Consul General wa Tanzania katika Dubai na Emirate za Kaskazini Bw. Ali Ahmed Saleh akiwa na baadhi ya waliohudhuria wakiwa katika kufuturu.
Mahanjumati na mambo mengine. Ila uji wa pilipili manga baadaye..

Consul General wa Tanzania katika Dubai na Emirate za Kaskazini Bw. Ali Ahmed Saleh wa pili kulia akiwa pamoja baadhi ya Masheikh waliohudhuria karamu. Sheikh Muhidin Abdulraham wa kwanza kushoto, Sharif Hussein Badawi wa pili kushoto na Sheikh Twalib wa kwanza kulia ambaye ni Imam wa Msikiti Maamur uliopo Upanga Dar es Salaam.

Consul General wa Tanzania katika Dubai na Emirate za Kaskazini Bw. Ali Ahmed Saleh akifungua kikaratasi chenye jina la mshindi wa tiketi baada ya kikaratasi hicho kuchaguliwa na moja ya mabinti waliokuwapo kwenye karamu hiyo.
Nderemo na vifijo baada ya kupatikana mshindi wa tombola
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania UAE Arch. Mohammed Shariff, kulia akipokea kasha lenye vikaratasi vya tombola toka kwa Ofisa wa Kenya Airways tayari kwa ajili ya kumpata mshindi wa tiketi ya Dubai – Dar – Dubai.

Consul General wa Tanzania katika Dubai na Emirate za Kaskazini Bw. Ali Ahmed Saleh kushoto, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania UAE Arch. Mohammed Shariff na Naibu Katibu wa Jumuiya Eng. Issa Majid Maggidi wakiwa kwenye bango la shirka la ndege la watani wa jadi KQ.

Jana tarehe 4 Septemba 2009 Jumuiya ya Watanzania UAE ilifanya karamu ya kufuturu pamoja Watanzania wanaoishi, kufanyakazi na waliokuwa matembezini UAE.
Watanzania toka Emirates za Abu Dhabi, Ajman, Dubai, Sharjah, Ras Al Khaimah na Umm Al Quwain walijumuika kwenye kwenye karamu hiyo iliyofanyika Ofisi za Ubalozi Mdogo uliopo Dubai.

Pamoja na mahunjumati ya kumwaga pia kulikuwepo na tombola ya tiketi ya ndege ya Dubai – Dar – Dubai iliyotolewa kwa hisani kubwa ya shirika la ndege la watani wa jadi Kenya Airways ambao walishiriki kwenye udhamini wa karamu hiyo.
Mshindi wa tiketi hiyo alikuwa Bibi Naima R. Nassor.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. weee! ubwabwa huo! ndo futari kuu huku. sioni mahanjumati hapo!

    ReplyDelete
  2. Naomba kuuliza.
    Katika miezi mingine(Si ramadhani)wanawake na wanaume wanakaa meza/jamvi moja kula chakula.Sasa inakuwaje wakati wa mfungo wanaume na wanawake hawakai (mezani/jamvini) pamoja kufuturu?

    ReplyDelete
  3. Assalaam to Sharrif Hussein

    ReplyDelete
  4. Uislamu na Tombola (bahati nasibu) wapi na wapi jamani...tena mwezi mtukufu wa Ramadhani??....tena katika tendo adhwiim la Iftari? Inna-Lillah Wainna- Illaihi Rajiuun!

    ReplyDelete
  5. Mie sijasoma sana dini lakini "TOMBOLA" ni bahati nasibu ama kamari, je si dhambi hii kucheza bahati nasibu wakati mnafunga na huu ni mwezi mtukufu, sasa hii si ndio ile ya kuoga kisha ukajipaka matope..wanazuoni nikosoeni kama nimekosea..

    ReplyDelete
  6. sasa hao wanakula biriani mwezi wa ramadhani, siku ya idi watakula nini?

    ReplyDelete
  7. hizo picha hazionyeshi mahanjumati bkoz watu walikuwa washafanya mambo yao(wakati izo picha zilivyopigwa) lakini ubwabwa muhogo sambusa na mengine mengi 2 yalikuwepo!mahanjumati FULL!niamini mimi niliyehudhuria

    ReplyDelete
  8. mdau ndi ujuwe ramadhan ni mwezi mwingine sio mwezi wa kawaida!
    hukulitambuwa hilo?
    aliyepotea anarudi, mwenye roho mbaya yawa safi, ... hio ndo ramadhan..
    kwa nini miezi mengine wanakaa pamoja sijui ila ni vizuri ukifika huu mwezi watu wanaupa heshima yake!

    ReplyDelete
  9. Anko Michuzi,

    Picha za Bango la Air Tanzania Liko wapi!? Au Hai-exist!?

    Mdau B anahoji.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...