, kero au hoja za wananchi.
Maofisa hawa, huifungua hoja yako na kuisoma kisha huituma inakotakiwa kwenda. Kama hoja inahusu Wizara Fulani, hutumwa kwenda katika Wizara hiyo moja kwa moja ambako itafunguliwa na Afisa Habari na Mawasiliano wa Wizara husika. Baada ya hapo hujibiwa baada ya kupata majibu kutoka kwa muhsika ambaye anaweza kuwa Waziri , Katibu Mkuu, au Afisa yeyote mwenye dhamana ya wizara hiyo.
Kazi yote hii haiwekwi hadharani kama ambavyo sms yako isivyowekwa hadharani kwa mtu yeyote kuisoma. Kazi hii hufanywa kwa usiri kati ya Mtuma hoja, kero au maoni na Afisa mwenye dhamana na hoja hiyo.
Kama mtuma hoja atakuwa ametumia SMS kutuma hoja yake kwa njia ya Tovuti ya Wananchi, atapata jibu lake kwa njia ya SMS. Hii ndiyo sababu kuwa si kila mtu anaweza kufungua Tovuti ya Wananchi na kusoma hoja, kero au maoni yako la sivyo kila mtu angeweza kumjibu mtoa hoja hata kabla hoja hiyo haijamfikia mhusika.
Hapa kinacholengwa ni kuifikisha hoja ya nwananchi kwa mhusika kwa njia ambayo mtu mwingine hataweza kuingilia kati mawasiliano baina ya mtuyma hoja na mlengwa ambaye ndiye anatakiwa kutoa jibu la hoja, kero au maoni ya mwananchi.
Tovuti iliyo wazi kwa kila mtu kufungua ni Tovuti ya Taifa ambapo unaweza kufungua na kusoma yaliyomo kama ulivyofanya kwenye Blog hii. Tovuti ya Wananchi ni daraja kati ya Mwananchi na Serikali yake. Haimzuii Mbunge kuwasilisha hoja ya mwananchi wake Bungeni. Zipo hoja binfsi na kila mmoja ana haki ya kufikisha kero yake panapohusika.
KWA MAELEZO ZAIDI FIKA OFISI YA IDARA YA HABARI – MAELEZO - ILI UELIMISHWE ZAIDI JINSI HUDUMA HII INAVYOTOLEWA BADALA YA KUIPAKA MATOPE SERIKALI KWA HILI
MAELEZO
Niliuliza swali kwenye hiyo tovuti sijajibiwa mpaka leo mwaka mzima sasa kwa hiyo haina faida
ReplyDeleteKwa jinsi utendaji kazi wa serikali ulivyo, malengo ya hii tovuti hayatafikiwa. Hayo ni maoni yangu but time will tell.
ReplyDeleteMaoni: Hii tovuti iko slow sana kufunguka. Na hapa nipo UK natumia 50MB broadband speed connection..!!
Huu ni mfano wa blog ya jamii inavyofanya kazi. Muda mfupi baada ya kero kuanikwa humu ufafanuzi umetolewa kwa umma. Kasi kama hiyo inahitajika katika kushughulikia kero zinazowasilishwa kupitia tovuti ya wananchi.
ReplyDeletembona mtoa maelezo anajihami na kupiga mkwara? timiza wajibu wako!
ReplyDeleteAisee ndugu uliyetoa jibu hili tunaomba ujibu hoja na si kutueleza jinsi tovuti inavyofanya kazi kwani ujue hapa unadili na watu waelewa na wengi wao wasomi kuliko wewe. swala ni kwamba mbona hata tukituma maoni yetu hatuoni responses zozote?? Mimi nadhani suala hili mngeliacha kwenye globu zetu za jamii tuendelee kulalama hukohuko kwa maana tunajua ujumbe unawafikia. tukiwa na kero tunatumia michuzi blog au jamii forum na huwa zinakuwa na impact ya harakaharaka kama tunavyotegemea. tuliweka kero yetu ya uwanja wa ndege kupitia michuzi na kero ziliwafikia walengwa haraka sana. hizo tovuti zenu za serikali ziko biased sana na zinataka mtu mwenye kunyenyekea kitu ambacho watanzania tunajitahidi kukiacha, hamna kunyenyekeana siku hizi suala hapa ni kwamba tunafanya kila liwezekanalo kuhakikisha siku moja utawala wenu dhalimu na mbovu unakwisha!!!! ningeandika mengi hapa lakini tatizo michuzi nae akiona ngoma inakuwa nzito ana-opt kuyabana maoni so ngoja niishie hapa lakini message sent. kama kero inahusu mkoa wa rukwa ni kwanini muanze kuyasoma nyie maoni yangu? kwanini msi-design hiyo tovuti yenu in such a way kama maoni yangu yanahusu ikulu yaende moja kwa moja ikulu??? huo sasa ndo ufisadi wenyewe. kwa hiyo mkiona ishu ya kwenda ikulu na haijakaa vizuri mnaamua kuibanjua juu kwa juu na isifike ikulu si ndio???? mnajenga au mnabomoa??? hebu acheni somjo mjue watanzania wa leo si wale mliowazoea!!
ReplyDeleteahsante
Kigosi, UDOM.
Wewe uliyejibu ni walewale watu wa zamani eti kama huelewi ufike maelezo, kwani kila mtu yuko bongo? we vipi? Kwanza jamaa hakuipaka matope alichouliza ni kwamba watu walihusishwa katika kutengeneza hiyo kitu unayotaka watu waje maelezo uwaelimishe. Which means you didn't even get the f@@@n point. Acheni mambo yenu ya kizamani kutisha watu eti njoo maelezo, kwanza kuna vumbi. Michuzi usiibane jamaa apate ujumbe.
ReplyDeleteCalifonian.
Hawa jama wangefungua kama blog hivi na kuwepo na kama forum hivi ingekua bomba
ReplyDeleteWazo nizuri kama serekali angelikua na nia nzuri kwa wazo hilo na sio mazingaombwe.Hapa najiuliza nini tovuti ya wananchi?Kama sikosei lengo ni wananchi kuwasiliana na serekali moja kwa moja na kuwakirisha kero zao au ushauri wao n.k.Ninavyofahamu kero nyingi za wananchi ambao naweza kuwahita WANANCHI KWA HERUFI KUMBWA!Ni walalahoi ambao idadi yao kubwa wanaishi vijijini na katika umasikini mkubwa hakuna,internet,TV, umeme,magazeti,hatawale wenye radio hakuna pesa za kununulia betrii ondoa ya kwamba hata radio hazisikiki katika sehemu nyingi vijijini.Hapa ndipo nipojiuliza nani mlengwa Mwananchi daraja la pili na la kwanza?ambao hawafikii asilimia 30!ambao wengi nanashiriki katika tovuti mbali mbali za jamii kama Hii ya michuzi,jamiiforums,Mwanakijiji,mjengwa n.k.na Kulumbani,kujadiliana,kushauliana,kupashana habari,na kusaidiana katika maafa mbalimbali kama vile misiba,matibabu n.k.Ningeishauri serekali kuingia ubia na tovuti hizo za jamii kwani kwa kufanya hivyo watakutana na kero,ushauri na mambo mengine muhimu online katika ujenzi wa taifa letu au washiriki ktk tovuti hizo na kutoa majibu papo kwa papo na sio kuziogopa!Mijadala na malumbano ni jia mojawapo ya kuelimishana.Pili Ningeliielewa nia ya serekali kuanzisha tovuti hiyo sambamba na kutoa computer(internet)Walau kila taraafa hapo kidogo ingeniingia kichwani.MUNGU IBARIKI TANZANIA
ReplyDeleteHiyo Tovuti ni ubabaishaji tu hakuna kitu. Mimi nimetuma maoni zaidi ya mara 3 lakini hakuna hata reply. Kila ukitembelea unaambiwa wanafanyia kazi. Hivi serekali imeenda likizo? Kwa nini hawataki hata kutoa jibu la matumaini wakati niliandika miaka 2 iliyopita.
ReplyDeleteHawa jamaa wa habari maelezo ni wababaishaji tu wala wasijihami.
Michuzi hizi web site za serkali ni ubabaishaji tu. Nadhani hakuna IT wa ku update hata site zao
ReplyDeleteSikuwa na nia mbaya na kamwe sikuona ubaya wa tovuti hii.. Kubwa ambalo nilitaka kuchangia sasa linazidi kufafanuliwa na wadau japo pale nilipoandika ilionekana kama ni kitu ambacho hakieleweki lakini sasa mjadala umefunguka hasa baada ya majibu haya toka kwa wenye tovuti. Hakika wadau wanachangia sasa mada ambayo labda hata Waziri mwenye wizara hajui linalotendeka na kwamba kabaki tu kuambiwa kuna tovuti ya wananchi "kuchangia mawazo yao"!! ... Tanzania ya leo si ya jana!!!! Tuendeleze Libeneke wadau.. na hongera kwa michango hii ya kuelimishana.. Mdau dRU
ReplyDeleteTovuti ya Wananchi!!Ubabaishaji MTUPU. Kufunguka kwenyewe kazi,heri Bro. Michuz tuibatize tovuti yako kuwa Tovuti ya wananchi
ReplyDelete