TFF imepokea kwa masikitiko kifo cha mwamuzi mstaafu wa kimataifa, Kanali mstaafu Gwaza Mapunda kilichotokea leo alfajiri katika Hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam.

Mapunda alikuwa mjumbe wa Kamati ya Waaamuzi na baadaye Kamati ya Mashindano ya TFF kati ya mwaka 2005 – 2008 na pia alikuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Chama cha waamuzi FRAT.

Gwaza Mapunda alianza kujihusisha na masuala ya uamuzi mwaka 1974 na aalkuwa mwamuzi wa kimataifa anayetambuliwa na FIFA kati ya mwaka 1980 hadi mwaka 1984.

TFF itashiriki kikamilifu katika msiba huu ulioifika jamii ya mpira.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Gwaza Mapunda mahali pema peponi Amina
Fredrick Mwakalaebela
KATIBU MKUU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. NAMKUMBUKA SANA CHAELES HILARY, LEO NI KINDUMBWENDUMBWE HAPA TAIFA KATIKA YA YANGA NA SIMBA KATI AKIWA GWIJI LA KIMATAIFA GWAZA MAPUNDA NA MPIRA UMEAANZA PALE, UNAENDA KWA ABDALA KIBADENI KING ANAMPIGA CHENGA YA MWILI PALE MAULIDI DILUNGA NA ANATOA MAJALO PALE KWA MARTINI KWIKA

    ReplyDelete
  2. ulale pema peponi refa gwaza mapunda.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...