hii ni sehemu ya maongezi ya JK na wananchi leo. kunradhi kwaliti ya picha sio bora sana na pia kuna sauti zinazoingilia mwanzoni. globu ya jamii itajitahidi kuleta clip zaidi kwa kadri mtandao utavyoruhusu maana spidi yake ni ile ile ya treni ya reli ya kati.

panapo majaaliwa na mara tu huduma za mkongo wa taifa (national fibre optic) utapotengamaa libeneke awamu ya pili ambalo liko njiani litakuwa na mambo haya na mengine mengi laivu. kwa sasa mdau unaombwa urumangie hivyo hivyo kwa sasa...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Aisee anko Michu, tunakushukuru mno kwa clip.

    ReplyDelete
  2. majibu mazuri sana,mjue kwamba demokrasi ni cheo kikubwa kuliko Raisi wa nchi. UTAWALA,MAHAKAMA NA BUNGE!!Kwa hiyo maraisi wa baadae mjue kwamba mtaingia madarakani sio kwenda kukoroga mihimili hiyo bali kwenda kuilinda na kuhakikisha mihimili hiyo inapata viongozi wenye uchungu na nchi yetu.

    ReplyDelete
  3. huyo moto wa nani tena jamani full kelele, kwani waliomba kujadiliana kwenye nyumba ya mtu? au ofisini?

    ReplyDelete
  4. nyie ndugu mheshimiwa rais ana kigugumizi? nimesikia kimtindo anakwama na kurudia looh

    ReplyDelete
  5. Shukrani bana Michuzi, nilitamani kuipata hotuba yote....lakini nafurahi angalau sijaikosa kabisa!

    ReplyDelete
  6. asanate sana kwa rais kujibu swala hili na amelijibu kisawasawa, hilo sio kosa la serikali ila ni kosa la mahakama hasa kuhusu neno " rushwa" majaji wengi bongo ndio zao na ninaweka kuthibitisha hiyo kwa sababu yameshanikuta kwenye familia yangu, jaji anaangalia mshiko

    ReplyDelete
  7. rais wangu kwishney,hakuna jipya yote ni yaleyale ukizingatia simu zilizoingia ni tatu tu kwa dk 90 hii inaonesha ni jinsi gani mambo yalishapangwa maswali yote na majibu alishakuwa anayo kaongelea barabara na umeme kwa tabora wakati swali hilo nila papo kwa hapo lakini rekodi zote anazo na kiasi cha pesa kilichotengwa sisi tumejaribu kutafuta line mpaka kipindi kinakwisha hatujapata line ziko busy lakini ni watatu tu wamepata line,pia nataka kujua mbona barabara ya dodoma mpaka babati kupitia kondoa ina miaka mingi haiwekwi lami na pesa wanasema zipo au ndio pesa zimepelekwa chalinze wakati watu wa kondoa na wanazidi kuuwawa na majambazi kwa kuvamiwa na majambazi barabarani kwa ubovu,pia inawezekana kweli kondoa ni kubwa lakini mawasiliano ya simu na redio ni tabu kuapikana katika vijiji vingi kama busi,sambwa kinyasi,na vingine vingi,

    michuzi usinibanie comment zangu hii itawasaidia wengi

    ReplyDelete
  8. mdau Sep 10, 09:10:00 AM wewe utakuwa mrangi, maana hata kiswahili chako kibovu!!! anyway lines kuwa busy mara nyingi ni mgongano wa simu zinapojaribishwa kupigwa na watu wengi, ungetuma email nadhani ingeprintiwa tu au sms. Next time tumia njia nyingine kupata mawasiliano, ulikuwa huna nia ya kumpata, umefuliaaaaaa!!!!!

    ReplyDelete
  9. kaka yangu mwenyewe michuzi, tafadhali do something, mimi sioni hiyo clip ni blank tu tafadhali mheshimiwa fanya mambo.

    ReplyDelete
  10. Kwa nini rais anaongea kama hajiamini? swali moja anaongea kalibu saa?pia mimi naona aliongelea maswali machache sana kutokana jinsi alivyokua anapoteza mda saana,,Kumbe kweli Kagame wa Rwanda yuko juu kwa kujibizana na waandishi wa habali.Napiga magoti mithupu usinipige konzi!!

    ReplyDelete
  11. Wadau mimi na swali moja, Mh alipoulizwa swali sensetive regarding kesi ya Zombe, alipoanza na KICHEKO inamaanisha nini?

    ReplyDelete
  12. Ningependa kusikia Mheshimiwa raisi anazungumzaje kuhusu maswala ya wizi,rushwa na huduma mbaya bandarini na viwanja vya ndege. Huduma mbovu,rushwa na misongamano katika hospitali za Taifa. Viwango duni vya elimu hasa swala la uvujaji wa mitihani ya Taifa. Sura,mwelekeo na matarajio halisi ya Jeshi la polisi,mahakama na bunge kwa ujumla. Dakika 90 hazitoshelezi kuchambua na kujibu maswali na hoja za wananchi.

    ReplyDelete
  13. Mbona Kubenea hakuwepo kuuliza maswali huu mchezo wa kiini macho kila media iwepo kumuuliza maswali!

    ReplyDelete
  14. Michu Kumbe Tv lako Libaya Hivyo !

    ReplyDelete
  15. hamna kitu hapo. hiyo si unavyoweza tegemea maswali kujibiwa na RAIS. hajajibu chochote uozo mtupu

    ReplyDelete
  16. Jamani kuongea na wananchi kwa kujibu maswali yao papo kwa papo si mchezo, ni kipaji na ni karama toka kwa Mungu ambacho si kila Rais au Mkuu yeyote wa nchi anabarikiwa nacho; hivyo basi washauri wa Rais wetu mnatakiwa mlifahamu hilo!!! Je mpendwa wetu JK ana karama hiyo?????? au mmetaka kumkosesha amani? Maswali matatu kwa dakika 90! doesn't make sense at all na maswali ni kama vile yalishapangwa kabla. Mh haya.

    ReplyDelete
  17. michuzi hii TV uliyokuwa ukiitazama ni ya nyumbani kwako?? kama ni home kwako kaka huna budi kubadili TV uende na wakati. nunua TV yenye hadhi yako kaka, hii imepitwa na wakati, ni ya kizamani sana!!! weka high definition that gives high quality pics weka flat screem acha ushamba wa baraka chibiliti wa cecena italy anayetumia computer ya 1967 hadi leo. halafu mwanao alikuwa anatupigia kelele mwanzoni tulikuwa hatupati sauti vizuri zaidi ya kusikia mtoto wako akililia uji wa mtama. una bahati hukuibiaibia kamera kidogo ukatuonyesha na masofa ya sebuleni kwako!!!
    Mkosa kazi, ATL US

    ReplyDelete
  18. bravo JK,umejibu vizuri sana.huyo anaosema rais anajibu maswali kwa muda mrefu ni bangi tu,majibu lazima yawe na ufafanuzi,huyu jamaa atakuwa ana damu ya kitusi maana anamsifia kagame wakati kawaida tu.hawa ndo wanaosifia rwanda kama ulay wakati last months nimepita pale hakuna cha kutisha,au vile vigorofa ziwili vitatu ndo vinawadanganya,hat dar,arusha na mwanza kuna mitaaa kama ulaya.na miundombinu ya kuvutia,acheni kusifu ujinga,tembeeni muone.

    ReplyDelete
  19. Misupu si ungeweza kurecord straight to your VCR/CPU/laptop au huna option hiyo kwenye TV yako? Kazana upate hivyo vifaa maana wewe ni mwana-habari achana na hawa wabeba box wanaokusemea mbovu

    ReplyDelete
  20. Michu nunua stand kaka....

    ReplyDelete
  21. jamani mi mbona naona kama Rais anapiga story na mtu, yani haijakaa ki- proffessional kama nilivyotegema au kama marais wengine wanavyofanya, au ndo kila mtu ana style yake? Afu anachukua too longo for 1 question na anazunguruka saaaana badala ya kujibu swali without beating round the bushes. Anyways, huo ni mtazamo wangu tu. But the good thing is tumepata nice opportunity ya kuongea na Rais directly, we hope hizo nyingine zitakuwa nzuri zaidi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...