BENDERA ya Taifa iliyokimbizwa kwa miguu na wanariadha nyota kwa siku
tano mfululizo, hatimaye jana ilifika kileleni mwa mlima mrefu kuliko
yote barani Afrika, Mlima Kilimanjaro na kusimikwa rasmi kwenye kilele
cha Uhuru kilichopo umbali wa mita 5895 (futi 19,331) kutoka usawa wa bahari.
Mwanamichezo mwenye uzoefu wa aina yake katika kuupanda mlima huo,
Elly Gerald Minja ndiye aliyeifikisha bendera hiyo mapema leo
asubuhi.

Mbali ya Minja mkazi wa mkoani Kilimanjaro, wanariadha mashujaa
walioandika historia ya kuzindua mbio hizo za aina yake nchini
walikimbiza bendera huku wakipokezana kila baada ya kilomita kati ya
10 na 15 kutoka Dar es Salaam hadi Marangu, Moshi mkoani Kilimanjaro
tangu Jumapili iliyopita.
Zaidi ya wanariadha 70 nchini, wengi wakiwa wa kimataifa walikimbiza
bendera hiyo kwa zaidi ya kilomita 567. Walifika Marangu Alhamisi
jioni na siku iliyofuata baadhi yao walianza kuipandisha Mlima
Kilimanjaro bendera hiyo ambayo mbio zake zimeasisiwa na kudhaminiwa
na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro.
Nyota kama Francis Naali na binti yake, Mary Naali aliyeipa Tanzania
medali ya shaba katika michezo ya Olimpiki iliyofanyika Beijing,
China, Samwel Mwera, Sarah Maja walikuwa kivutio kikubwa kama
ilivyokuwa kwa Peter Pallagyo, mkongwe mwenye umri wa miaka 50 na
malemavu wa mikono aliyewaikilisha nchi katika michuano ya Olimpiki na
Jumuiya ya Madola, Joro Mathias.

Akiwa mwenye furaha isiyo kifani mara baada ya wanariadha kufika
Marangu, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe alisema
amefurahishwa na jinsi Watanzania walivyozipokea mbio hizo za aina
yake nchini.
“Ninawashukuru ndugu zangu Watanzania kwa sababu bila ya ninyi kamwe
tusingefika hapa, asanteni kwa kuwaunga mkono wanariadha waliokimbia
kwa umbali mrefu kutoka Dar es Salaam hadi hapa, na asanteni kwa
kuiunga mkono Bia ya Kilimanjaro…tunaahidi kuendelea kuwafanya makubwa
zaidi Watanzania…
“Tunajivunia mlima mrefu kuliko yote Afrika na tunajivunia bia yetu ya
Kilimanjaro…hatuna budi kuungana kuvitangaza vivutio vyetu,”
alisisitiza Kavishe huku akielezea umuhimu wa mbio hizo zilizopewa
jina la “Fikisha Tanzania Katika Hatua za Juu”.
Licha ya kuanzisha na kudhamini mbio hizo za kwanza za aina yake
nchini, kwa karibu muongo mmoja sasa Bia ya Kilimanjaro imekuwa mstari
wa mbele katika kudhamini michezo mingine nchini.
Bia hiyo, ndiyo inayozidhamini klabu kongwe na maarufu zaidi katika
soka nchini, Simba na Yanga ikiwa inabeba jukumu la kulipa mishahara
ya wachezaji, makocha na viongozi. Inamwaga pia vifaa vya michezo kwa
klabu hizo.
Pia ni wadhamini wa muda mrefu wa mbio za kimataifa za Marathoni za
Kilimanjaro na zile zinazoshirikisha wanariadha kutoka zaidi ya nchi
25 duniani.
Hata linapokuja katika suala la kutambua umuhimu wa sekta ya muziki
nchini, Bia ya Kilimanjaro ndiyo kinara, kwani kila mwaka imekuwa
ikimwaga mamilioni ya shilingi kudhamini Tuzo za Muziki za
Kilimanjaro.
Imekuwa pia ikidhamini michuano ya mpira wa kikapu ya
mkoani Dar es Salaam `RBA Kili’.
mkoani Dar es Salaam `RBA Kili’.
Balozi wa nanihii, hivi ni futi 5895 au ni mita 5895 kutoka usawa wa bahari (a.s.l)?
ReplyDeleteRekebisha haraka haraka kabla watoto wetu hawajalishwa "kasa". Ni MITA 5895 siyo futi!! Kha!
ReplyDeleteMichuzi, tafadhali tuwekee picha za hiyo bendera kufikishwa kileleni..
ReplyDelete