Kaka Michuzi,
Ninawaomba wadau wanipe ushauri kuhusu suala moja muhimu. Nina mpango was kununua FUSO kutoka Japani. Kuna watu wananishauri kununua Fuso ya mizigo na kuna wanao nishauri kunua ya kubebea mchanga wa ujenzi.
Wadau naomba ushauri wenu, mimi nimetoka bongo miaka kama kumi, kwa hiyo siijui hali halisi. Lakini ningependa kununua hii kabla sijarudi bongo mwakani mwezi wa tano.
Asante,
Mdau Japani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Kwenda Bongo kwanza usiwe na haraka
    go see for yourself, do not count
    on other people, that is what I did
    I'm going back and I'm well set

    ReplyDelete
  2. kanunua fuso ya mizingo, achana na hiyo ya kubebea mchango wa ujenzi.

    ReplyDelete
  3. hi there
    ushauri wangu nunua lori la mchanga au kwa jina lingine TIPPER biashara yake ni ya kilasiku sio ya msimu kama ya mizigo this is my line of business for futher info contact me on NTL@nunuatokalondon.co.uk
    urs Jayjay at
    www.nunuatokalondon.co.uk

    ReplyDelete
  4. Mdau.
    kitu cha msingi hapa kinachoonekana ni kuwa unataka kufanya hii biashara ambapo huna idea inafanywaje au itaambatana na vitu gani hapo baadae.
    Hili ni tatizo kubwa sana kwa watanzania wengi, kufanya mambo kwa kufuata mkumbo na ile "mentality" ya kuwa "hii inalipa sana" kwa kuwa fulani na fulani wanaifanya tu.Go back to the basics, fanya survey ya kutosha mwenyewe na kujiuliza ndani ya nafsi yako kama kweli hii biashara ndio unayotaka fanya. Kuuliza kwenye hii forum kunasaidia pia lakini cha msingi ni kuwa wewe ndio uta invest hapo na pesa itatoka mfukoni mwako.Watoa maoni hapa wengi watakuwa hawana watakalopoteza iwapo mambo yako yatakwenda mrama hapo baadae!

    ReplyDelete
  5. Nunua maFUSO matatu kaka.
    1. La kubebea mchanga
    2. La kubebea mizigo
    3. na la kutemebelea mitaani na Coco Beach siku ya umapili.

    ReplyDelete
  6. Biashara Yangu Team will do a research and give you feedback!Please,let us know you most concerns, then we will know what kind of research to be conduced.

    contact us anytime through our email address;biasharayangu@gmail.com

    OUR SERVICE IS FREE OF CHARGE

    ReplyDelete
  7. Bila shaka concern yako ni ugumu wa kununua FUSO unalolitaka ukiwa Tanzania. Lakini ni muhimu sana kufanya utafiti wako binafsi wa biashara unayotaka kuifanya kabla hujaingiza mtaji kwenye hiyo Biashara. Maoni ya jumla yatakusaidia kidogo sana, maana kuna watu wanafanya biashara ya aina moja na wengine wanapata hasara huku wengine wakipata faida kubwa. Mchanga au Mizigo, vyote vinatememea sana strategy zako, uaminifu na utendaji kazi wa watu unaofanyanao kazi!

    ReplyDelete
  8. ALLAN MAKWAIAOctober 18, 2009

    This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  9. Ndugu yangu fuso ,kufanya buss bongo au Africa ni 100% risk na ni 100%profit kama utafanikiwa ,kila kitu bongo dili watu awana mitaji,ila cheki sana,wish u luck

    ReplyDelete
  10. kama utakuwa wewe ndiye msimamizi basi biashara yoyote ile inalipa

    BWAWA LA NYONGO... VIPI? MBONI SIONI MATOKEO SIKU HIZI

    glory, glory..

    ReplyDelete
  11. Biashara zote mbili zinalipa sana. Ila kuna wengine haziwalipi pia. Kulipa au kutolipa kwake kunategemea na madalali unaowatumia. Kwani kwa Bongo biashara ya michanga na mizigo kwa ujumla inategemea na madalali wanaotafuta mizigo, ukipata dalali shapu utapata kazi mpaka utakimbia au utazalisha Fuso lingine. Ni hayo tu.

    Mdau
    Makumbele.

    ReplyDelete
  12. ndugu nunua tipper ya mchanga tena hiwe MitsubishiFuso, Engine type 8DC10, kama utaipata iliyo bomba basi mwaka tu mjomba inakulipa,kisha unao huwezo ya kuiuza na kutafuta ingine

    ReplyDelete
  13. Michuzi matokeo na picha za bwawa la maini vipi au tumeshatupa taulo

    ReplyDelete
  14. Gari ya mizigo inalipa zaidi ila ni kwa wale ambao wana kampuni za kusafirisha mizigo na wana magari mengi
    Gari ya mchanga inalipa kwa sababu unapata hela kila siku (hesabu) ila nakushauri ununue tipper ya tani 18+ (double diff) hivi vya tani 5 viko vingi sana soko lake si kubwa sana

    ReplyDelete
  15. Ushauri wangu kwako ni:

    1. Usifanye biashara kwa kuiga.

    2. Fanya biashara ya kitu ambacho unakijua na una imani nacho.

    Biashara ya magari (lori la mchanga, lori la mizigo, teksi, daladala, mabasi ya mikoani, magari ya kukodi ya harusi nk) ni ngumu na ina risk nyingi. Usiianze kwa kufuata ushauri kwenye blog ya michuzi.

    ReplyDelete
  16. I GUESS THIS IS YOUR FINAL SHOT, SO BE CAREFULLY, WHAT YOU CAN DO IS THAT DON'T BE MYOPIA AND THINK MYOPICALLY, IF YOU CAN GO BY YOURSELF DO A MINI STUDY OF VARIOUS BUSINESSES GOING ON IN TANZANIA NOW, A BIT OF A MARKET RESEARCH, BUSINESS DEVELOPMENT RESEARCH, LOOK AT DEMAND AND SUPPLY, LOOK AT COMPETITORS AND HOW THEY DO THEIR BUSINESS, FIND YOUR NICHE MARKET FOR WHTA YOU WANNA DO, THEN GO BACK TO JAPAN AND THERE AS WELL TRY TO SEE WHAT KIND OF BUSINESS YOU CAN IMPORT TO TANZANIA, NEW AT ITS NATURE BUT ONE WHICH BUYABLE BUT OUR NEED AND PURCHASING POWER, AS WELL YOU CAN DO AN INCOME SURVEY OF TANZANIA, ALSO DON'T THINK OF DAR ES SALLAM ALONE THINK OF THE ENTIRE COUNTRY, MANY OF US WE DO THAT A GRAVE MISTAKE OF THINKING IS IS DAR ES SALLAM ONLY, WE TEND TO FORGET THAT THERE IS THE MONEY TOO UPCOUNTRY. SO MY BELOVED FRIEND THINK BIG, MORE THA TWICE AND DEEPLY BEFORE TAKING A PLUNGE INTO WHAT YOU WANNA DO. TANZANIA USIWAAMINI WATU FANYA MWENYEWE KILA KITU SIMAMIA FROM A TO Z FROM ONE TO INFINITY, UKIWAAMINI WATU WATAKULIZA HATA NDUGU NI MOJA TU

    ReplyDelete
  17. Kaka michuzi, nashukuru kwa ku post hii.

    Wadau, nawashukuru sana kwa maoni na ushauri wenu. Kama kuna mtu mwingine ana mtazamo tofauti keep the posts coming.

    Mdau Japan

    ReplyDelete
  18. Usiwe na haraka ,keep your maoney until when u get back home,halafu fanya uchunguzi mwenyewe kwa drivers na owners wa hayo mafuso.Unaweza order ukiwa bongo na utakuwa na uhakika zaidi na uamuzi unaotaka kufanya, si ajabu ukangundua kuna business nyingine ambazo ni nzuri na ngeni kuliko hiyo ambayo imeanza siku nyingi sana na wengine wameshaichoka

    ReplyDelete
  19. KWA USHAURI (USIRUDI NA HELA, NUNUA GARI - UKISHAFIKA HUKU NI VIGUMU KUAGIZA GARI, UTAPELI, PIA UTAKAE MWAGIZA ANAWEKA HELA KUBWA SANAAA CHA JUU)

    WEWE NUNUA GARI UKIFIKA UKIONA HUKU IPENDA HIYO BIASHARA UNAWEZA KUUZA TENA NA KUFANYA BIASHARA INGINE.

    UKIJA NA HELA POPO BAWA WA BONGO WATAZILA. HUTAJUA ULIPOPELEKA (((UTAJUTAAAAA))) NA WAKIMALIZA KUZILA HUTAWAONA KAMWE. USIJIDANGANYE ETI UTAKOMAA NAZO NI UONGO.

    TAFADHALI NUNUA GARI BIASHARA ZOTE ZINALIPA (ILA PIA LORI LA MCHANGA NI RAHISI KUMANAGE ZAIDI)

    UKIRUDI NA HELA, ILI UFANYE SAVEY KWANZA, UTAKUJA FANYIWA SAVEY NA UKIMALIZA HUNA HATA SENTIIIII

    MAISHA BONGO NI MAGUMU - WASIKUDANGANYE.

    ReplyDelete
  20. Ukinunua gari zingatia pia ushuru wa kuiclear port. uliza kabisa manake itakuwa nusu au zaidi ya hela ya kununulia.

    Ukitaka everyday return nunua la mchanga. La masafa marefu inategemea dalali wako na connection[nchi jirani na mikoani] na makampuni au port kusafirisha mizigo.

    Karibu sana na nakutakia kila la kheri. Pia nakushauri kuwa na another small business idea for plan B iwapo hii itachukua muda kupick.

    Mama B

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...