akiipeperusha bendera ya Umoja wa jumuiya ya Afrika mashariki kuashiria kuzindua rasmi mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya nchi za jumiya hiyo huko Monduli, Mkoani Arusha leo asubuhi.
Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange akimwonyesha Amiri Jeshi mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete maeneo ya makao makuu ambapo Mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya nchi za Afrika Mashariki yanafanyika wakati Rais alipofungua rasmi mazoezi hayo huko Monduli,Mkoani Arusha leo.Kulia ni Kamanda wa Kamandi ya majeshi ya nchi Kavu Meja jenerali Winjoynes Kisamba.

Baadhi ya makamanda waandamizi wa majeshi ya nchi za Afrika Mashariki wakiomwonesha Amiri jeshi mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete uwanja na maeneo ya Mazoezi ya pamoja kutoka katika kilima cha Nodosoito huko monduli mkoani Arusha leo asubuhi.
Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kuna jeshi la East Africa limeundwa wananchi hatujui au mi ndo mimepitwa na mambo? Mazoezi ya pamoja kupigana na nani?

    ReplyDelete
  2. mazozi ya pamoja ya kijeshi yapo sehemu nyingi tu duniani si ajabu. ila mimi nina walakini na uwezo wa haya majeshi,kwa mtizamo wangu nadhani kwa afrika labda nchi tatu tu sitazitaja huenda ndizo zinaweza angalau kufurukuta kidogo kijeshi ukizipambanisha lets say hata na portugal tu!wengine wote nadhani ni kujiridhisha tu!!au kama watachapana wao kwa wao.

    ReplyDelete
  3. MAMBO YA 2010 HAYO KAKA haaaa!!!!! haaa!!!!! kazi kweli kweli lakini ndio mwendo: UBAVU UNAO?????

    ReplyDelete
  4. michuzi naomba kuuliza hivi hizi ziara za JK Arusha mbona ni nyingi sana. hivi kunani Arusha. au wadau mnaonaje? ni hayo tu mkuu wa wilaya ya nanihii.

    ReplyDelete
  5. kwa kweli kama ni askari kuna huyu Afande wa kulia kwa JK wakati anapeperusha Bendera.........Huyu jamaa nilishamuona tena kwenye picha nyingine. Bwana huyu ni proper Afande hana muchezo. Jamani anaitwa nani? na nini cheo chake Jeshini?
    Mzawa

    ReplyDelete
  6. Jenarali anacheka mguu sawa, heshima kulia, anapishana hatua na raisi. imekaaje hii?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...