Kwako brother Michuzi,
Naomba unirushie haya machungu yangu, kwakweli sasa naona tunakoelekea ni kubaya,mimi nimejibana nikafanikiwa kupata usafiri wangu mwenyewe baada ya kutaabika na usafi wa jumuia(public transport).
Hapo natakiwa kila mwaka kukatia Bima (insurance) ambayo nikaona sawa.
ikaja unatikiwa ukatie leseni ya barabara(Road licence) tukaona sawa.
ikaja mambo ya wiki ya nenda kwa usalama, unapeleka gari linakaguliwa na unatakiwa kulipa Tsh 3000 kwa ajili ya stika(sticker) wananchi tumekubali.
Naona serekali kuona vyote hivyo sasa tunatakiwa kuwa na sticker ya Fire, hizo windscreen zipo kwa ajili ya kujaza sticker tu na kilicho kibaya gharama yake ni Tsh 20,000 kwa gari ndogo kama sio ufisadi huu ni nini tena niweke mtungi wa kilo moja gari yenyewe Toyota March kweli hii ni haki??
Wanachi wenzangu naombeni tusaidiane kwa hili, kama maisha bora kwa kila mtanzania ndio haya, tumekwisha!
wenzetu waipeleka nchi kubaya kila siku kesi mahakamani halafu zinaishia hewani na sisi tunaojitahidi angalau kidogo kitu tunazidi kubanwa. Basi boresheni usafiri wa jumuia ili tupande mabasi mbaki na magari yenu. Kesho na kesho kutwa tutaambiwa watu wa FIRST AID naona wanataka magari yote yawe na KIT na sticker zipandikwe kwa gharama wanayotaka wao.
This is too much jamani...........
tunaelekea wapi?????????
nisaidieni ndugu zangu
WENU
DaimaFuraha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Pole sana Ndugu, hiyo ndio TANZANIA ya sasa.Wala usihofu hizo sticker zipo Kariakoo, na jangwani buku kwa moja.
    Bora kuweka hizi feki, maana hata gari lako likiungua hakuna anaekulipa ni bima yako kama sio ya porini nayo.
    Otherwise Tanzania ni ujinga mtupuuu!

    ReplyDelete
  2. Kwa mtazamo wangu labda sina utaalamu sana ila kwa kuweka hii mitungi ya kuzimia moto ndani ya gari, je, ikitokea wakati wa joto umefunga vioo vyote na gari ndani kutokana na jua/joto kali likafanya mtungi ulipuke/ufumuke, jamani si hatari hiyo??

    ReplyDelete
  3. Toyota March...umeuziwa kanyaboya ndugu yangu.
    Ushauri wa bure ni kuwa tumia kura yako kuleta mabadiliko bungeni. Chaguo ni lako. Business as usual au change?

    ReplyDelete
  4. Ha ha ha ha Watz bwana mtu analalamika vitu ambavyo vina faida kwakwe mwenyewe....kama umeweza kuwa na uwezo wa kununua gari basi tuna uhakika unao uwezo wa 20,000...Ni sawa abiria/dereva kuaambiwa afunge mkanda halafu hafanyi hivyo mpaka akimuona trafik ndo anafunga mkanda sasa sijui anamdanganya nani ajali itakapotokea...Wangesema kila nyumba iwe na fire extnguisher hapo ningesaidia kulalamika sabab wengine hali zao haziruhusu kula ya shida pia....lakin kama ni gari hivyo vyote ni kwa usalama wako.

    ReplyDelete
  5. Mdau mi nadhani usalama wako na gari yako ni muhimu sana kuliko elfu ishilini (upewe na risiti ya serikali vinginevyo usitoe pesa).

    Kwa gari ndogo ni wa kilo moja, magari ya abiria ni zaidi ya kilo moja kuna mengine wa kilo mbili na magari makubwa na yanayobeba bidhaa zinazoweza kulipuka kama mafuta ya petrol/diesel ni wa kilo 4.5 au 9 sikumbuki vizuri lakini uwe wenye dry powder ya carbon.

    Hiki ni kitu kidogo ambacho wengi hupuuzia kwa kuona hakina umuhimu lakini kama hufahamu kuna watu na makampuni mengi hata hapa bongo wamepoteza magari yao ya thamani kumbwa kwa kukosa fire extinguisher tu kuzima moto ambao kama wangekuwa nayo wangokoa magari yao.


    Kuwa nayo tu haitoshi pia ujue namna ya kuitumia kwa sababu wengine wanayo kwenye gari lakini hajui namna ya kuitumia huyo ni sawa tu na ambaye hana.

    Tatizo la kuungua kwa gari linaweza kutokea wakati wowote bila kujari gari ni mpya, ya zamani au vinginevyo. Inaweza kutokea ukiwa kwenya barabara ya lami ambapo hakuna mchanga wala maji sasa hapo ndio utajua umuhimu wake.

    ReplyDelete
  6. Naomba nifahamishwe, hii gari aina ya Toyota March ndio ikoje? Ninavyojua mimi "March" ni brand ya Nissan

    ReplyDelete
  7. JAMANI HUYU MDAU HAJALALAMIKA KUWEKA FIRE EXTINGUISHER KWENYE GARI YEYE ANACHOLALAMIKA NI GHARAMA YA HIZO STICKER KWANI HIYO EXTINGUISHER UNATAKIWA KUNUNUA NA PESA ZAKO.NAONA HAMJAMUELEWA AU AKILI ZENYEWE NDIO ZERO.

    ReplyDelete
  8. Jamani unajua akili ni mali na kusoma ni kutoa ujinga na uongozi uelevu wa kutambua mambo muhimu katika jamii na vilivyo na madhara fire extinguisher kuweka kwenye saloon come on si silaha gari ikipata ajali ikampiga mtu usoni swala si hela swala kwamba wengi wliokua viongozi leo wamezaliwa bila ya magari halafu watu wakuja unajua kuna vitu inabidi wakae chini wajiulize kabla ya kutoa kwenye jamii mie sina la kuongea najua hizi kelele kwenye michuzi na zinaishia humu haziwafik wahusika lakini siku moja kuna mtu ata stand up yote yataisha ndio maana niliondoka mdogo sipo lakini inauma ukisikia vitu kama hivi yote kheri

    ReplyDelete
  9. Du!!! Hayo yote unayozungumza ki kweli mzee!! tunahitaji nguvu ya pamoja kulalamika na tusipolalamika utaambiwa first AID kit mra dust been na vikorokoro kibao. Haya ndo maisha boraaaaaaaaa!! eti WADANGANYIKA upoooooooo!!!!! kuweni na thubutu!! ya kupinga kila kinachowezekana sio kusapot haya kwani najua hao wadau waliopita woote wapo katika Mamlaka hizo hizo na wanaendesha magari ya Ofisi zao. ndio maana utafikiri wana support kumbe du!!! wana oppose ishu. kuweni kama watani wetu.

    ReplyDelete
  10. daima furaha kaka pole sana
    hila kaka wenzio wanafanya makaratee weee siku hizi wanachukua VX,na magari mazuri ya kifisadi hili wafanane nao mafisadi maana wao magari yao hakuna cha bima sijui sticker trafic akiwasimami wanamuuliza unata kazi autaki? alafu anachukua simu anajifanya anaongea "mh.nitachelewa kidogo kuna trafic hapa salenda amenisimamisha anaangalia stika alafu ana muuliza nikutumie namba yake?
    hapo trafic anaondoka huku hakiomba samahani kumbe jamaa si lolote si chochote ndio bongo darisalama hiyo
    prof, jay aliimba kwenye wimbo wa bongo "kuwa aliyeuza cheni kauza bandia na aliyetoa pesa katoa pesa bandia " so fuata ushauri nenda njoo huku mwembe yanga tukupe mtungi feki sh 2000,stika moja sh 500 hata leseni class C km auna njoo utapata ndani ya dakika 5 tu
    km unajifanya unauchungu sana na hii nchi haya lipa hiyo 20,000/= watoto wao waende ulaya kutesa hao mafisadi si wameua shule za serikali we unategema nini? akili kukichwa ukizubaa utachwa feli

    ReplyDelete
  11. Naipongeza idara ya usalama barabarani kwa kuwa wabunifu kufuatana na mazingira ya Tanzania.

    Kwani Idara ya zimamoto haina magari ya kutosha na pia ni ya bei mbaya kwa nchi kama Tanzania.

    Pia miundo mbinu kama barabara na mabomba ya dharula ya maji kwa ajili ya magari ya zimamoto hakuna.

    Hivyo ni sahihi kabisa wenye vyombo vya usafiri kuwa na mitungi ya kuzimia moto, ili kupunguza uwezekano wa kuteketea kwa mali ya mwenye gari na mali za raia wengine ikitikea moto kulipuka.

    Ubunifu huuu kufuatana na mazingira yetu ya Tanzania lazima ipewe sifa zinazostahili sio kulalamika kwa sababu ya ubinafsi.

    Mdau
    jijini London.

    ReplyDelete
  12. HUO NI UJANGALA, USANII MTUPU, HUKU HATA TRAIN HAIN MTUNGI WA KUZIMIA MOTO, HATA NDEGE HAINA, HIVI NANI ALIANZISHA UJINGA HUO!!! KWANZA NI HATARI KUWEKA MTUNGI HUO NDANI YA GARI KWANI VITU VILIVYOWEKA NDANI YA MITUNGI HIYO NI VILIPUKA, KWA MFANO VIKIPATA JOTO LA KIASI FULANI TU NI HATARI KWA WATU WALIO NDANI AU HATA KAMA LIMEEGESHWA MAHALA NA ISHITOSHE MTUNGI MOJA HAUWEZI KUZIMA MOTO WA GARI HUO NI U-ALI NACHA, TUNA MTAKA MKUU WA POLISI ALITOLEE MAELEZO HILI, HIVI WAPI ALIKOSIKIA MTUNGI HUWEKWA NDANI YA GARI NA ZIMA MOTO WATAFANYA KAZI GANI, HIYO NI HATARI NA NI BOMU LIKILIPUKA HAPAKALIKI, HAYA HATA WANATAKA KULAZIMISHA BASI PESA WANAYOCHUKUWA YA NINI JUU YA STICKER WAKATI MTUNGI HUNUNULIWA NA MWENYE GARI NA NI KAMA NI MOJA YA USALAMA WA GARI NA DEREVA KWANI STICKER YA WIKI NENDA KWA USALAMA HAJUMULISHI NA HUO MTUNGI, AU NDO MNABUNI MRADI WA KUCHONGA PESA WATU WANATOWA RUSHWA YA BILA KIJUWA, NI TENDA YA MKUBWA KUCHONGA STICKER, NA MKUBWA MWINGINE KUAGIZA MITUNGI KAMA NAMBA ZA GARI LAZIMA ZIWE ZA MASASI SIGNS ZA KARIOKOO HAMZITAKI ZA SHS 1000. MKUBWA KACHONGA DEAL LAKI NAMBA ZOTE ZOTOKE KWA MASASI HIVI HAWA VIJANA WA KARIAKOO WAKALE WAPI ALAFU NDO MNALALAMIKA MAJAMBAZI WAKATI AJIRA ZOTE MNATAKA ZIWE ZENU KWANI NINI WASIIBE VIJANA NA KUUWA WATU WAKATO VYANZO VYOTE VYA PESA MNATAKA VIWE VYENU. HII KITU YA MTU SAID MWEMA TUPE UFAFANUZI, MLICHOMOWA WAPI HII DESIGN, NIMETEMBEA SANA NCHI NYINGI SIJAIONA HII MPYA ON TOP OF THAT MUNATAKA MTU ANUNULIE STICKER, JAMANI MOTORISTS TUANZISHE CHAMA CHETU CHA KUTUTETEA MAMBO HAYA YA KIJINGA - SAID MWEMA TUNATAKA MAELEZO, IKIBIDI TUANDAMANE KWA WAZIRI USIKA NA KWA RAIS PIA TUMECHOKA NA HIZI KODI MNAZOTUKAMUA ILI MUONGEZEANE MISHAHARA NA MARUPURUPU MUJINGE VIGOROFA MBUZI HUKO OSTERBAY

    ReplyDelete
  13. mdau anonymous @0650, mbona waongea machicha, unaishi london wewe ulishaona Brown ana national private jet, pesa walizotumia kununua ndege ya rais wangenunua fire engines ngapi? even second hand, nimeziona huko uk for less than £10,000/-, AU NAWE NDIO TOTO LA FISADI ULIOPELEKWA UK KWA PESA ZA WALALA HOI, Waombe wananchi msamaha, kabla hatujapasua jipu

    ReplyDelete
  14. Anonymous Sat Oct 17, 09:00PM
    Nimeshaona gari ndogo nyingi hapo Tanzania toka Ujerumani kama Mercedez Benz miaka ya 1990, na zina mitungi midogo ya kuzimia moto chini ya 'dash-board' sehemu ya abiria wa mbele anapoweka miguu na kifaa hicho-mtungi unakuja na gari lililo 'brandnew'.

    Hivyo siyo kweli wenzetu ulaya hawana kitu kama hicho. Ila wenzetu wana 'advantage' ya kutokuwa na 'ulazima' wa mitungi ya kuzimia moto. Hii inatokana kuwa na vituo vya magari ya zima moto kila 'tarafa' na wana uhakika wa zimamoto kufika ndani ya dakika 5.

    Hivyo bado kabisa hiki kifaa cha kuzima moto(mtungi) ni muhimu kwa mazingira yetu ya Bongo kutokana na ukosefu wa miundo mbinu ya kisasa na pia hata jiji la DSM kituo pekee cha zimamoto kipo hapo karibu na shule ya sekondari Jangwani.

    Hivi kituo hicho pekee cha zimamoto DSM kinaweza kuhimili 'miito' ya moto sehemu zote za Jiji? . Uwanja wa Ndege na Bandari ni taasisi muhimu kuangalia usalama wa moto kutokana na ndege au meli kuwa na shehena ambazo ni hatari hivyo hawawezi kutegemewa kulihudumia jiji la DSM.

    Hivyo kwa kipindi hiki tukubali huu ubunifu wa idara ya usalama barabarani kujikinga na ajali za moto.

    Mdau
    jijini London.

    ReplyDelete
  15. I don't get it. Hiyo hela ni ya kufundishwa jinsi ya kutumia huo mtungi au kuonyesha tu kuwa una mtungi kwenye gari yako? Kwanza hiyo mitungi na weather yetu, inaweza kugeuka kuwa ammunition.

    Halafu kama ni kuzima moto kweli itabidi kila mwenye gari ajali ilikotokea atoe mtungi wake ili wazime tu kagari kamoja.

    Na ku-refill ni wapi, njiani kutakua na station za kurefill hii mitungi? Au ndio disposable? Wengine watakua nayo tu kwenye magari empty.

    Ni hiyo tenda ya nani tena? Ulaji hapo.

    Hakika kwa mlala hoi ukiweka leo elfu 20,000, kesho tatu, kesho kutwa sijui 10,000 zinadd up kishenzi. Gari bado ni luxury sana tu Tanzania.

    ReplyDelete
  16. MTUNGI MMOJA HAUZIMI MOTO WA GARI, BENZ ZILIKUWA NA MITUNGI ETI ZAMANI.

    SASA SIKU HIZI IKO WAPI? WENZIO WALIFANYA REVIEW (HEALTH AND SAFETY) NA KUONA HATARI YAKE WAKAACHA KUFANYA HIVYI NA HIYO HAIKUWA POLICY YA NCHI NI KIWANDA CHA BENZ NA HAIKUWA SHERIA YA NCHI.

    TUKUBALIANE HUU NI UPUUZI NA ULAJI TU NA HATA KAMA NI LAZIMA KWA NINI ISIUNGANISHWE NA UKAGUZI WA MAGARI WA WIKI NENDA KWA USALAMA IN PRINCIPLE THAT IS WHERE IT SHOULD HAVE BEEN NOT SEPARATELY, KWANI WIKI YA NENDA KWA USALAMA HUWA WANAKAGUWA NINI? KAMA SI USALAMA WA MAGARI IKIWA PAMOJA NA UJANGALA WAO WA MTUNGI WA KUZIMIA MOTO, BASI SI ZA MBELENI WATAKUJA NA HOJA INGINE YA KUKAGUA BREAK NA KUPEWA STICKER NA MALIPO JUU, HUU NI U-KIHIYO IF THAT IT IS ABOUT SAFETY THEN WHY NOT BE TOGETHER WITH WEEK YA USALAMA BARABARANI KWANZA MTUNGI HAUZUWII GARI KUUNGUA MOTO SO SI KITU KINACHOWEZA KUZUWIA MOTO KUTOKEA KAMA VILE BREAK INAWEZA KUZUWIA KUGONGA MTU. LET US BE ANALYTICAL WHEN ISSUES LIKE THESE COME TO OUR ATTENTION. ETI MMOJA ANASEMA UMESHAONA BROWN ANA-PRIVATE NATIONAL JET, KWANZA HAKUNA RAIS MWENYE PRIVATE JET, ZOTE UNAZOZIITA PRIVATE JETS NI MALI YA SERIKALI HUSIKA NOT PRIVATE, HATA HUYO BROWN WA UK HAPANDI NDEGE PAMOJA NA KAJAMBA NANI WENGINE (ABRIA) WENGINE NI SPECIAL BA JET IKO KWA AJILI YA PRIME MINISTER ANAPOSAFIRI NJE YA NCHI INA OFISI, CONFRENCE ROOM, MEDIA PRESS BRIEFING ROOM, GYM, A ROOM FOR MEDICATION UNAWEZA KUITA HOSPITAL NA HAITUMIKI KWA SHUGHULI INGINE YOYOTE ILE, MAYBE THE SAME COULD BE USED WHEN THE QUEEN TRAVELS ABROAD WHICH IS VERY RARELY NA HAINA MTUNGI WA KUZIMIA MOTO. USIROPOKE BILA UTAFITI. KWA KUMALIZIA HAMNA GARI YOYOTE YENYE MITUNGI ULAYA KWA SASA NA HII NI BAADA YA STUDY YA HEALTH AND SAFETY ILIYOFANYWA NA EU COMMISION WALIPIGA STOP LONG TIME AGO MAKAMPUNI YASIWEKE HIYO KITU NI HATARI. SO ACHENI UBABAISHAJI.

    ReplyDelete
  17. Mimi naona huu ni wizi mtupuuu!!!!!hakuna lolote.
    Hayo mahela waliyo nayo TRA ya Payee as you earn nasikia yanaibiwa mabilioni kila siku.TRA wana hela nyingii mnoo mpaka wanashindwa hata kuziangalia na kuzitunza zinaibiwa kila siku. Bado wanataka kuwakamuwa wananchi wake. Loohh nchi hii jamani kasheshe hivi tutafika lini safari yetu ??? watu ni wizi wizi wizi saa zotee..
    Wanatakiwa wakusanye kodi vizuri toka kwa walipa kodi wotee hasa ndugu zetu wahindi hawalipi kodi vizuri hata kidogo, jamani serikali angalieni mnaongeza ukali wa maisha.

    ReplyDelete
  18. kwa ufupi wafanyakazi wengi serikalini ni wavivu wa kila kitu na waonevu. kudai tsh 20000/= kwa sticker tu ni unyang'anyi, afadhali kama katika gharama hiyo pia ungepewa mafunzo (sio maelekezo) ya namna ya kuitumia hiyo fire extinguisher. lakini pia serikali kutaka watu kufunga mitungi hiyo kwenye magari yao ni kukwepa jukumu lao la kuboresha huduma za zimamoto katika miji yetu. kama inavyokwepa kusafirisha wanafunzi na kulazimisha wenye daladala wakati kuna uda ambalo ni la serikali ni kuamua tu uda asubuhi na jioni zibebe wanafunzi. pia kuna mabasi ya jeshi yanaweza kusaidia.kushindwa kutanua na kujenga barabara mpya kupunguza traffic jams badala yake kulaumu vipanya, vipanya vimepungua mjini traffic jam mjini imepungua? kujaza sticker kioo cha mbele ni hatari kwani kinapunguza uwezo wa dereva kuona mbele. kama lengo lingekuwa kuongeza usalama moto unapotokea basi fee yake ingekuwa chini sana ili kila mtu aweze kumudu na si 20000/. kuhusu ndege kuwa na mitungi hiyo, ndege zote zina mitungi hiyo lakini midogo midogo na kila mfanyakazi katika ndege amefundishwa na anafundishwa mara kwa mara namna ya kuitumia,na lengo la mitungi hiyo ni kujaribu kuokoa abiria wasidhurike na moto na si kuokoa ndege isiteketee kwa moto. kama ni kitengo cha fire and rescue kimeamua hivyo, basi wanataka nao waonekane wanazalisha ingawa ni kwa unyang'anyi. na kama ni polisi ofcourse polisi wanaeleweka.(ulinzi shirikishi??). mdau mmoja amesema hana tatizo kwa sababu mitungi hiyo inatakiwa kwenye magari na si majumbani, namuonea hurumu kwa kuwa ziro kichwani, kwani majumba hasa ndio wangelazimisha kuwa na mitungi hiyo, gari yangu ikiungua mimi nimepona nakusanya chuma chakavu narudi nyumbani kwangu kulala. nauza, nyumba yangu ikiungua naende kulala wapi na familia yangu, kwenye gari? napenda kumtia shule huyo mdau kwamba thamani halisi ya mali sio ulinunua shillingi ngapi bali uhitaji wake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...