
Na Mwandishi Maalum
New York
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio la kuizindua rasmi Julai 18 kuwa siku ya Kimataifa ya Nelson Madiba Mandela. ( Nelson Mandela International Day)Na itaanza kuadhimishwa rasmi mwaka 2010.
New York
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio la kuizindua rasmi Julai 18 kuwa siku ya Kimataifa ya Nelson Madiba Mandela. ( Nelson Mandela International Day)Na itaanza kuadhimishwa rasmi mwaka 2010.
Azimio hilo ambalo liliandaliwa na Ubalozi wa Afrika ya Kusini katika Umoja wa Mataifa, na kuungwa mkono na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zaidi ya 120. Pamoja na mambo mengine inataka jumuia ya kimataifa kuiadhimisha siku hiyo katika namna inayofaa.
Julai 18 ndiyo siyo aliyozaliwa Mzee Nelson Mandela mpigania ukombozi na rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini huru.
Madhumuni ya siku hiyo ya Mandela na kwa mujibu wa azimio hilo , ni kutambua na kuheshimu mchango wa kutukuka ambao Nelson Mandela ameutoa, katika kupigania uhuru na demokrasia nchini afrika kusini, kupigania usawa na haki, kupinga utawala wa kibaguzi dhidi ya dini, rangi, kabila na jinsia na kujenga utamduni wa amani na maridhiano.
Kila mzungumzaji aliyesimama kuchangia umuhimu wa kuwa na siku ya Nelson Mandela kimataifa, alimuelezea kiongozi huyo , kama kiongozi wa aina yake, ambaye licha ya mateso aliyoyapata kutoka kwa utawala wa kibaguzi wa makaburu, lakini aliamua kwa nia ya dhati kuwasamehe wabaya wake.
Na kama hiyo haitoshi, akaanzisha mchakato wa mapatano na maridhiano. Mchakato uliolenga kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini bila ya kujali tofauti zao.
Akizungumza kwa niaba ya serikali ya Tanzania , Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Augustine Mahiga, akiungana na wasemaji wengine, anaeleza kwamba katika mambo yote ambayo Mandela aliyasimamia, kuyatetea na kuyapigania.
Kati ya yote hayo kubwa ni ule wito wake kutaka maridhiano na makaburu watu ambao walimfunga na kumtesa kwa miaka 27.
“ Hiki ni kielelezo hai na ambacho kinatakiwa kuigwa na jumuia ya kimataifa. Umoja wa Mataifa unatakiwa kurithisha vizazi vijavyo kwa kuadhimisha na kusherehekea siku Kimataifa ya Mandelea ambayo leo tunaipitisha kama sehemu ya kuendeleza na kudumisha utamaduni wa amani” akasema Balozi.
Akasema katika kilele cha umri wake wa miaka 92, Mandela anabaki kuwa alama ya mapambano ya uhuru, usawa na demokrasi dhidi ya utawala wa kibaguzi, ubaguzi wa aina yake kupata kutokea katika mfumo wa siasa za karne ya 20.
“Mandela yuko katika kilele cha maisha yake,
maisha ambayo yamekuwa tafsiri sahihi ya amani ndani ya Afrika ya Kusini, Barani Afrika na dunia kwa ujumla. Ni alama ya ushujaa pale kwenye machafuko, mwenye moyo wa shupavu mbele ya kifo, aliyesimamia hadhi dhidi ya udhalilishaji, na mwenye ukarimu dhidi ya dhuluma. Na zaidi ya yote ni alama na kielelezo cha utafutaji wa haki kwa gharama yoyote ile” anasisitiza Balozi Mahiga.
Balozi Mahiga anabainisha kwamba, kwa sasa Mandela ndiye kiongozi hai aliyebaki kati ya viongozi wengine maarufu na mashuhuri wana-afrika na ambao ni watangulizi wake.
Anawataja viongozi hao waliokuwa mstari wa mbele katika kuendesha vita vya ukombozi, kuwa ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Kwame Nkuruma, Jomo Kenyata, Nandi Azikiwe na Sengho.
Kampeni ya kutaka julai 18 ambayo ni siku ya kuzaliwa Nelson Mandela, itambuliwe kama siku kimataifa ya Nelson Mandela ilianzishwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Nelson Mandela Foundation , kwa kushirikiana na wadau wengine.
Kampeni hiyo ilieendelezwa mwaka huu na ubalozi wa kudumu wa Afrika kusini katika umoja wa mataifa kwa kuanzisha mchakato wa utayarishaji wa azimio hilo ambalo baada ya kuungwa mkono na nchi wanachama wa umoja wa mataifa, hatimaye liwasilishwa katika Baraza Kuu ambapo limepitishwa rasmi.
Mbona Steve Biko akumbukwi?alipoteza maisha yake katika harkati za ukombozi.
ReplyDeleteSusan Rice alimsemaje, maana ninavyoelewa mimi bado wanamtambua kama Gaidi (inabidi senate ipitishe bill kumuondoa kwenye list). Anamkubali Obama hata hivyo.
ReplyDeleteKuna mganga mmoja kanituma nilete kwenu habari hii, amenituma anasema tuwe macho kwenye vyombo vya habari mwaka 2013 miezi ya March/April..kutakuwa kuna habari kubwa sana duniani ikitokea kusini na Magharibi ya Afrika.Dunia nzima itazizima!
ReplyDeleteHakutoa maelezo zaidi anasema yeye hatokuwepo duniani katika masiku hayo.Sisadikishe maneno yake ila naleta kwenu ujumbe huu na watu waje watoe ushuhuda kwenye blogu hii na ikibidi hii meseji iwekwe kama ukumbusho
Mjumbe hauwawi
hakika chema chajiuza. hao UN hawakumuona nyerere?
ReplyDeleteWELL,MANDELA MSHIKAJI WANGU LAKINI HIYO SIKU WANGEIFANYA WASOUTH AFRICA KIVYAO KWANI AKUNA UMUHIMU WA DUNIA NZIMA KUSEMA SIKU YA MANDELA DUNIANI.KWANI KUNA MAFREEDOM FIGHTERS KIBAO DUNIANI.
ReplyDeleteMDAU MONEY UK,
Kweli nakumbuka pale Mazimbo Morogoro tulipowalea na kuwahifadhi vyema wana ANC.
ReplyDeleteJamani, Mandela na A/Kusini wangestahili kumpa Nyerere heshima anayostahili katika harakati za ukombozi wao.
Ilifika wakati tukawa tunalalamika kuwa Wakimbizi wa A/Kusini toka Mazimbo ndio wanaonekana Morogoro mjini kama wenye nchi na sisi ndio Wakimbizi maana walikuwa wanavaa nguo nzuri za kupendeza na wana mpaka sports bykes wakati sisi tunatembea na midabwada kwa miguu!
Chuo chao (Mazimbo) kilikuwa kisafi na misosi ya nguvu kuliko Moro Agri. University au hata mlimani na hata vifaa vya michezo na mziki ulikuwa hupimi hapo.
Mnaomponda Nyerere mna haki zenu ambazo sisi hatuzijui pengine aliwazuia ninyi au wazazi wenu wasifisadi nchi kwa manufaa yetu sisi wote.
The united nations sucks! sikubali kabisa dunia nzima eti tumkumbuke Mandela. Kaifanyia nini Afrika hukimlinganisha na Nyerere?.Afrika kusini pekee ndio wawe na siku ya kumbukumbu yake sio dunia nzima.Nyerere amechangia kwa kiasi kikubwa uhuru na ukombozi wa Afrika lakini HAKUMBUKWI.Hata ndio sababu watu kadhaa wanamlalamikia Nyerere kwa kuisacrifice nchi kwa ajili ya ukombozi wa nchi nyingine.
ReplyDelete