Joel Natalino Santana
Kocha wa Bafana Bafana, timu ya Taifa ya Sauzi, Joel Natalino Santana kibarua kimeota mbawa na hana kazi kuanzia leo. Yaani huyu bwana katika mechi tisa walizocheza Sauzi wameshinda moja tu.
Juzi juzi tu baada kupigwa na Norway pamoja na Iceland wakubwa wakaona isiwe taabu. Anza!
Inasemekana baada ya yeye kuondoka Alberto Perreita (Mbrazil pia kama Santanta),ambaye alijiuzuru ili akamuuguze mkewe, huenda akapewa mikoba ya kuionoa Sauzi tayari kwa kombe la dunia miezi takriban minane ijayo.
Ukitaka undani wa Joel Natalino Santana
Na ukitaka kumuona laivu bofya linki hii
Jamaa watakuwa wamechemsha kama watamchukua tena Parreira. Kama wanataka Mbrazil wamchukue Big Phil au Maximo. Vinginevyo bora wamrudishie jukumu mzalendo Clive Barker.
ReplyDeleteWasauzi hawafundishiki,hata aje kocha gani hakieleweki,Pereira aliyaona mapema akasepa,madai mkewe mgonjwa..hawa bwana waambie Rugby na Cricket hapo swadakta...Jamaa wana kila kitu cha kuwawezesha kuwa na timu fresh,ila hawafundishiki..si wapenzi wa soka kiiivyo,Yani unaweza siku uko Pub unataka cheki game labda ya Arsenal vs Man U,yani kama kuna Local Rugby game wanaonesha kwenye Tv Basi hamwangalii soka,walivo ovyo hawa watu...na mpira kuangalia nyumbani havinogi,inabidi urudi ukaangalizie home tu...
ReplyDeletehawa jamaa wakitaka timu yao iwe nzuri waache ubaguzi wakuto wachagua wazungu unaona timu zao zenye wazungu wengi zote zinatamba ulimwenguni mfano Rugby ni wolrd champion Cricket wapo juu sana ktk ulimwengu sasa hii soccer wapo mwisho sababu ya ubaguzi wao au wanunue wachezaji toka tanzania ndo itawasaidia hahaha
ReplyDeletenafikiri 2010 kwa sauzi itakuwa kama switz & austria euro 2008
ReplyDeletenasi tujifunze kutoka kwa South Africa Maximo kafanya nini Tanzania zaidi ya kila siku kuambia ummah kuwa anajenga timu toka ameanza ni kujenga timu tu hakuna kipya kila siku ana wachezaji zaidi ya 1000 kila leo ni kujenga timu lini atamaliza hebu na sisi tumfukuze maaana huu ujinga ndio unaifanya Tanzania kila siku kuwa nyuma kwenye kila kitu kwanini hatuwi wakweli kwenye nafsi zetu. kuwa kamaliza ufundi wake na sasa hawezi na hatoweza tena huko mbele aondoke tupate mtu mwingine mbona tunabadilisha wawakilshi na wabunge tukiona hawawezi yeye nani tumechoka na Rushwa hii ya maximo basi nae afunge virago arudi kwao hakuja kuwa jugde wa miss Tanzania hapa
ReplyDeleteWatanzania tuseme basi . nawakilisha
...wewe ni mpumbavu! na yeyote anae lalamika kuhusu MAXIMO ni mpumbavu kama wewe!! Pia hujui soka ndio maana huwezi ona nini MAXIMO amefanya!!
ReplyDeleteunajua huko nyuma tulikotoka kulikuwa hakuna hata mchezaji mmjoa aliye lelewa kisoka? (kwenye academi)umeona mabadiliko ya wachezaji makinda waliokulia kisoka nini wanafanya kwenye ligi kwa sasa? unajua wafungaji bora wa sasa ni vijana wa MAXIMO (BOKO, TEGETE, MGOSI na wengine wengi)
unafikiri kufanya vibaya kwa TANZANIA kwenye medani ya soka sio TATIZO la Kocha, bali ni maandalizi finyu ya huko nyuma, na hiyo Rushwa unayoongelea ni WAKINA NDOlanga?
na UNAjua kuwa Tatizo la SOUTH AFRICA kufanya vibaya sio KOCHA? mimi nipo SOUTH AFRICA naona mipira mpaka ya mchangani, hawana vipaji, na wabaguzi. Perreira ni world class coach na kachemka, kipindi walichokuwa wanafanya vyema kwenye soka ni zama zile ambazo TImu zetu na NNCHI nyingi za africa hawakuwa serious na mpira!!
BIG UP!!! MAXIMO you are doing a very wonderful job, keep it up!!!