Home
Unlabelled
libeneke la ray the greatest
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
wee haya wee...! na hayo mambo yenu ya "the greatest". Muangalie mwenzako Steven Maimuna, u-greatest wote hautaki sasa hivi.
ReplyDeleteHivi Viingereza vyenu vina mambo, tangu lini FAIR DECISION ikatafsirika Maamuzi sahihi?
ReplyDeleteKwenye hizo Movie hakuna shida.. Maumivu ya kichwa huanzia kwenye KIINGEREZA. Mwenzako KANYOLEWA, sasa wewe anza kutia MAJI.
ReplyDeleteRay tunashukuru kwa kazi nzuri kweli mnajitahidi.
ReplyDeleteHata hivyo kama mdau mmoja alivyoshauri hapa kwa Kanumba tafadhali tafuteni wataalamu wa kuwa wanasahihisha na kusanifu kazi zenu za usanii kabla hamjaziweka kwenye maonesho au mauzo.
Ni aibu sana na hakika ni kuchemsha kama sio kufulia kitaaluma ukikosea mwenyewe(katika sarufi (umoja na wingi - 'UAMUZI' NA 'MAAMUZI') na maana ('CORRECT/RIGHT' isn't synonymous to FAIR) kutafsiri kichwa cha habari au jina la sinema au onesho lako.
Kama jina hilo mlilitunga kwa Kiswahili basi kwa Kiingereza lingesomeka,
'THE RIGHT DECISIONS'
Kaka Michuzi mimi nawakubali kuwa hawa ni Magwiji wa Bongo katika hiyo fani lakini pia wawe wanakubali kusahihishwa vinginevyo itakuwa kama aibu tuliyoipata leo wakati Gwiji Serena Williams ananyea taranta yake hadharani kwa kutokubali kosa alilolitenda!
SWALI,KUELEWA KWANGU ENGLISH NISINGE TAFSIRI 'FAIR DECISON' KWA KISWAHILI 'MAAMUZI SAHIHI' WALIOSOMEA LUGHA NAOMBA MTAZAMO WENU.
ReplyDeleteTARATIBU TUNATOKA BY 2045 TUNAWEZA KUWA ZAIDI YA HOLLYWOOD MAANA SASA HUKO KUNACHOMEKA KILA SIKU.
ReplyDeleteNdugu yangu Ray nimefurahishwa sana na moyo wako wa kupenda maendeleo, nimefurahishwa na kitendo chako cha kusikiliza maoni ya watu na kuchukua ushauri wao na kubadilisha title ya blog yako sasa inasomeka vizuri, huu ni mfano wa kuigwa kwa wasanii wengine pengine rafiki yako Kanumba ataiga mfano wako na kuchukua ushauri wa watu badala ya kulialia na kuona ameonewa, nakupa pongezi sana kwa hilo, ukifuata mtindo huu utafika mbali Ray, sio kila mtu anawaonea wivu kama wachache wanavyofikiri. Nakutakia kila la heri.
ReplyDeleteMdau Mnoko
UKANUMBA MWENGINE NDIO HUU SASA.
ReplyDeleteVIPI MTATAYARISHA DVD COVER YA KITOTO KIASI HICHO.
JAMAA NAONA AMEWEKEWA MIKONO YA BANDIA KAMA MUNGU WA KIHINDI.
PLEASE!FANYENI MAMBO YANAYOINGIA AKILINI.
NAAMINI UWEZO HUO MNAO SASA KWA NINI MNALETA UCHAFUU HUU .
huyo jamsi bondi wa kibongo mbona pozi kama mungu wa kibaniani???
ReplyDeleteFair decision = Uamzi wa haki
ReplyDeleteRight/correct decision = Uamzi sahihi
Hii unaweza kumuuliza hata mtoto wa sekondari akakusaidia kabla hujaweka kazi yako sokoni. Tusiwe wavivu kwa mambo hata haya madogo.
Ebawana mdau wa 10:12pm u made my day to day!!yaani nimecheka sana sana, yaani wewe ni kichwa fulani, poa mshikaji tuletee vingine vya kututo vistres!!!
ReplyDeletendimbo Indonesia!!!
Ndiyo kawaida yenu kutumia maneno ya English halafu hamjui hata kiswahili chake ni kipi. Fair maana yake "haki" na decision maana yake "uamuzi". Hence fair decision ni "maamuzi ya haki" na siyo "haki maamuzi". Umeelewa???
ReplyDeleteNinawashauri muwe na kamati au board ya kufanya editing. Lakini najua hata hizo bodi nazo zimejaa vihiyo vitupu. Nchi yetu elimu kwa kweli ni ya kimaimuna jamani. Aaagh!!!
hawa WANACHOKIKOSEA UMOMBO WAO MWINGI WANAJIFUNZIA KWA WANIGERIA SASA NDIO MADHARA YAKE HAYA WENZAO WANIGERIA WAO WANA-MIX UMOMBO,IGBO NA PIGIN ENGLISH HUKU ULAYA SIE TUNAOTOKA EAST/SOUTHERN AFRICA TUNAONEKANA TUNAJUA UMOMBO KUWAZIDI HAO WAJAMAA MAANA YAKE WANA BIG DIALECT
ReplyDeleteUgomvi wangu na nyie Amitabh Bachchan wa bongo ni filamu ya kiswahili kuipa jina la kiingereza...ina maana kiingereza mwakijua sana au ndo ulimbukeni? Kwani mgeipa jina la kiswahili kisha jina la kiingereza likawa kwenye mabano isingekuwa sahihi?
ReplyDeletePOOR COVER DESIGN..! U can do better than this.
ReplyDeleteNYIE WABONGO KWENU LIPI JEMA? NAONA HAMNA KAZI ZA KUFANYA MAANA KILA KUKICHA MNASEMA WATU, JARIBUNI KUWA POSITIVE JAMANI. NA HAWA WANAOSEMA WENZAO NI WAJINGA WACHACE TU!
ReplyDeleteKwani lazima muandike kingereza jamani, kumbukeni wengi hamkusomea sanaa wala hamkwenda shule kiasi cha kuwa fit kwenye gramma, na tatizo kubwa MNATAKA KUFANYA KILA KAZI, YAANI ETI MMEKUWA MPAKA MADIRECTOR!, WAKALIMANI! FAIR DECISION SIO UAMUZI SAHIHIM, SI KILA KILICHO FAIR NI SAHIHI, Nimeangalia Movie nyingi za kibongo ambazo zina SUBTITLE ZA KINGEREZA, NI VITUKO TU!
ReplyDeleteMwana toka TMK
sasa bila mikono bandia mnafikiri hicho kitambi kingefikiwaje?
ReplyDeleteblog hii ukifungua ni lazima ucheke tu mbavu zangu wee kwi kwi kwiiii umeniacha hoi mdau uliyesema kaweka mikono kama mungu wa kihindi duh sina mbavu
ReplyDeletemiss michuzi ukerewe
Ah nyie watu mnaokosoa lugha bora muache tu!manake naona huyu ndugu yangu Ndimbo wa Indonesia ameiandika today as if it is a preposition.Tafadhali kaka.....................!
ReplyDeleteUamuzi wa Haki ni : RIGHT DECISION:
ReplyDeleteFAIR DECISION ni Uamuzi YAKINIFU.
Wabongo mnakuja kasi!?
= = =
Buffalo (huku hatuongei kiswahili ki ivo?),
New York
Kwa kweli kina Govinda wa bongo bado kazi mnayo. Inaonekana kama vile mnakurupuka hivi.
ReplyDeleteFAIR DECISION ni UAMUZI WA HAKI
CORRECT DECISION ni UAMUZI SAHIHI
Na hiyo picha imeiga picha ya sinema ya Bond, James Bond iitwayo Octopussy. Kwa nini msipate mawazo kutoka kwa wenye vipaji vya masuala ya taswira kama Michuzi? Au maswala ya michoro kama "Kipanya"? Msione ubahili kugawana na wengine kabla ya kutoa sinema.