
Washindi wa Miss Utalii Ilala 2009- Shaymaa NTEMENA (Kati) mshindi wa pili Aghata Kilala (kulia) na mshindi wa Tatu Sheila Baha
Wasomi wengi mwaka huu wamemejitokeza kushiriki katika mashindano ya Miss Utalii Tanzania, na kutwa mataji karibu yote katika ngazi mbalimbali za mikoa,Wilaya, na Kanda ambazo tayari zimekwisha fanya mashindano yake mwaka huu.
kama ilivyokuwa katika shindano la Miss Utalii temeke 2009, ambapo mrembo mwenye Digrii ya Uhasibu na Utawala wa Fedha Erica Allan, alipotwaa taji la Miss Utalii Temeke 2009/2010, jana Msomi mwingine mwenye shahada ya Sayansi ya Komputa, Shaymaa Ntetema aliweza kutwaa taji la miss Utalii Ilala 2009/2010 katika fainal iliyofanyika katika ukumbi wa Da' West Park Inn Tabata, Dar es Salaam.
Huku mwanafunzi wa Digrii ya Sayansi ya Jamii katika chuo Kikuu Shiriki cha Sayansi ya Jamii (Ustawi wa Jamii) Kijitonyama , Aghata Kilala aliweza kutwaa nafasi ya Pili akifutiwa na Sheila Bahamary , Mwanafunzi wa Shahada ya Juu ya Uhandishi wa Habari katika chuo cha DSJ.
nafasi ya nne ilitwaliwa na Tausi Thomasi mwenye Elimu ya Kitato cha Sita huku nafasi ya tano na taji la kipaji likitwaliwa na Mwanafunzi wa Kozi za awali za Komputa, Jamida Abdu.ambapo katika shindano hilo warembo wote walipita kwa mavazi mbalimbali likiwemo a Asili ambalo pia walilitumia kama ngao ya Asili kwa kuchezea ngoma ya tamaduni za makabila ya Tanzania.
aidha warembo waliweza kujibu maswali mbalimbali yanayohusiana na Utalii, Mila na Desturi, Vivutio vya Utalii na Hifadhi za Taifa za Utalii, Mikoa na Tamaduni mbalimbali, ikiwemo kuimba nyimbo za Tanzania.
washiriki wengine walioingia katika kinyang'anyiro hicho ni pamoja na Tickey Lithon, Frola Nicholuas, Janneth Samson, Edna Endrew, Nezia Mangaka, ambapo shindano hilo lilipambwa na wanamuziki wengi wakiwapo bendi ya Extra Bongo chini yake ally Choki, Zia Musiki, Kundi la Muziki la Ngoma za Asili, Mfalme Bendi chini yake Costar Siboka, pamoja na wanamuziki wa Kizazi Kipya, Abubakary Msasu(Kiboot) ambaye hata hivyo alichelewa kuingia Ukumbini.
kwa mujibu wa Waandaaji wa mashindano hayo, sasa shindano ambalo linatazamiwa kufana kwa aina yake ni shindano la Miss Utalii Kinondoni, ambalo limesheheni wasomi wengi kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali ikiwemo, chiuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mzumbe, IFM, CBE, na Vingine Vingi
Mgeni Rasmi katika Shindano hilo alikuwa Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mwantumu Mohamed, huku wadhamini wa shindano hilo Kampuni ya Mlonge by Makai Enterprises wakiweza kukabidhi zawadi kwa washindi zilizokabidhiwa na Afisa Utamaduni wilaya ya Ilala Shani Mohamed.
jamani vigezo vya miss utalii...sina hamu!!haya natuone
ReplyDeleteuwo unga au poda usoni ni hatari! du wanatisha! wamekuwa kama wametoka kwenye jango fulani hivi! hongereni anyway na poleni sana.
ReplyDeleteHAHAHAHAH.....mbavu zangu mie!
ReplyDeleteWadau umewaona mamisi wetu. Niliposema mitoto ya kihabeshi mwisho nikaonekana nimedata.
ReplyDeleteWanatesa na manywele ya kubandika. Mimi ndio maana nikatafuta shombe nikao sina gharama za kununua mikorogo wala minywele ya kubandika.
Wabantu wenzangu amkeni hatma ya usawa aliokua akilia mpaka kufa kwa nyerere umeshafika.
kaazi kweli kweli!
ReplyDeleteHuyo Samenya toka Afrika ya Kusini wa kati ktk photo ametua lini Bongo?
ReplyDeleteMmmmmmmmmh wajameni,haya.
ReplyDeleteSi ajabu wasichana wa watu ni wazuri sana tu lakini camera za china ndio matatizo yake hayo.
ReplyDeleteIla huyo wa kati makeup imezidi...wakulia nimempenda naturali
Mademu wengi waliokula nondo sana huwa hawalipi kabisa,kwanza hawa cha mtoto mi nakula masters hapa aisee hawa mademu classmates duh wakali ni wawili tu alafu wameolewa waliobaki tofauti na wanaume ni nguo tu.
ReplyDeleteukweli ni kwamba mabinti wa bongo wanazeeshwa bado wadogooo. ebu waone si kazi wana miaka 18 au 20. kazi kukimbilia vibabu matokeo yake ndo haya. kisa blueberry sijui rav4....haya sasa.
ReplyDeletemkereketwa
wewe anon wa nne Sat Nov 07, 11:57:00 PM unaosema kuhusu wahabeshi.
ReplyDeletehivi unafikiri watakutaka wewe nywele zako ngumu hata kama ni mwanaume? ungejua wanavyowadharau wanaume wengine waafrika wenye nywele kama zako, wanawaita "pua pana, nywele ngumu" pumbavuuu. nakunukuu tena "Wabantu wenzangu amkeni". Sasa unataka watu woote watafute hao mashombe halafu dada zako wasiolewe kamwe kwasababu tu ya nyele zao, mimi nataka kujua mama yako wewe nywele zake zikoje? and did your dad had a problem with it?
je wakina dada na wao waanze kutafuta wanaumwe wenye nywele za kuteleza au?
shika adabu yako its the beauty inside that counts.
go east go west home is always the best.
peace
mdau
Canada
Canada
Jamani.... mh, hiyo midomo na vipodozi ni mojawapo ya vigezo??????????????. Hapana kwa kweli.
ReplyDeleteJamani...kulikuwa na washiriki wengine au ni hawa hawa watatu? kama walikuwepo, sasa wao wakoje? manake hawa washindi hawajanishawishi kabisaaa...
ReplyDelete