Mh. Spika Samwel Sitta anahudhuria mkutano wa umoja wa mambunge duniani a.k.a International Parliamentary Union (IPU) , mjini Geneva uswisi ambapo ameongoza ujumbe wa wabunge wanne na waziri mmoja toka Tanzania ambao ni Mh. Kilonsti Mpologomyi, Mhe. Suzan Lyimo, Mhe. Dr. Mwita haji, na Mhe. Idris Mtulia pamoja na Waziri Mhe. Margareth Sitta.
Katibu wa spika, Daniel Eliufoo, akimfafanulia jambo Mhe. Dr. Idris Mtulia katika mkutano huo. Mbele ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, mhe. Magreth Sitta, ambaye nae anahudhuria mkutano huo. Kwa nyuma ni mhe. Dr. Mwita Haji.

Mh. Spika Samwel Sitta akisalimiana na baadhi ya wabunge toka bunge la uingereza ambao wengi wao wamemiss matukio waliyoyafaidi wakiwa Tanzania kwenye mkutano wa 55 wa CPA.


Mdau Owen David, afisa habari wa Bunge, naye hakuwa nyuma sana katika mkutano huo



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Nimefurahi kuona jina sahihi la nchi limendikwa litakiwavyo UNITED REP OF TANZANIA .

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi naomba uweke a message kwa watu kumpigia kura dada yetu Elizabeth, tunatakiwa kumpigia kura Elizabeth kwa wingi na siyo mtu mwingine...dada yenu kwa mara nyingine yupo nominated...

    ReplyDelete
  3. dah! owen! sasa hivi inatakiwa uwe mwali ndani tu.tunasubiri harusi next wiki.martina

    ReplyDelete
  4. nimependa hivyo viti vya kwenye hiki chumba cha mikutano, hapo hakuna kulala sio ile mi sofa ya DODOMA ndo maana wabunge wanalala, humo ni kuchangia mswada ukilala lazima uanguke.
    Spika kama kuna uwezekano ahirisheni kununua VX2 mbadilishe viti kwenye chumba cha bunge kuongeza ufanisi wa mijadala, najua litapingwa sana wazo langu.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa hoja ya vitu nakuunga mkono pamoja na mguu kabisa. Vitu hivyo hakuna kulala.

    Dodoma viweke kama hivyo pia.

    ReplyDelete
  6. Mama Sita anaelekea kulala kwenye vijanja. Lakini wapi, akilala watu wengine wanamuona hivyo hawezi kwani kuna nafasi ya kutosha katika ya meza na meza. Sio kule Dodoma watu wanajificha nyuma ya wengine na kupiga usingizi.

    Kazi kazi tu hapo.

    ReplyDelete
  7. dah wee amdau #3 toka juu
    una akili sana duh nimebidi nichunguze ivo viti yan una mawazo yaenye akili saaaaana,ivi viti vinawafaa sana SANAAA bungeni Dodoma hakuna"kutafakari" yani ni kazi tu,ata maofisi yetu uko kwa wakubwa utakuta kochii kwanini usilale-lale tu!!

    ivi viti poa sana,afu mke na mume wote walienda kama wajumbe????

    asante

    ReplyDelete
  8. hivi we michuzi umevaa kale kafulana?? mbona una kisirani namana hiyo utadhani una mimba changa nani kakuambia ubane meseji yangu??? kitambi kama fuko!! simaanishi fuko mfuko noo ni kile kimnyama kinachokaa aridhini!!!!!

    ReplyDelete
  9. Ama kweli jina sahihi la nchi linanzia na neno 'UNITED'

    ReplyDelete
  10. ona sasa picha ya mwisho alivokaa tansiooo,,wee hakuna kulala na ivi ata meza hakuna unashika adabu km ni 5-9 hours,,,lazima per diems zenu mzitendee kazi uko alaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...