Home
Unlabelled
ndolela chaseleleka
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
...Simon Cowell may disagree, but this is what I call natural talent. A born artist who brings old memories flooding back - good ones...Keep it up Maringo.
ReplyDeleteEchilato nicho chi tali cha bhajita go! aha awo niwo uchemushga wa mai!
ReplyDeleteduh nimekipenda hicho kiatu alichovaa, usifanye mchezo utadhani kimetoka ile fassi ya pariii,
ReplyDeleteDuh! Mzee huyu kiatu chake kinanikumbusha kitabu nilichosoma zamani cha "Mpiga Filimbi Wa Hamelini", aliyehamisha panya wote waliokuwa wakila mazao ya wanakijiji kimoja enzi hizo.
ReplyDeleteHe he he he heee
This Is Black=Blackmannen
I love maringo so much..especially na chaserereka..guy u defenetly wanna invite this guy in ur wedding....
ReplyDeleteBwana Maringo namkubali kwa sana kwani ameweza kuwatoa kimasomaso wajita ambao bahati mbaya kwa kipindi kirefu kimuziki hawakuwa wakijulikana kwa watanzania wenzao japo miaka ya sabini kuna mzee mmoja aliyekuwa akijulikana kwa jina la Nyang'omboli (sasa ni marehemu)alitamba sana Radio Tanzania enzi hizo na zeze lake.
ReplyDeleteLakini pamoja na kwamba Maringo amebahatika kuutambulisha muziki wa Wajita kwa watanzania na pia watanzania wakaaminishwa kuwa yeye ndiyo mtunzi wa nyimbo nyingi anazoimba na hasa ule ulio mararufu zaidi wa "NDOLELA CHASEREREKA" napenda kumkumbusha maringo na pia kuwambia watanzania wenzangu kwamba Maringo siyo mtunzi wa wimbo ndolela chaserereka. wimbo huo mimi binafsi nikiwa mdogo kabisa mwaka wa 1970 nimeukuta ukiimbwa maharusini na ukionekana kuwa ni wimbo wa siku nyingi uliokuwa umezoeleka kwa wajita wote. Nadhani hata Maringo mwenyewe wakati huo alikuwa hata hajazaliwa na nina hakika kuwa wajita wote wanafahamu hilo kuwa Maringo siyo mtunzi wa wimbo huo ila alichofanya yeye ni kuufanya wimbo kuwa maarufu tu kwa watanzania wengine na hasa baada ya kutumia vyombo vya kisasa na ukasikika katika radio na cd na kanda.
Nimeshawishika kutoa ufafanuzi huu kwani Maringo amekuwa akitajwa katika vyombo vya habari kwamba ndiye mtunzi na muimbaji wa wimbo huo wakati ukweli ni kwamba yeye siyo mtunzi wa wimbo husika,
Pia nakumbuka kuna mwanamuziki Fadhili William (marehemu) wa Kenya alivyokuja kupata umaarufu kwa kuonekaan kuwa ndiye mtunzi wa wimbo maarufu wa Malaika ambao wanamuziki wengine maarufu kimataifa kama Boney M, Miriam Makeba, Eddy Grant n.k waliuiga na wakawa wanalipa pesa nyingi kwa Fadhil William kwa mujibu wa masuala ya hakimiliki.Lakini kumbe mtunzi wa wimbo huo wa malaika hakuwa yeye Fadhili bali mzee mmoja wa kichaga (mtanzania)aliyekuwa kautunga na kumwimbia binamu yake aliyetamani kumwoa na kumfanya mkewe huyo binamu yake.Na Fadhili akaupenda wimbo baada ya kuwa akiusikia wimbo huo kwenye vilabu vya huko Moshi/Arusha wakati ukiimbwa na huyo mzee wakichaga na akiwa kwao Kenya akafanya ujanja wake na akapata hakimiliki ya wimbo.
Pia kuna nyimbo kadhaa ambazo Maringo amezikuta zikiwa tayari ni maarufu ambazo zilitungwa na kuimbwa na wanamuziki wengine wa kijita walimtangulia kama Lubhali (huyu alikuwa ndiye maarufu zaidi), Wasaga, Musoke n.k.
Kwa ujumla ninapoandika hapa sina maana ya kumshushia heshima Bwana Maringo kwani na mimi ni mmoja wa wanaomkubali sana kwa utunzi na uimbaji wake (ukiondoa hizo nyimbo ambazo amenakili kwa wanamuziki wa kijita waliomtangulia) lakini mimi ninachojaribu kukionyesha hapa ni kuhusu huko mbele ya safari litakapojitokeza suala la hakimiliki ya nyimbo kama hizo ambazo sasa zinajikuta zikipata kasi ya umaarufu na mtu fulani kuhesabika kama ndiye mtunzi wa wimbo wakati sivyo.
Pia ikumbukwe kwamba maringo siyo wa kwanza kunakili nyimbo zilizo maarufu katika kabila la kijita kwani kuna wengine kama Chime na Ya Leo Kali ambao nao wanapiga muziki mzuri uliojaa vionjo vya kijita ambao ndani yake unakuwa umejaa gitaa la galatone, mlio wa chupa ya fanta inayosuguliwa na msumari n.k na mara nyingi wakiimba visa vya matukio ya kweli ambayo yamepata kutokea katika vijiji mbalimbali vinavyokaliwa na wajita, kama vile vifo, njaa, fumanizi, kufanya mapenzi kwenye mashamba ya mihogo(nyugunyugu),wanandoa kuachanan.k na mara nyingi wakitaja majina ya wahusika wa matukio hayo waziwazi.
Yangu ni hayo, otherwise big up sana kwa bwana Maringo.
Abhajita amwi nayabha ukwaika kutyo bhana bhasu? Labha nayabha enisabhwa mufwile chigongo.
What has been written by anony Tue 17 09:12 am is absolutely true.
ReplyDeleteHata wimbo wa omlembo msononoko ni wimbo wa siku nyingi sana na haukutungwa na Maringo. pengine ni kutokana na mazingira halisi ya watanzania watu kutojua sheria ya hakimiliki na faida zake na pia kutokuwa wafuatiliji wa mambo. Unakuta watu wanatunga nyimbo zao nzuri zinazokubalika katika jamii. Matokeo yake hakuna wanachofaidika nacho na wao wanabaki nakiangalia nyimbo zao zikipaa tu kwenye umaarufu bila kufikiria mbele zaidi
kuhusu watakavyofaidika na nyimbo hizo tena ikiwa ni kiijini ndiyo kabisaaaa.. Na wajanja wanawahi.
Kwa mawazo yangu Maringo ndio ameleta hiyo miziki ya jadi mainstream na watu kama sisi tumeweza kusikia na kumuona anafaa na hii ndio kazi yake sasa kuanza kuongelea haki ooooh nyimbo zimetungwa kijijini na watu wengine Maringo hizo ni feelings tu jamaa yupo kazini anakubalika na sisi akina Binti wa Mugango Coast Village aka Mara vijijini tunampa shavu sana tu... Ni watu wachache wanaoendeleza mila zetu za ki-Africa ni bora kumpa shavu kuliko wakina yo yo yo what's up kibao tunaowapa shavu pia ila ndio hivyo tena mila zinapotea!
ReplyDeleteWakondya mwana wasu!
Ni Mtazamo tu :-)
Pamoja na masifa yanayotolewa kwa Bw. Maringo kwa kufanya kile kinachoitwa Ujanja ni Kuwahi kama si kupata, Mimi bado sijaukubali usanii wa huyu Mheshimiwa. Kwani tungependa kuona kama si kusikia vitu vipya vya kijita, kikwaya kiruri n.k na si kuendelea kutukwaza hasa siye watu wa enzi hizo ambapo harusi zote zilitumbuizwa kwa nyimbo hizo na maharusi kutembea umbali mrefu bila hata kuchoka. Bw. Maringo pamoja na maboresho unayoyafanya kwenye nyimbo za zamani na kwa kuwa umeingia kwenye fani hiyo ya sanaa, hebu jaribu kuifanya iwe kazi ya Sanaa kweli ili wadau tupate raha zaidi. NI HAYO TU.
ReplyDeleteEti mUgango coast wakumbusha kula mwana wasu..kila mmoja anajua awe mjita, mruri, mkwaya au aje kwamba nyimbo hajatunga maringo ila tumpe credit kwamba kazifikisha hapo zilipo wengine tumezaliwa tumezikuta, na wengine basi kuzeni mbegete, jombole, na wale wakerewe vidogoli ili mamabo yawe safi..kuhusu suala la hakimiliki hapo tena utata aliyeutunga sijui hata kama bado yupo manake hizi nyimbo za long kishenzi..kina kanyoni ka mulutanga..wengine tuliimba wakati tunaamia ndege na sasa ndo ziko juu..
ReplyDeletepamaoja na yote tumpe credit tu..
ila kaka maringo sasa tunga mpya nyingine basi watu tuendelee kula raha manake siku hizi hata harusi za wasukuma ndoleala ipo..ahh omwana unu uli kula wa mayi...teh teh
Aiyaoyeeee mai awe aiyaoeeee aaaah,aiyaoyeeeh mai awe nina mawazo mumwoyoo!
ReplyDeleteUtalola okwonda mai-awe nuwitogela ndwae-aaaaah, utalola okwonda mai-awe nina mawazo mmwoyo! (usione ninakonda mpenzi ikadhani naumwa, mwenzio nina mawazo moyoni)
yaani huu wimbo kila nikiukumbuka napata hamu ya kwenda kusalimia ndugu zangu huko majita. Kweli miziki ya asili ina nafasi kubwa katika maisha yetu. Wanaosahau asili yao wajilaumu.
Watu wengine mkoje?mbona mna roho za kwanini?hata kama hajatunga yeye bila yeye kuuboresha huo mwimbo wengine tungeujuaje?au mnafikiri kila mtu ni mjita,mmekazana ooh uliimbwa zamani..na hiki na kile mbona hamkuuboresha sasa.
ReplyDeletetubadilike jamani,mtu akifanya kitu kizuri apewe sifa zake.....huyu jamaa amenifanya hata mimi mchaga niupende na kuucheza nikisikia unapigwa kwenye radio au harusi za wajita.
kwakifupi hata kama hajatunga yeye ,mkubali tu ndio yeye ameutoa kimasomaso!!
Big up mkuu!!..ila usibweteke,ongeza na nyimbo zako nyingine.