Pambano la kabumbu Simba na Yanga litakalochezewa 1417 Kalmia St, Nw, Washington Dc,jumapili sept 6, saa kumi kamili(4:00Pm) limegeuza sura nyingine pale mpiga picha wa wetu alipo mkuta mmoja wa wazee wa kamati ya ufundi (pichani) akifanya vitu vyake uwanjani.
haikuweza kujulikana ni shabiki wa timu gani. Mpiga picha wetu alikua katika pita pita ya kupata picha la wanja ambalo kitale cha Yanga na Simba kitapigiwa. Shabiki alistukia kama anapigwa picha na kutishia kuvunja kamera. bahati njema mpiga picha ni mtu wa ma-kung fu hivyo akasevu.
Kambi ya Yanga bado ipo kimya mpaka sasa haijajulikana ni kikosi gani kitashuka dimbani lakini katika kudodosa inasemekana Timu zote zimeimarisha vikosi vyao kwa kuwaleta wachezaji kutoka mikoani,lakini makocha wa pande zote walikataa kusema chochote, huku Simba ikisema sisi tutashusha skwadi letu la mauaji Kaka, Jumapili Yanga hawanywi maji tunawapiga mkono, safari hii hawaingizi timu half time.
Kocha wa Yanga Yasin Manyoka amesema mpira dakika 90, simba kuongea jadi yao, kila siku sio jumapili,mpira unapodunda anaefungwa hajulikani. jumapili haiko mbali.
wakati huo huo masahihisho ya muda wa kuanza East Africa Tournament ni 11:30 Am jumamosi sept 5 Meadowbrook pk.
Asanteni na karibuni
Visit my website at
hivi kuna mahusiano kati ya kuloga na kuvaa kanzu? mbona mna kasumba za kijinga. shame on you!
ReplyDeleteHee!!!!1 Na nyie wabeba box mna kamati za ufundi! Makubwa!!
ReplyDeleteKumbe hamjasahau asili yenu eeenhe?
ReplyDeleteHaya kazi kwenu ila msije mkatoana roho.
habari zenu,
ReplyDeletemsitengeneze picha hapa na kutaka kuanza kuleta hoja za ajabu,hakuna cha uchawi hapa...nani ana mda na uchafu huo hapa Amerika...upuuzi huo upo ukouko tanzania...tumezungukwa na habari za spacewalk na sio nani kamloga nani...
alitoa hiyo picha na aibu iwe kwake
Nyie wabeba box bora mrudi tu nyumbani huko kwa obama mambo hayaendi na si mrefu wataanza kuwadunda! Tumeshawasikia wameanza kulalamika wamexico wanachukua kazi zao, you are next!
ReplyDeleteHUYU ATAKUWA DULA NA WALA SIYO MWINGINE.NINAMSIFU KWA KUENDELEZA UTAMADUNI WA NYUMBANI SIYO KUIGA YA UGENINI MWANAUME KUVAA HELENI.
ReplyDeleteRidiculous.
ReplyDeleteKwani hakuna namna nyingine ya kuwavuta watu? Ni lazima "kutengeneza" mambo namna hii kupata attention?
Come Onnnn.
Ww anon wa Amerika Sept05, 04:27:00PM mbona unahamaki hivyo? Mtu kuelezea tabia mlinazo uku ughabuni imekua kosa? Huo ndio uhalisia wako hata kama kwenye kadamnasi hii unakana!
ReplyDeletewabongo kwa uchawi lol utawaona wakirudi likizo bongo mara sumbawanga mara tanga ooh sasahizi wanabisha hapa na wakirudi likizo mabegi yao full hirizi si nawaona airport mie nipo ktk xray machine hapa
ReplyDeleteEnhe wewe Anon sept 07, 11:04 AM kumbe pale airport Xray mwaona vingi eenhe, ndio maana inakua rahisi kutukwapulia mali zetu.
ReplyDeleteWewe aonymous wa 7.36am, hulali? au ndo ulikuwa umetoka kubebe ma-box? huyo Dula gani?mpemba au wa Zaina? maanake hafanani na Dula yoyote wa hapa washington,umechemsha bro.
ReplyDelete