Rais Jakaya Mrisho Kikwete amemteua tena Jenerali Mstaafu Roberth Mboma kuendelea kuwa Mwenyekiti mpya wa bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Julai mwaka huu hadi Juni 2012.
Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini Alyce Tesha inasema kuwa kufuatia uteuzi huo waziri wa wizara hiyo William Ngeleja amewateua wajumbe tisa katika bodi hiyo.
Wajumbe hao ni Emanuel Ole Naiko ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha uwekezaji, Ngosha Magonya Kamishna wa fedha za nje kutoka wizara ya Fedha na Uchumi, Maduka Kessy Meneja Public Private Partnership kutoka National Development Corporation (NDC), Gosbert Blandes Mbunge wa Karagwe na Mudhihir Mudhihir Mbunge wa Mchinga,.
Wajumbe wengine ni Faida Bakari Mbunge viti maalum Pemba, Prosper Victus Kamishna Msaidizi wa Mafuta na gesi kutoka wizara ya Nishati na Madini, Mwalimu Mwalimu ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Ujenzi, Nishati na Ardhi (MUNA) Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na William Haji (Mhasibu) ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu Air Tanzania Corporation (ATC).
Hivi hizi kazi za ujumbe wa bodi zinaombewa wapi? Na mimi nataka ulaji japo sio mbunge.
ReplyDeleteNataka kuona hatma ya hili sakata kwa upande wa ZNZ, jee SMZ ni double standard ama vipi! Zenj wanataka mafuta yasiwe ya Muungano na walishatoa msimammo wa Serikali, huyo Katibu mkuu wa Zanzibar boss wake (Waziri Mansour)ameshaweka bayana, yeye anamuwakilisha nani sasa wakati SMZ wanachoimoa juu ya suala hilo?
ReplyDeleteama ni ULAJI TU!!!,
mapinduzi daima mbele!!!!!!!!!
Hongela sana General Mboma
ReplyDeletefrom Carlos Muhuga
hawa watu si ni juzi tu hapa walikuwa wanapinga wabunge kuwa wajumbe wa hizo bodi kwamba kutaathiri utendaji wao wa kazi,mbona serikali yetu haieleweki?
ReplyDeleteutajua mwenyewe
ReplyDelete