vijana wa jangwani
Juu ni kikosi kamili cha Yanga ya Dc kilichoitambia Simba (chini) na kuwakata ngebe bila huruma kwa kuwacharanga jumla ya mabao 5-3.
Mechi hii iliyokuwa na shamra shamra za kila aina ikiangaliwa na washabiki kutoka majimbo mbali mbali waliokwenda Dc kwa ajili ya sherehe za Labour day ilikuwa ya kuvutia.Simba ndio waliokuwa wa kwanza kuona lango la wapinzani wao lakini Yanga walisawazisha na hatimaye kupata ushindi.
Simba wamemlalamikia refa kuwanyima penalti kunako dakika za mwisho za kipindi cha pili na pia wakidai kukosa wachezaji wa akiba. hali kadhalika mchezaji wao wa kutumainiwa Libe ambaye hakuweza kufika uwanjani.'
mbali na hayo mshambuliaji hatari wa timu hiyo Said alidai swaumu imewabana wengi wao lakini hata hivyo baadhi ya wachezaji wa Yanga pia walikuwa na swaumu kutokana na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani unaoendelea.
Itakumbukwa mara ya mwisho timu timu hizo zilipokutana Simba walishinda kwa jumla ya mabao 3-2 na hii ilikuwa ni Aprili 26 wakisherehekea sherehe za muungano wa bara na Zanzibar.
wekundu wa msimbazi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. simba awatuwezi numbani ata ugaibuni Yanga oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  2. ha ha haaa uuuwwii mmewakata vilimilimi kimyaaaaaaaaaa
    miss michuzi a.k.a shatashata

    ReplyDelete
  3. kipigo hiki kimetulia kweli hapa imba kimya kimya simba kainama......... yanga.........

    ReplyDelete
  4. 'Asavali' hii yanga ya ughaibuni inatutoa kimasomaso, hii ya tanzania mwaka huu ni kimeo. tunafungwa hata na water-water ya songea? Kocha anapanga wachezaji 7 wa kigeni huku akijua hairuhusiwi, anasajili hata magarasa (mmoja anaita mba kutoka kameruni). wachezaji wanafanya fujo mpaka wanafungiwa (chuji). simba walikuwa sahihi walivyosema chuju ni nunda. tukachonga weee mpaka tukafanya 'namna' mpaka akasajiliwa yanga. haya huko taifa stars kafanya ununda huohuo mpaka kafukuzwa na 'makisio' maximo. wenye kumtetea (akiwemo kondic) wakamtetea weeeee, haitoshi kawamwagia shuzi tena. huyo ndio chuji na kocha wake.

    ReplyDelete
  5. Keshi money nimekuona Baba tunakuumbuka Holland.

    ReplyDelete
  6. Walienda wapi kuroga?

    ReplyDelete
  7. kweli ule wombo ulikuwa ni mtamu sana simba kainamaaaa yanganga kamtia dole!

    ReplyDelete
  8. Hatukuroga babuuu, Kocha Luke wa yanga amehakikisha Yanga imekamilika.

    ReplyDelete
  9. eeeeh eee kitim tim jamani tulikiona juziii nyumba ya shetani mwendawazimu kaingiajeeee????
    miss michuzi

    ReplyDelete
  10. nyie simba mlizidi sana kuchonga mmefuliaa ha ha haaa imekula kwenu mliingia choo cha kike!
    mdau ukerewe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...