MKUGENZI Mkuu Mtendaji wa shirikisho ya mpira wa miguu la mji wa Kent nchini Uingereza, Keith Masters ( wapili kushoto) akifuatilia kwa makini mchezo wa soka baina ya timu ya Veterani ya Mtibwa Sugar na timu ya Viongozi wa CCM wa Wilaya ya Mvomero, wakiwemo Madiwani mara baada ya kukabidhi msaada wa vifaa vya michezo ikiwemo mpira na jezi kwa Kata 17 za Wilaya hiyo wakati wa halfa ya Bonaza la Michezo ililioandaliwa kwa ajili ya makabidhiano ya vifaa hivyo, timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
MKUGENZI Mkuu Mtendaji wa shirikisho ya mpira wa miguu la mji wa Kent nchini Uingereza, Keith Masters ( wapili kushoto ) akizikagua timu ya soka ya veterani wa Mtibwa Sugar na ya Viongozi wa CCM wakiwemo Madiwani , kwanza kushoto ni Katibu wa Uchumi na Fedha wa Taifa wa CCM, Amos Makalla, mchezo huo uliandaliwa rasmi kwa ajili ya makabidhiano ya vifaa vya michezo kutoka kwa mfadhili Keith Masters wa nchini Uingereza, timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
MKUGENZI Mkuu Mtendaji wa shirikisho ya mpira wa miguu la mji wa Kent nchini Uingereza, Keith Masters ( wapili kushoto) akimkabidhi vifaa vya michezo Diwani wa Kata ya Tchenzema, Modesta Lubakiji ( kulia) , wa kwanza kushoto kwa Masters ni Katibu wa Uchumi na Fedha wa Taifa wa CCM, Amos Makalla, wakati wa halfa ya Bonaza la Michezo ililioandaliwa kwa ajili ya makabidhiano ya vifaa hivyo, kila kata ilipata jezi jozi mbili na mipira mitatu.
Picha na mdau wa mji kasoro bahari John Nditi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...