mwafika merinyo (kati) akiwapiga konozzz mai waifu wake ailinda sawe (shoto) na manju msitta, wabunifu wakongwe wa mitindo ambao wanashiriki katika wiki ya mtindo ya swahili.

KUHUSU WIKI YA MITINDO YA SWAHILI
(SWAHILI FASHION WEEK)
Swahili Fashion Week (WIKI YA MITINDO YA SWAHILI) ilianzishwa Novemba 2008 na Mustafa Hassanali mmoja wa wabunifu wa mavazi maarufu nchini.

Swahili Fashion Week ni jukwaa kwa wabunifu wa mavazi na urembo mwingine kutoka katika nchi zinazozungumza Kiswahili kuonyesha kazi zao, kujitafutia masoko, vile vile kukutana na wateja. Pia ni sehemu ya kuhamasisha fani ya ubunifu mavazi kama njia moja wapo ya kujiongezea kipato na kutoa ajira na kudumisha dhana ya ‘Made in Tanzania’ ambayo inahamasisha watu kununua bidhaa zinazotengenezwa nchini.

Swahili Fashion Week inategemewa kuwa ni tukio la kila mwaka ambapo wabunifu mavazi wachanga na waliobobea katika fani hiyo kuonyesha kazi zao mpya na vile vile ni sehemu muhimu kwa wapenda fani ya mitindo kujionea ubunifu mbali mbali kutoka kwa wabunifu maarufu nchini na nchi za jirani.

Ikiwa na nia ya kutoa nafasi ya pekee kwa wabunifu wa mavazi nchini Tanzania, Swahili Fashion Week pia ina lengo la kuiweka Tanzania katika ramani ya ulimwengu wa mitindo kupitia wiki hii ya mitindo kila mwaka..
Kufanikiwa kwa uzinduzi wa Swahili Fashion Week mwaka jana ndio kulimeweza kufanikisha kwa tukio hili kubwa la mitindo kufanyika mwaka huu. Mwaka jana Swahili Fashion Week ilifanyika Novemba 5 na 6 chini ya uongozaji wa Jan Malan kutoka Afrika ya Kusini.
Katika tukio hilo wabunifu mavazi wa nchini walipata nafasi ya kuonyesha kazi zao na pia washiriki wa shindano la kumtafuta kisura wa Afrika, ‘Mnet Face of Africa’ walishiriki katika kuonyesha mavazi hayo ikiwa ni sehemu mojawapo ya shindano hilo.

Wabunifu wanaoshiriki katika Swahili Fashion Week huchaguliwa na bodi maalum ya Mitindo inayoitwa ‘Fashion Advisory Board (FAB)’. Bodi hiyo inashirikisha Emelda Mwamanga Mkurugenzi Mkuu wa Jarida la Bang, Mwanasheria Matukio Chuma, Mkurugenzi wa sanaa na promosheni wa BASATA Nsia Shalua, na mmiliki wa klabu maarufu ya starehe jijini Dar Es Salaam Abigail Plaatjees.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa onyesho hilo la mavazi mwanzilishi wa SFW Mustafa Hassanali ambaye ni mmoja wa wabunifu maarufu nchini alisema mwaka huu Swahili Fashion Week inahamasisha ‘Mitindo kama biashara.’

“Swahili Fashion Week mwaka huu ni mwanzo wa ari mpya; tunaandaa onyesho litakalohamasisha mitindo kama biashara. Tunataka kukuza shughuli za mitindo nchini ili isiwe inachukuliwa kama fani ya burudani bali mojawapo ya njia za kukuza kipato.
Ulimwenguni kote fani ya mitindo ni moja kati ya fani zinazochangia katika uchumi wa nchi, hivyo basi na sisi tungependa kusisitiza umuhimu wa fani hii nchini ili watu waipe umuhimu unaotakiwa kama njia mojawapo ya kuongeza ajira na kuondoa umaskini kwa ujumla,” alielezea Hassanali.

Wiki ya Mitindo ya mwaka huu itajumuisha wabunifu mavazi 14 kutoka mikoa mbali mbali nchini na wabunifu 6 kutoka nje ya nchi na maonyesho hayo ya mavazi yatafanyika tarehe 4 hadi 6 novemba mwaka huu katika viwanja vya Karimjee jijini Dar Es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. du yani michuzi hii post ilinichanganya au kiswahili changu ndo hakieleweki. Pale ulipoandika akiwapiga konozza my waif wake na .. kushoto na manju basi mi niliwaza wote ni wake wake kuangalia naona manju nimwanamme kweli ulinipatia chemsha bongo.
    Manju siku nyingi nilikuwa sijamsoma tangu kipindi alichobuni vazi la twiga akalivaa basila kama sikosei, nililipenda vazi lile sana. Mwendo mbele wanamitindo wetul

    ReplyDelete
  2. Mustafa Hassanali's success owes much to his flare for self-projection, PR and marketing. Arguably it is this more than his skill as a designer and couturist that has made him the best known fashion design name in Tanzania to-date. Mustafa no doubt has his equals and even superiors in design and couture in the Tanzanian fashion industry; but what these colleagues of his still have to learn from him is that fashion design is for show not just in one's studio and on the catwalk but on a myriad of other platforms and through a variety of other media in so many ways- even they know this they still have to show that they know how to do it. Hongera Mustafa for blazing the trail in not only being creative but also in being creative about projecting creativity and creating a new marketing platform to share with your Tanzanian fashion colleagues.

    ReplyDelete
  3. kaka michuzi.. nifafanulie.. hii Bodi ya Ushauri imeteuliwa na chombo gani? BASATA? ...

    Pili, najua pale UDSM Matukio Chuma alisoma Politiocal Science and Public Administration (PSPA).. kumbe ni mwanasheria? alisoma sheria baadaye? kama hivyo basi Hongera Matukio

    ReplyDelete
  4. Mmeku Merinyo na msheku shamesheni mnu. Ngakunda amu iveni ihokuto mamboeva nya kikwamotukwamotu undhusha. Ni mwanake ulya uleansa nafe kira undi, ali fo shomba.
    Shamesheni se na mnu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...