Save Albino Benefit Concert ilioandaliwa na Babu Sikare anayekwenda kwa jina la Albino Fulani ambaye ni msanii, muigizaji na CEO wa Afrobino.Inc.(WWW.AFROBINO.ORG) iliyofanyika huko Columbus, Ohio, ilifana kupita kiasi ambapo watu wengi walijitokeza kutumbuizwa na wasanii mbalimbali kutoka Tanzania, Kenya na Zambia.

Akihojiwa na mtangazaji wa VOA Sunday Shomari, bwana Sikare alitoa shukurani za dhati kwa wote waliohudhuria na kutoa ushirikiano wa hali juu kufanikisha shughuli hiyo. Aliongeza kuwa imefika wakati kwa wasanii kutumia vipaji vyao kusaidia kwa namna moja ama nyingine watu wanaohitaji misaada katika jamii.

Alitoa shukurani za dhati pia kwa kampuni ya Walgreens Pharmacy ya Marekani ambao walitoa bei poa ya mafuta ya kinga ya jua kwa watoto wenye ualbino yaliyonunuliwa.

Mafuta hayo yatakwenda kusaidia watoto kuanzia miaka 5-10 na yatakabidhiwa kwa chama cha maalbino Tanzania hivi karibuni.

Albino Fulani akiwa na Chino toka Zambia wakitumbuiza
mashabiki wakishangilia



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. kwa kweli mie namzimikia saana albino flani yuko juu anang'aaa na mchuchuuu yani acha tu kitu kimetulia sana. we michuzi leo usiibane hii acha tu ajue walimwengu huku hatujiwezi ni hayo tu meseji hii ifike bila kwakwaru hata we michuzi ni handsome kama p didi na tuna kuluv kwa sana tuu ila mie kwa albino wa ukweli nimefika
    mdau canada

    ReplyDelete
  2. Michuzi naomba sana sana sana unipatie contacts za huyu Albino Fulani na unihakikishie kuwa hana mke, nataka nimuenzi kama mboni ya jicho langu.

    ReplyDelete
  3. Albino kaka ninakuaminia sanaaaaaaa.... wasanii igeni mifano sio kukalia ngono, bangi, kunusa na ulevi!!!

    ReplyDelete
  4. Albino ukija home ntakupikia ugali na dagaa kwa kanzi nzito uliyoifanya, mume wangu itabidi akae kando kidoooggoooo....nnakufia!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...