Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini mchana wa leo, Jumamosi, Novemba 7, 2009, kwenda Misri kuhudhuria Mkutano wa Pili wa Ushirikiano Kati ya Afrika na China, ujulikanao kama Forum on China-Africa Cooperation.
Mkutano huo wa siku mbili, unaotarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wengi wa Afrika, umepangwa kuanza kesho, Jumapili, Novemba 8, 2009, kwenye mji wa Misri wa Sharm El Sheik.
Kwa mujibu wa ratiba za shughuli za Mkutano huo, Mhe. Rais Kikwete jioni ya leo, mara baada ya kuwasili Misri kwa Mkutano huo, amepangiwa kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa China, Mhe. Wen Jiabao kuhusu masuala mbali yanayohusu Mkutano huo, na yale ya mahusiano kati ya Tanzania na China.
Baada ya kumaliza Mkutano huo, Mhe. Rais Kikwete atafanya ziara rasmi ya siku mbili nchini Misri kwa mwaliko wa kiongozi wa nchi hiyo, Mhe. Hosni Mubarak.
Hiyo itakuwa ziara ya kwanza rasmi kufanywa na Mhe. Rais Kikwete katika Misri tokea achukue usukani wa kuiongoza Tanzania, Desemba, 2005.

Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Rais Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais Mubarak kuhusu masuala ya kimataifa na yale yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Misri.
Uhusiano huo ulianzishwa miaka mingi tokea enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Marehemu Abdel Gamal Nasser.
Tanzania na Misri zimekuwa zinashirikiana katika nyanja nyingi zikiwamo zile za afya, elimu, biashara, kilimo, na zinayo Tume ya Pamoja iliyoanzishwa mwaka 1989.
Chini ya Tume hiyo, Tanzania na Misri zimetiliana mikataba kadhaa ikiwa ni pamoja na ile ya ushirikiano katika sekta ya utalii, ushirikiano katika sekta ya habari, na ushirikiano katika utamaduni na sayansi.
Mikataba mingine ni ya ushirikiano katika masuala ya ufundi, ushirikiano katika masuala ya biashara, ushirikiano katika usafiri wa anga, na ushirikiano katika masuala ya uchumi na ufundi.
Ingawa Mhe. Rais Kikwete atakuwa anaitembelea rasmi Misri kwa mara ya kwanza, viongozi waliomtangulia katika uongozi wa juu wa Tanzania, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, na Mhe. Benjamin Mkapa walipata kuitembelea Misri.
Naye Rais Mubarak ameitembelea Tanzania mara mbili, mara ya kwanza, mwaka 1978, akiwa Makamu wa Rais, na mara ya pili Februari 5-7, 1984, akiwa tayari Rais wa nchi yake.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...