TFF imepokea kwa masikitiko kifo cha mwamuzi mstaafu wa kimataifa, Kanali mstaafu Gwaza Mapunda kilichotokea leo alfajiri katika Hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam.
Mapunda alikuwa mjumbe wa Kamati ya Waaamuzi na baadaye Kamati ya Mashindano ya TFF kati ya mwaka 2005 – 2008 na pia alikuwa mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Chama cha waamuzi FRAT.
Gwaza Mapunda alianza kujihusisha na masuala ya uamuzi mwaka 1974 na aalkuwa mwamuzi wa kimataifa anayetambuliwa na FIFA kati ya mwaka 1980 hadi mwaka 1984.
TFF itashiriki kikamilifu katika msiba huu ulioifika jamii ya mpira.
Mungu ailaze roho ya Marehemu Gwaza Mapunda mahali pema peponi Amina
Fredrick Mwakalaebela
KATIBU MKUU
NAMKUMBUKA SANA CHAELES HILARY, LEO NI KINDUMBWENDUMBWE HAPA TAIFA KATIKA YA YANGA NA SIMBA KATI AKIWA GWIJI LA KIMATAIFA GWAZA MAPUNDA NA MPIRA UMEAANZA PALE, UNAENDA KWA ABDALA KIBADENI KING ANAMPIGA CHENGA YA MWILI PALE MAULIDI DILUNGA NA ANATOA MAJALO PALE KWA MARTINI KWIKA
ReplyDeleteulale pema peponi refa gwaza mapunda.
ReplyDelete