Jumamosi hii familia ya marehemu Profesa Haroub Othman itasherehekea siku ya kuzaliw kwa mwanazuoni huyo aliyefariki mapema mwaka huu kwa kujenga choo na maabara katika shule ya msingi ya Msasani jijini Dar na wadau wote tumealikwa kushiriki harambee hiyo itayoanza asubuhi hiyo siku ya jumamosi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Nadhani kujenga choo kama kumbukumbu ya Profesa Haroub Othman ni kutokumtendea haki kabisa.

    Prof Haroub Othman was a famous academician who contributed a lot in his area of specialisation and in community development, especially in Zanzibar and Middle East politics, so to build a toilet as a symbol of his birthday anniversary is a shame. Big thing should be done to remember him. I agree with idea of laboratory not the toilet.

    I do not know why you people want to build the toilet in the name of this great academician. May be the toilet has been considered because of lack of enough funds that could be used to construct a better thing. I suggest if problem is money, instead of using his name to build the toilet, people involved in this event should lay foundation of some classrooms which can be finished in the future.

    Please note my argument is not that the toilet is unimportant thing rather my point is to avoid honouring Professor with the toilet. If school does not have a deceit toilet well and good you can build it but please do not do so in the name of this great man.

    ReplyDelete
  2. German goalkeeper kills self by stepping in front of train, police say...http://www.cnn.com/2009/WORLD/europe/11/11/soccer.goalkeeper.suicide/index.html

    ReplyDelete
  3. Anonymous wa 12:20 nashukuru sana kwa mchango wako. Hatujachelew kufanya zaidi kwa jina la profesa, tunakukaribisha ushirikiane nasi. A toilet is what we thought was urgently needed and so we started with the toilet. It made more sense to start with something that will help more than a 1000 kids and finish it than aim to start something bigger and end half way. Our aim is to do something to the community and no matter how big or small one is a toilet is very important. We have also started rehabilitating an abandoned classroom to turn it into a library and classroom. We are also hoping to rally more funds and finish the audiology room for the deaf which was left half way (as would have been the classroom you proposed). Haroub didn't become a well known academician overnight and Inshallah we do have more years to celebrate his life. We have started polepole, brick by brick and we will be more than honored to join your efforts of building a better Tanzania wherever they are.
    Pamoja we can.

    tahir haroub othman
    joinus@haroubothman.org

    ReplyDelete
  4. Sasa Michu umepost hii comment ya goalkeeper hapa!!!!!!!!what it relationship between German goalkeeper suicide and late prof Othman birthday anniversary?????

    ReplyDelete
  5. Tahir,

    Nami pia nakubaliana na wazo kuwa kujenga choo kwa kumbukumbu ya Prof. si wazo zuri sana, nafikiri hilo wazo la jiwe la msingi lingekua zuri zaidi na fund raising ianze mara moja kwa ajili ya ujenzi wa jengo kamili,

    Sioni ugumu wa kukusanya funds kwa ajili ya project kama hii, kwani walioguswa na kazi za Prof. ni wengi mno, ni suala la kuwa strategic kwenye ku publicise tu, magazeti, redio, mtandao kama hivi n.k

    Aidha, kwa ufahamu tu, kwanini mlichangua shule ya MSasani? isingekua vyema kufanya hivyo kwenye shule ya kijiji alichozaliwa au aliyosoma Prof.

    Na kwa watakaoshindwa kuhudhuria tukio la jumamosi, je wanaweza kuwasilisha mchango wao namna gani?

    Mwisho, zoezi hili liwe endelevu sio la mwaka huu tu

    Mwanafunzi wa Prof,
    UDSM

    ReplyDelete
  6. Nadhani hamumtendei haki Prof Haroub Othman.

    Pamoja na umahiri wake katika uchambuzi wa mambo ya kisiasa, na umaarufu wake katika nchi mbalimbali, alikuwa hapendi kujikuza wala kutukuzwa--hiyo ndo ilikuwa mila yake. Tuienzi kwa kufanya mambo yake katika jamii yake.

    Kumuweka kwenye mitandao kutaamsha hisia mbaya katika baadhi ya watu, na inaweza kuleta picha tofauti.

    Yote mnayofanya hadharani kwa jina lake yaweza yakawa yawahusu ninyi, yake myafanye kwa ukimya naofanana na maisha yake.

    Samahani kama maneno yangu yamewakera.

    ReplyDelete
  7. Mwanafunzi wa Prof,
    Nashukuru sana kwa mchango wako. Nakumbuka nilivyokuwa mtoto miaka ya 80, mzee alinichukua katika matembezi ya hisani kujenga library Zanzibar, last weekend nimepita na kuona ndio wamemaliza kujenga 1 storey building decades later. Dhumuni la kujenga vyoo, library, kukarabati darasa na Inshallah kumalizia audiology rooms ni kusheherekea birthday ya 67 ya mzee na si kusheherekea maisha yake yote. Tunategemea tuwe tumemaliza shughuli hizi ifikapo tarehe 30 Novemba siku ya kuzaliwa mzee. Ilikuwa uamuzi wetu kufanya kitu ambacho nunaamini tunaweza kukisimamia hadi mwisho wake tukishirikiana na nyinyi marafiki na wazazi wa shule na kusaidia kuonyesha jamii kwamba si kila kitu kiachwe kufanywa na Serikali. Come January the kids will have their own toilets, library and an extra classroom, its not much but its the first brick. Nakubali makubwa zaidi yanaweza kufanywa lakini katika hilo wewe huwezi kuwa mtazamaji, standup and do your part and we will rally behind you.
    Kwa jinsi gani unaweza kuchangia tafadhali tuandikie joinus@haroubothman.org

    ReplyDelete
  8. Nakumbuka kumsikiliza sana Profesa na kusoma articles zake kwenye magazeti na mtandao. Nashukuru kwa mchacho wake.

    Kwangu naelewa uamuzi wenu wa kutaka kufanya project ambayo mnaimaliza mapema, lakini kama wengine ilivyosema inshallah itapatikana project kubwa zaidi siku za mbele. Wengine wanaweza wakawa wanaoverlook umuhimu wa choo kwa shule hiyo hata hivyo. Nitawasiliana na nyinyi.

    Kingine, kwenye kitabu cha Godrey Mwakikagile aligusia kwamba Profesa alikuwa anashirikiana na Profesa Ahmed Mohiddin na Ferdinand Ruhinda kuandika biography ya Mwalimu Nyerere kabla Mwalimu hajafariki. Unaweza kutugusia kama kuna siku kazi ile inaweza kuja kutoka?

    ReplyDelete
  9. Sijui kama maprofesa Haroub Othman na Ahmed Mohiddin, pamoja na Ferdinand Ruhinda, walianza kuandika kitabu hicho, biography ya Mwalimu Nyerere.

    Mimi pia nimesoma kitabu cha Godfrey Mwakikagile, "Nyerere and Africa: End of an Era," Fourth Edition, ambamo ameandika mengi kuhusu maisha ya Mwalimu tangu utotoni. Ikiwa bado hujafanya hivyo, soma edition ya nne ya kitabu hicho. Kuna mengi zaidi kuhusu Mwalimu katika edition hiyo kuliko yaliyomo katika edition zingine zilizotangulia.

    Pia Godfrey Mwakikagile amesema mwanzoni mwa kitabu hicho, "Nyerere and Africa: End of an Era," kwamba Andrew Nyerere alimwambia dada yake, Anna Nyerere, alikuwa anakusanya details mbali mbali kuhusu baba yao Mwalimu Nyerere. Sijui kama kusudi la dada huyo ni kuandika kitabu kuhusu baba yao au vipi. Ukiweza kuwasiliana naye, muulize.

    Haroub Othman, Ahmed Mohiddin, na Ferdinand Ruhinda walisema nini kuhusu suala hilo?

    Nimesoma mtandaoni, pamoja na Jamii Forums, kwamba Professor Haroub Othman alisoma kitabu cha Godfrey Mwakikagile, "Nyerere and Africa: End of an Era." Labda pia Ahmed Mohiddin na Ferdinand Ruhinda walisoma kitabu hicho. Lakini sijui kama kuna mtu aliwahi kuwauliza kama bado walikusudia kuandika biography ya Mwalimu Nyerere.

    Waulizwe, pamoja na Anna Nyerere.

    Kitabu cha Godfrey Mwakikagile kina biographical information nyingi kuhusu Mwalimu Nyerere. Lakini sidhani kina details za kutosha kama zile ambazo akina Haroub Othman, Ahmed Mohiddin, Ferdinand Ruhinda, na Anna Nyerere wangeweza kuzikusanya na kuziandika.

    Walio hai kati ya hao waulizwe wamefanya ni na wanakusudia kufanya nini kuhusu biography ya Mwalimu Nyerere.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...