Rais Rupiah Banda wa Zambia ambaye pia ni mwenyekiti wa Sekretarieti ya nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) akiwa na mwenyeji wa mkutano wa nchi hizo Pierre Nkurunzinza wa Burundi, Makamu wa Rais wa Kenya Mh. Kilonzo Musyoki na Katibu Mtendaji wa ICGLR Balozi Liberata Mulamula katika kikao cha asubuhi na wafadhili pamoja na viongozi wa nchi wanachama jijini Bujumbura ambako kulifanyika mkutano wa mstakabali wa amani, usalama na maendeleo ya eneo hilo uliomalizika Ijumaa. Pamoja na mambo mengine mkutano huo umeiagiza ICGLR kuhamasisha na kuratibu juhudi zote za kuleta maendeleo, usalama na amani katika Maziwa Makuu na kutaja vipaumbele vitavyogharamiwa na michango wa wahisani na nchi wanachama.
Balozi Liberata Mulamula akiwa na viongozi wa nchi za Maziwa Makuu wakiwasili kwenye kikao cha asubuhi cha mstakabali wa ICGLR jijini Bujumbura
Balozi Liberata Mulamula akiwa na Marais Rupia Banda wa Zambia na mwenyeji wao Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi kabla ya kuanza kikao cha siku ya pili cha ICGLR jijini Bujumbura. Shoto ni Rais wa Benki ya Afrika, Dk. Bernard Kaberuka
Balozi Liberata Mulamula akipongezwa na marais Rupiah Banda wa Zambia (shoto) na Pierre Nkrunzinza kwa kuandaa mkutano uliofana na ICGLR jijini Bujumbura leo




Bungeni: Richmond yalala doro
ReplyDeleteNa Mwandishi wetu
6th November 2009B
Sakata la mkataba tata wa kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Richmond, limelala doro tena.
Hiyo inatokana na ukweli kuwa Bunge litaahirishwa bila Serikali kutoa taarifa juu ya utekelezaji wa maazimio 23 yaliyotolewa na chombo hicho.
Kwa mujibu wa ratiba ya shughuli za Bunge iliyotolewa leo asubuhi, kikao kilitarajiwa kuahirishwa leo na wala hakuna muda uliopangwa kwa ajili ya Serikali kutoa taarifa hiyo. Badala yake ratiba ilionyesha nafasi ya Waziri Mkuu , Mheshimiwa Mizengo Pinda kuahirisha Bunge.
Taarifa hiyo ya Serikali kuhusu Richmond, ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wabunge wengi pamoja na wananchi kwa ujumla ili kujua nini kimefanyika kuhusiana na maazimio hayo 23.
Miongoni mwa maazimio hayo ni lile la kutaka Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa nchini (TAKUKURU), kutakiwa kujiuzulu kutokana na kashfa hiyo ya mkataba tata.
Picha ya kwanza juu, naona mtasha wa kwanza kulia kauchapa usingizi kama vile kingunge wa bongo anasubiri muda wa posho tu...wizi mtupu
ReplyDeleteHuyu mama ni kichwa safi kwani tulipokuwa naye NY,NY enzi za balozi Mwakawago tuliona vitu vyake.Go mama Mulamula go.....?
ReplyDeleteHiyo ndio vakesheni ya mkuu wa nanihii huko burundi
ReplyDeletekila safari yake yeye ni vakesheni hasemi kama anaenda kupiga picha wakubwa na kuchukua habari ndio kibarua chake cha kumuweka mjini
yeye anasema vakesheni na fulana yake ya kichawi aliyopewa na mganga wake kama sindiko
haya mkuu wa nanihii weka wazi ajira yako ieleweke kwani unawapotosha jamii kwa kusema unaenda vakesheni na kumbe ni safari za kikazi.
Lakini kwenye kamkutano ka asasi za jamii kule finland mwaka fulani alijaza watu wa kasehemu kamoja tu na hata mzazi!
ReplyDeleteMmmh!! huyu Anonymous wa Sat Nov 07, 02:20:00 PM
ReplyDeleteInaonekana hizi vekesheni za mkuu wetu zinamkereketa kweli kweli....Anyway ndo binadam tulivyo!!
Mheshimiwa balozi kula vekesheni baba,na utuhabarishe zaidi na zaidi.
mkubwa ni kalonzo musyoka sio kalonzi musyoki.
ReplyDelete